Hata kama niko ndani ya CCM, nitaziita kuwa hizi ndio siasa uchwara

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Ndiyo hata kama nitaitwa majina mengi ndani ya chama kwangu ni sawa tu, haiwezekani jambo lenye ukakasi kama hili likakailiwa kimya eti kisa tu kuwa tutapewa majina mapya kama ilivyo desturi yetu ndani ya chama kuwa kila analosema kiongozi ndani ya chama kiwe ni ndiyo.

Haiwezekani hata kidogo wala sitaki kuamini kuwa chama kimetosheka kupokea wanachama wapya, wala haiingii akilini kuwa upo wakati muafaka wa kuunga mkono jitihada za mwenyekiti na muda mwingine sio muafaka.

Hili ni jambo la ajabu haijapata kutokea. Huyu anataka kutuaminisha kuwa chama hakina haja ya kupokea wanachama wengine wapya, kama sio mbona amelenga kwa wabunge na madiwani ? Tena kwa kutaja tarehe eti 15/12/2018, hapo ndipo ninapo jiuliza maswali mengi.

1: Tuki ambiwa kuwa tulikuwa tukiwanunua na sasa fungu la manunuzi limekwisha tutakataa?

2: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeitia nchi hasara kubwa kwa kuwanunua wabunge na madiwani toka upinzani na hili nalo tutasema tunaonewa?

3: Tukiambiwa kuwa tumetumia vibaya fedha za walipa kodi wa nchi kwa kurudia chaguzi za kutengenezesha tutakataa?

4: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeshiriki kutoa rushwa ya madaraka kwa kuwashawishi wabunge na madiwani kuachia nafasi hizo na kisha tuka wahonga kwa kuwarudishia nyadhifa hizo hili nalo tutasema kuwa tunaonewa ? Nk.

Na ndiyo maana nasema hili jambo lina tia kichefu chefu sana , haiwezekani kuwa chama kikaishiwa mbinu za kuendesha siasa hadi kutuletea ukakasi wa kiwango hiki.

Iwapi CCM yetu ya zamani ambayo viongozi wake wali nadi Sera kwa wananchi na zikakubalika?

Si vibaya juhudi za mwenyekiti wetu kuungwa mkono, lakini kwanini tulishindwa kuwaambia hawa wahamiaji kuwa wamefanya jambo jema ila chama kina utaratibu wake wa kuwateua wagombea katika nafasi hizo walizo kuwa nazo na tuka washindanisha na walio kuwa na sifa za kugombea ndani ya chama ?

Au chama kimeishiwa watu makini na hata uchaguzi wa 2020 tutarajie kuona hamiaji hao hao wakipitishwa kugombea nafasi zao bila ya kupingwa ? Huu ni ukakasi unao zidi ule wa mtu aliye jikamulia maji ya ndimu kinywani.

Tunaitaka CCM yetu ambayo ilitembea kwa hoja zenye nguvu, na sio CCM inayo uogopa upinzani kwa kiwango cha kutisha kama hivi sasa.

Tunaitaka CCM yetu iliyo waandaa viongozi kwa kuptia vyuo vya siasa vya chama na kisha tuka wakomaza kiuongozi kupitia umoja wa vijana wa CCM.

Hatutaki CCM inayo okoteza okoteza wanachama, tena mbaya zaidi wengine walikimbia chama wakati hali ilipokuwa mbaya wakaenda upinzani leo wanarudi tunawaona kuwa wao ni bora kuliko waliovumilia hata katika kipindi ambacho chama kilipitia wakati mgumu.

Na ndiyo maana nasema nikibatizwa jina la namna gani ndani ya chama nitalikubali kuliko kukaa kimya ndani ya siasa uchwara kama hizi ambazo sikushuhudia hata mbunge mmoja wa viti maalum kumuunga mkono mwenyekiti wa chama ni aibu.
 
kiukweli ccm hii inazidi kupotea siku hadi siku. yaani rushwa inatolewa waziwazi lakini takukuru iko Kimya tu. ccm kimekuwa chama chaku zoazoa Kama dodoki.
Imepotea au ndo wanajiimalisha ndo mana kiburi kama yote.
 
Yafanyike yatakayofanyika lakini muhimu kuliko yooote ni AMANI....AMANI ......AMANI..na kumcha MWENYEZIMUNGU
kiukweli ccm hii inazidi kupotea siku hadi siku. yaani rushwa inatolewa waziwazi lakini takukuru iko Kimya tu. ccm kimekuwa chama chaku zoazoa Kama dodoki.
 
We mwana wee..ya ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe. Wewe ni nani kuhoji maamuzi ya Mwenyekiti wa CCM. Tumeisafisha "RUSHWA" ndani na nje ya Chama wewe wasema tunatoa rushwa ya madaraka..waache watuunge mikono. Point moja niliyoiona hapo labda ni hiyo kwamba..wapinzani sio Wabunge na Madiwani ama kiongozi tuu..Bali ni jamii mzima ya watanzania. Ni ujinga kudhani tunadhoifisha upinzani kwa kuwachukua wawakilishi wao..
 
Mkuu mbona hatukufahamu we nan? Mana umejificha haraf unaandika kuwa mwanachama jioneshe kama sisi kuwa upo against na mbinu mbovu za chama kwa sasa
 
Ndiyo hata kama nitaitwa majina mengi ndani ya chama kwangu ni sawa tu, haiwezekani jambo lenye ukakasi kama hili likakailiwa kimya eti kisa tu kuwa tutapewa majina mapya kama ilivyo desturi yetu ndani ya chama kuwa kila analosema kiongozi ndani ya chama kiwe ni ndiyo.

Haiwezekani hata kidogo wala sitaki kuamini kuwa chama kimetosheka kupokea wanachama wapya, wala haiingii akilini kuwa upo wakati muafaka wa kuunga mkono jitihada za mwenyekiti na muda mwingine sio muafaka.

Hili ni jambo la ajabu haijapata kutokea. Huyu anataka kutuaminisha kuwa chama hakina haja ya kupokea wanachama wengine wapya, kama sio mbona amelenga kwa wabunge na madiwani ? Tena kwa kutaja tarehe eti 15/12/2018, hapo ndipo ninapo jiuliza maswali mengi.

1: Tuki ambiwa kuwa tulikuwa tukiwanunua na sasa fungu la manunuzi limekwisha tutakataa?

2: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeitia nchi hasara kubwa kwa kuwanunua wabunge na madiwani toka upinzani na hili nalo tutasema tunaonewa?

3: Tukiambiwa kuwa tumetumia vibaya fedha za walipa kodi wa nchi kwa kurudia chaguzi za kutengenezesha tutakataa?

4: Tukiambiwa kuwa chama chetu kimeshiriki kutoa rushwa ya madaraka kwa kuwashawishi wabunge na madiwani kuachia nafasi hizo na kisha tuka wahonga kwa kuwarudishia nyadhifa hizo hili nalo tutasema kuwa tunaonewa ? Nk.

Na ndiyo maana nasema hili jambo lina tia kichefu chefu sana , haiwezekani kuwa chama kikaishiwa mbinu za kuendesha siasa hadi kutuletea ukakasi wa kiwango hiki.

Iwapi CCM yetu ya zamani ambayo viongozi wake wali nadi Sera kwa wananchi na zikakubalika?

Si vibaya juhudi za mwenyekiti wetu kuungwa mkono, lakini kwanini tulishindwa kuwaambia hawa wahamiaji kuwa wamefanya jambo jema ila chama kina utaratibu wake wa kuwateua wagombea katika nafasi hizo walizo kuwa nazo na tuka washindanisha na walio kuwa na sifa za kugombea ndani ya chama ?

Au chama kimeishiwa watu makini na hata uchaguzi wa 2020 tutarajie kuona hamiaji hao hao wakipitishwa kugombea nafasi zao bila ya kupingwa ? Huu ni ukakasi unao zidi ule wa mtu aliye jikamulia maji ya ndimu kinywani.

Tunaitaka CCM yetu ambayo ilitembea kwa hoja zenye nguvu, na sio CCM inayo uogopa upinzani kwa kiwango cha kutisha kama hivi sasa.

Tunaitaka CCM yetu iliyo waandaa viongozi kwa kuptia vyuo vya siasa vya chama na kisha tuka wakomaza kiuongozi kupitia umoja wa vijana wa CCM.

Hatutaki CCM inayo okoteza okoteza wanachama, tena mbaya zaidi wengine walikimbia chama wakati hali ilipokuwa mbaya wakaenda upinzani leo wanarudi tunawaona kuwa wao ni bora kuliko waliovumilia hata katika kipindi ambacho chama kilipitia wakati mgumu.

Na ndiyo maana nasema nikibatizwa jina la namna gani ndani ya chama nitalikubali kuliko kukaa kimya ndani ya siasa uchwara kama hizi ambazo sikushuhudia hata mbunge mmoja wa viti maalum kumuunga mkono mwenyekiti wa chama ni aibu.
Aliyekupa hii ripoti hakupendi, nakushauri itafute mwenyewe uisome tena vizuri. Ila kwa ufupi hakuna sehemu waliposema hawatapokea wanachama wapya wanaohamia kutoka upinzani ISIPOKUWA baada ya tarehe 15/12/2018 watakaohamia hawatapewa nafasi ya kugombea nafasi walizoziacha upinzani BALI watapokelewa na kuwa wanachama wa kawaida.
 
Aliyekupa hii ripoti hakupendi, nakushauri itafute mwenyewe uisome tena vizuri. Ila kwa ufupi hakuna sehemu waliposema hawatapokea wanachama wapya wanaohamia kutoka upinzani ISIPOKUWA baada ya tarehe 15/12/2018 watakaohamia hawatapewa nafasi ya kugombea nafasi walizoziacha upinzani BALI watapokelewa na kuwa wanachama wa kawaida. USIWE KISEBENGO
Nyie ndo wale wale mnao endekeza rushwa ndani ya chama, na safari hii lazima tuwafagilie mbali na hizo siasa zenu uchwara. Bora ukae kimya upigwe sindano upate kupona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom