Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Kuna wakati tulikuwa wengi, wengine wakabadilika, wengine wakachoka na wengine wakakata tamaa wakaacha.
Tulijenga hoja pamoja, tulijadili kwa hoja, tuliikosoa serikali na hata vyama vya siasa kwa hoja nzito na lugha za kistaarabu, tuliishauri serikali, tulishauri vyama vya siasa, tuliwashauri viongozi wetu kwa hoja zenye ushawoshi na kueleweka vyema.
Leo hii ukileta mada inayojadili hoja au ushauri kwa serikali, viongozi au vyama, utajikuta unachangia mwenyewe. Watu hawataki tena kuumiza vichwa vyao.
Binafsi bado naamini tutatoka hapa tulipo kwa kuibua mijadala inayofikirisha, kumshauri viongozi, serikali na vyama, na kwa kukosoa kwa njia ambayo ni constructive. Bado naamini, kupoteza muda kwenye kujadili matukio, kulumbana, kulaumiana na kukashifiana hakuwezi kutufikisha popote.
Kwa upande wangu nitaendelea kufanya mambo hata hata kama nitabaki peke yangu, naamini maadam naamini Niko sahihi na ninachohamasisha na kifanya ni kitu kizuri, IPO siku matunda yatapatikana, sitarudi nyuma nitasonga mbele kama so Leo nasi kesho, mabadiliko yataonekana. Kama nawe una imani juu ya jambo lolote zuri, lisimamie hata kama utabaki peke yako, IPO siku utafanikiwa.