Hata kama niko ndani ya CCM, nitaziita kuwa hizi ndio siasa uchwara

Sitachangia lolote lakini 2020 kazi ipo sabb wanafiki wa sasa na wale wenye chama chao wataona hawana cha kupoteza zaidi ya kumuonyesha mwenyekiti mlango wa kutokea siasa ni nzuri lakini ni mbaya Sana ukienda kinyume matakwa ya walio wengi
 
Ndiyo hata kama nitaitwa majina mengi ndani ya chama kwangu ni sawa tu, haiwezekani jambo lenye ukakasi kama hili likakailiwa kimya eti kisa tu kuwa tutapewa majina mapya kama ilivyo desturi yetu ndani ya chama kuwa kila analosema kiongozi ndani ya chama kiwe ni ndiyo.

Haiwezekani hata kidogo wala sitaki kuamini kuwa chama kimetosheka kupokea wanachama wapya, wala haiingii akilini kuwa upo wakati muafaka wa kuunga mkono jitihada za mwenyekiti na muda mwingine sio muafaka.

Hili ni jambo la ajabu haijapata kutokea. Huyu anataka kutuaminisha kuwa chama hakina haja ya kupokea wanachama wengine wapya, kama sio mbona amelenga kwa wabunge na madiwani ? Tena kwa kutaja tarehe eti 15/12/2018, hapo ndipo ninapo jiuliza maswali mengi.

1: Tuki ambiwa kuwa tulikuwa tukiwanunua na sasa fungu la manunuzi limekwisha tutakataa?

2: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeitia nchi hasara kubwa kwa kuwanunua wabunge na madiwani toka upinzani na hili nalo tutasema tunaonewa?

3: Tukiambiwa kuwa tumetumia vibaya fedha za walipa kodi wa nchi kwa kurudia chaguzi za kutengenezesha tutakataa?

4: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeshiriki kutoa rushwa ya madaraka kwa kuwashawishi wabunge na madiwani kuachia nafasi hizo na kisha tuka wahonga kwa kuwarudishia nyadhifa hizo hili nalo tutasema kuwa tunaonewa ? Nk.

Na ndiyo maana nasema hili jambo lina tia kichefu chefu sana , haiwezekani kuwa chama kikaishiwa mbinu za kuendesha siasa hadi kutuletea ukakasi wa kiwango hiki.

Iwapi CCM yetu ya zamani ambayo viongozi wake wali nadi Sera kwa wananchi na zikakubalika?

Si vibaya juhudi za mwenyekiti wetu kuungwa mkono, lakini kwanini tulishindwa kuwaambia hawa wahamiaji kuwa wamefanya jambo jema ila chama kina utaratibu wake wa kuwateua wagombea katika nafasi hizo walizo kuwa nazo na tuka washindanisha na walio kuwa na sifa za kugombea ndani ya chama ?

Au chama kimeishiwa watu makini na hata uchaguzi wa 2020 tutarajie kuona hamiaji hao hao wakipitishwa kugombea nafasi zao bila ya kupingwa ? Huu ni ukakasi unao zidi ule wa mtu aliye jikamulia maji ya ndimu kinywani.

Tunaitaka CCM yetu ambayo ilitembea kwa hoja zenye nguvu, na sio CCM inayo uogopa upinzani kwa kiwango cha kutisha kama hivi sasa.

Tunaitaka CCM yetu iliyo waandaa viongozi kwa kuptia vyuo vya siasa vya chama na kisha tuka wakomaza kiuongozi kupitia umoja wa vijana wa CCM.

Hatutaki CCM inayo okoteza okoteza wanachama, tena mbaya zaidi wengine walikimbia chama wakati hali ilipokuwa mbaya wakaenda upinzani leo wanarudi tunawaona kuwa wao ni bora kuliko waliovumilia hata katika kipindi ambacho chama kilipitia wakati mgumu.

Na ndiyo maana nasema nikibatizwa jina la namna gani ndani ya chama nitalikubali kuliko kukaa kimya ndani ya siasa uchwara kama hizi ambazo sikushuhudia hata mbunge mmoja wa viti maalum kumuunga mkono mwenyekiti wa chama ni aibu.
Umesema jina lako nani vile?
 
Nyie ndo wale wale mnao endekeza rushwa ndani ya chama, na safari hii lazima tuwafagilie mbali na hizo siasa zenu uchwara. Bora ukae kimya upigwe sindano upate kupona.
Hilo kupewa nafasi kugombea katika moot elections ndiyo rushwa yenyewe ya madaraka.
 
Nyie ndo wale wale mnao endekeza rushwa ndani ya chama, na safari hii lazima tuwafagilie mbali na hizo siasa zenu uchwara. Bora ukae kimya upigwe sindano upate kupona.
Jikite kwenye hoja kwanza, nilikuwa nafuta upotoshaji uliyowekwa bila haya
 
Mleta uzi ameuliza kwanini hamkuwashindanisha tangu mwanzo?kuna maana gani kurudia uchaguzi halafu arudi yuleyule aliyekuwa akiongoza ,ndio akasema hii si rushwa ya uongozi au ndo hampeleki maendeleo majimbo yanayoongozwa na upinzani hadi wahamie kwanza chama chenu?
Sikuja kujibu hoja zake, either ziwe na mashiko au laa, Bali nilikuwa nasahihisha upotoshaji kwenye Uzi wake
 
nyie hamjajua tu,hao wote wanaopokewa sasa,uchaguzi wa 2020 wote sweka nje,watabaki pure ccm.na huo ndiyo utakuwa mwisho wao kisihasa. za kuambiwa changanya na zako
 
Alisema Nape, chama chenu kinapoyatafuta madaraka kinabadilika na kuwa kitu kingine kabisa,na huo ndio ukweli wenyewe,hakuna kipya hapa.
 
Ndiyo hata kama nitaitwa majina mengi ndani ya chama kwangu ni sawa tu, haiwezekani jambo lenye ukakasi kama hili likakailiwa kimya eti kisa tu kuwa tutapewa majina mapya kama ilivyo desturi yetu ndani ya chama kuwa kila analosema kiongozi ndani ya chama kiwe ni ndiyo.

Haiwezekani hata kidogo wala sitaki kuamini kuwa chama kimetosheka kupokea wanachama wapya, wala haiingii akilini kuwa upo wakati muafaka wa kuunga mkono jitihada za mwenyekiti na muda mwingine sio muafaka.

Hili ni jambo la ajabu haijapata kutokea. Huyu anataka kutuaminisha kuwa chama hakina haja ya kupokea wanachama wengine wapya, kama sio mbona amelenga kwa wabunge na madiwani ? Tena kwa kutaja tarehe eti 15/12/2018, hapo ndipo ninapo jiuliza maswali mengi.

1: Tuki ambiwa kuwa tulikuwa tukiwanunua na sasa fungu la manunuzi limekwisha tutakataa?

2: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeitia nchi hasara kubwa kwa kuwanunua wabunge na madiwani toka upinzani na hili nalo tutasema tunaonewa?

3: Tukiambiwa kuwa tumetumia vibaya fedha za walipa kodi wa nchi kwa kurudia chaguzi za kutengenezesha tutakataa?

4: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeshiriki kutoa rushwa ya madaraka kwa kuwashawishi wabunge na madiwani kuachia nafasi hizo na kisha tuka wahonga kwa kuwarudishia nyadhifa hizo hili nalo tutasema kuwa tunaonewa ? Nk.

Na ndiyo maana nasema hili jambo lina tia kichefu chefu sana , haiwezekani kuwa chama kikaishiwa mbinu za kuendesha siasa hadi kutuletea ukakasi wa kiwango hiki.

Iwapi CCM yetu ya zamani ambayo viongozi wake wali nadi Sera kwa wananchi na zikakubalika?

Si vibaya juhudi za mwenyekiti wetu kuungwa mkono, lakini kwanini tulishindwa kuwaambia hawa wahamiaji kuwa wamefanya jambo jema ila chama kina utaratibu wake wa kuwateua wagombea katika nafasi hizo walizo kuwa nazo na tuka washindanisha na walio kuwa na sifa za kugombea ndani ya chama ?

Au chama kimeishiwa watu makini na hata uchaguzi wa 2020 tutarajie kuona hamiaji hao hao wakipitishwa kugombea nafasi zao bila ya kupingwa ? Huu ni ukakasi unao zidi ule wa mtu aliye jikamulia maji ya ndimu kinywani.

Tunaitaka CCM yetu ambayo ilitembea kwa hoja zenye nguvu, na sio CCM inayo uogopa upinzani kwa kiwango cha kutisha kama hivi sasa.

Tunaitaka CCM yetu iliyo waandaa viongozi kwa kuptia vyuo vya siasa vya chama na kisha tuka wakomaza kiuongozi kupitia umoja wa vijana wa CCM.

Hatutaki CCM inayo okoteza okoteza wanachama, tena mbaya zaidi wengine walikimbia chama wakati hali ilipokuwa mbaya wakaenda upinzani leo wanarudi tunawaona kuwa wao ni bora kuliko waliovumilia hata katika kipindi ambacho chama kilipitia wakati mgumu.

Na ndiyo maana nasema nikibatizwa jina la namna gani ndani ya chama nitalikubali kuliko kukaa kimya ndani ya siasa uchwara kama hizi ambazo sikushuhudia hata mbunge mmoja wa viti maalum kumuunga mkono mwenyekiti wa chama ni aibu.
Mcoloo umenena ukweli 100&
 
Subiri matusi toka kwa Bokoharam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom