Jimmy George
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 1,733
- 1,648
Habari wana JF
Nasema humu JamiiForums naamini itawafikia wahusika maana humu kuna watu wa aina mbalimbali.
Kipindi hiki serikali inasisitiza wananchi kulipa kodi ya jengo pamoja na ardhi na kwa upande wa kodi ya majengo wametoa karatasi zinazoonyesha fedha unayotakiwa kulipa kutokana na tathimini wanazodai wamefanya kulingana na thamani ya nyumba yako. Tatizo lipo kwenye tathimini kwani thamani ya nyumba iliyoandikwa ni tofauti na uhalisia.
Hapa mtaani kwetu nyumba nyingi zinafanana kwa ukubwa wa viwanja na hata ujenzi wa nyumba yaani ramani lakini gharama zimekuja tofauti. Kuna jirani yangu nyumba yake ni ya kawaida lakini wanasema nyumba ina thamani ya milioni 128 hivyo kodi yake ni laki 1 na elfu 92 wakati nyumba ambayo inaendana na yake wanasema ina thamani ya milioni 12 na kodi yake ni elfu 18.
Mimi nawaomba wahusika wafanye tathimini upya kama kweli serikali inawajali wananchi wake wa hali ya chini maana kodi hizi zinatuumiza sana