Hata kama Mbowe na Slaa wangekuwa Vibaka, CCM bado ni nyoka hatari kwa Uhai Wa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata kama Mbowe na Slaa wangekuwa Vibaka, CCM bado ni nyoka hatari kwa Uhai Wa Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Analyst, May 14, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wakuu tutafakari mambo haya kwa kina.

  CCM na M/kiti wao waliahidi kujivua gamba ili waweze kukubalika kwa jamii ya Tz. Kwa bahati mbaya wameshindwa (Binafsi, nilijua tangu mwanzo wasingeweza kwa kuwa JK ndiye aliyeahidi). Cha ajabu sasa kupitia Nape, wanajaribu kujenga hoja kwamba hata wengine ni Mafisadi pia. Sijui lengo ni nini hasa but that's it!

  Naandika thread hii kutokana na watu wengi kupoteza muda kujadili nani fisadi zaidi kati ya CCM na viongozi wa CDM. Personally sihitaji kuingia huko sana kwa kuwa nahisi hapana umuhimu tena kwa kuwa kinachotusababishia maisha magumu hapa nchini si malori ya Mbowe wala Mshahara wa Dr. Slaa. Wenye akili timamu wote mnajua Tanzania inatapatapa kwa kuwa Ikulu kuna mtu aliyeshindwa kazi. Anayebisha asiishie kuandika pumba hapa jukwaani badala yake afuatilie hotuba ya JK kwenye semina elekezi (Anaomba Mawaziri wasiofuata taratibu wajiondoe wenyewe. What the hell.....?)

  Watu kama Nape wameamua kutumia muda mwingi mno kuzungumza na kutumia sekunde chache sana kusikiliza na kutafakari, ndiyo maana jamaa anapoteza muda kuelezea ufisadi wa malori ya Mbowe na Mshahara wa Slaa. Angetumia japo dakika moja kwa siku kusikiliza hoja za watu na kutafakari mantiki zake sina shaka angechagua kuwa mkimya. Kasoro za CCM zimevuka kuwa chama cha Mafisadi na kufikia hatua ya kushindwa kabisa kufanya kazi yoyote ya maana kwa ajili ya wananchi. Ndiyo maana nasema hata kama Mbowe na Slaa wangekuwa mafisadi kweli bado CCM inaendelea kuwa hatari kwa wananchi na taifa letu kuliko CDM na njia nzuri ya kuliokoa taifa letu ni kuwaondoa madarakani.

  Imagine uchaguzi uliopita tu; JK kaponea chupuchupu kuingia ikulu kwa maguvu lakini leo yupo malalamikoni dhidi ya mawaziri. Jamaa anafikiri madaraka yote ya kuteua na kutengua uteuzi amepewa ya nini kama si kuondokana na wasioweza ila kazi ziende?

  Nape amesema mengi sana ikiwa ni pamoja na ukabila wa CDM lakini hajatuambia ni Chama gani kitaifaa nchi kwa kuwa wao (CCM) tayari wamekubali viongozi wao ni wachafu lakini hawajawafukuza kwa kuwa watajitoa wenyewe. Binafsi, najua hakuna siku JK atajitoa CCM kabla ya 2016.
  • Vyombo vya habari vikiwanukuu viongozi wa Jiji la Dar es salaam (Ippmedia) vinadai hata Magufuli tunayedhani anajitahidi kutekeleza wajibu wake anadaiwa kung'ang'ania uondoaji wa Mabango ktk barabara kuu ili kumkomoa adui yake ambaye hata hivyo hakutajwa. Pia kwa mara nyingine swala la urais limetajwa. Sijaamini bado maneno haya lakini ndiyo yamesemwa na miongoni mwa Magamba. So, hata Mzee Pombe urais ndiyo unampagawisha! Kweli CCM Nyoka na magamba yake.
  • Nape (ktk CCM) anadaiwa kushangilia kujivua magamba kwa kuwa alitaka Lowasa na Rostam wapotee kabisa maana wao ni kikwazo kwa ambitions zake za uongozi.
  • JK hawezi kuchukua hatua kwa mafisadi wakubwa kwa kuwa ni wafadhili na rafiki zake.
  • Spika Sitta aliruhusu Kamati ya Mwakyembe kumsulubu Lowasa kwa kuwa jamaa walikula pasipo kumgawia chake. Naye alipohojiwa juu ya posho mbilimbili aligeuka mbogo.
  • Orodha ni ndefu lakini ujue katika CCM hakuna anayefanya kazi kwa nia ya kuisaidia nchi kwa dhati isipokuwa unafiki na ajenda binafsi za siri. Nisinukuliwe vibaya hapa maana yote haya yanaelezwa na Magamba wenyewe si CDM wala mimi.
  Tatizo la CCM wanasahau kuwa wanachojaribu kukiita ufisadi ndani ya Chadema kiliidhinishwa na vikao na wafuasi wao wanaona Slaa anastahili kulipwa kiasi hicho lakini CCM wenyewe wanarumbana juu ya ufisadi wa viongozi wao lakini hawafanyi kitu.

  Kauli yangu ni kwamba wanasiasa wengi katika nchi zetu ni wabinafsi kwa hiyo naogopa kumtetea mtu yeyote anayejiita mwanasiasa kwa kuwa uwazi wa tabia yake unajulikana kwa unakika zaidi anapokuwa madarakani tayari. Lakini hapa tulipo CCM mmeishiwa hoja sawa na mnavyoshindwa kuongoza nchi.
   
 2. mwanaharakati m

  mwanaharakati m Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kipimo cha gamba walilovua ni watz, hivo tunaomba ccm waende kwa watz ili tuone km watz wanaweza kuwapokea km wanavopokea cdm.
  Laana ya watz inawatafuna ccm, na ss wanatapatapa, tuwaache watapetape mwisho ni muda si mrefu ccm itazikwa, maana imeshakufa.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280

  Siyo kwamujibu wa chama, ni kwamujibu wa PPRA....Public Procurement Regulatory Authority. Chadema inatumia ruzuku ambazo ni mali ya wananchi (kodi za wananchi) hakinunui vitu kwa mujibu wa chama au kamati kuu kinatakiwa kifuate ACTS!

  What Chadema did is WRONG! Baregu, Kitila Mkumbo , Mnyika na Zito walikuwa against na wazo hili la Mbowe na Slaa!!

  Kitu kisichoeleweka hapa ni nini? kinachotetewa hapa ni nini?

  Ni kweli magari yalitumika tangu yakiwa mapya ...lakini

  1. Mbowe alipaswa kuingia mkataba na chama chake kuhusu hayo magari kuanzia mwanzo ( ab initio), na Chadema hawakupaswa kupokea kitu kipya..bure bila kuandikikishiana kuwa nini kitafanyika
  2. Magari hayo ya Mbowe yamenunuliwa kwa pesa yake ya binafsi? je kuna auditing inafanyika kutofautisha mali za chadema, mali binafsi za mbowe, n.k
  3. facts kuwa Mbowe ana influence kila steji katika manunuzi ni sawa na kujiuzia, I mean ALIJUA TOKA MWANZO lengo lake ni nini! This kind of biashara is against the rules


  Kuna faida nyingi kwa Mbowe kuiuzia chadema magari kwa sasa ,,,,tuache huko


  MR. ANALYST NILIKUWA NINAMJIBU MWENZAKO HAPO JUU NAAMINI NA WEWE INAKUHUSU

  KWANZA NI AIBU SANA KUWA UNAKUBALI KUWA KUNA UFISADI ILA UNACHOFANYA NI KUUBARIKI NA KUUFANANISHA NA UFISADI WA CCM

  KWA MAANA NYINGINE CCM ni mafisadi kwa sababu ni wakongwe na hivyo ufisadi wao ni nkubwa
  chadema ni mafisadi wachanga na ufisadi wao ni mdogo mdogo

  Ulichoandika hapo juu ni aibu sana

  Ukweli sina tatizo na mshahara wa Slaa mwache alipwe even 10 million is ok, ili karadi chadema mikoani wasilalamike hawapelekewi ruzuku

  Ila ninachosema

  jifunze kuwa na standard ambayo utaitumia kila mahali regardless kwenye familia yako au kwa jirani!! double standard inatisha na inakudhalilisha

  tunaposema ufisadi HATUISHII KWENYE VYAMA, KUNA UFISADI KWENYE MASHIRKA YA UMMA, PRIVATE SECTORS, n.k ambako hakuna CCM wala Chadema, no matter how much money wameiba hata kama ni shilingi 100 HUWEZI KAMWE KUSEMA IS OK ETI KWA KUFANYA COMPARISON NA CCM!!!

  Please badili title yako au mwombe mods aifunge hii thread inakudhalilisha sana  I believe na nimesema mara nyingi mwisho wa DOUBLE STANDARD NI AIBU! TUKISEMA TUNAKATAA UFISADI NI ULIO CCM NA ULIO CHADEMA NA KWINGINEKO KOTE! TUKISEMA maamuzi ya base zaidi upenzi wetu ndio aibu hizi zinwakumba wengi humu ambao mke mbele kuisema CCM ili hali kwenu hakujakaa sawa

  Leo hii mkuu wangu bila woga unaandika sentensi hiyo hapo juu....kana kwamba haujui sakata zima, kweli unataka kusema akina baregu wajinga mpaka waishauri

  SO IS NOT KAMATI KUU WAMEAMUA NINI , BALI SHERIA YA MANUNUZI INASEMA NINI...........where problems starts
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu umetumia muda mwingi sana kutoa a partisan analysis ambayo si tu kwamba ina factual defects lakini inaonyesha wazi kwamba wewe hujui mijadala inayoendelea lengo lake ni nini na tumefikaje hapo ambapo Nape amekuwa anaongea juu ya kinachodaiwa kuwa ni ufisadi wa CDM. Wakati upande mmoja unaonekana kukerwa na ufisadi, upande mwingine umebeba mbeleko ya kuwabeba mafisadi hao hao ukidai eti Lowassa alitundikwa msalabani na Sitta kwa sababu Sitta alinyimwa mgao, what a wild and unsubstantiated allegations that are hard to find a purchase.

  Wakati nakubaliana na wewe kwamba the President ought to walk an extra mile and assert authority na hasa kwa kuanzia awashughulikie wale walioonekana magamba na watendaji wabovu, sikubaliani na wewe hata kidogo kwamba tushughulikie ufisadi wa serikali halafu tuache ule wa CDM (kama upo) eti ukidai hauna madhara kwa wananchi. Hela zinazochezewa ni za walipa kodi na huu ndiyo mwanzo wa kuelekea huko huko maana mhalifu yeyote kama alivyo mwanafunzi huwa ana-graduate na kuwa hatari zaidi. Hawa wanakoelekea ni huko huko kama wataachwa leo wafanye watakavyo (maana ndiyo tunategemea wachukue dola huko mbele).

  Kwa ujumla kuna kupotoka kwingi katika mijadala yetu humu ndani na in most cases we have not been able to rise above partisan myopia na kudhani kwamba hawa viongozi wetu ni malaika na kudhani kwamba na wenyewe ni weupe mithili ya pamba. Nao wanaishi na jamii na kuna watu wanawafahamu na kwa hiyo ikitokea mtu anatoa anachokijua kuhusu kiongozi huyo tusiwe na tabia ya kufanya mob justice na kumwaga matusi humu!
   
 5. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mkuu Waberoya,
  Nashukuru kwa kuwa umeisoma thread hii pamoja na kutokukubaliana na Heading yake. Nasikitika tu kwamba kama walivyo wafuasi na wanachama wengi wa Chama Chenu huwa hampendi kutumia muda kusoma kitu kwa makini ili mpate mantiki, badala yake kila mnapoambiwa kitu hudhani mnashambuliwa bure. Soma aya ya mwisho kama huwezi kurudia maandishi yote. Sikusudii kubariki ufisadi wowote ninachosisitiza ni ubovu mkubwa wa nyoka na uwezo wake mdogo wa kujirekebisha pasipo kusahau total failure ya M/kiti wenu.
  Sijajidhalilisha (kwa mtu anayesoma kwa makini) so, siwezi kubadili heading wala kumwomba Mod. chochote. Kubali ukweli ndugu yangu, JK na Nyoka kwa ujumla wake wameshindwa kuongoza nchi na swala haliishii watanzania wangapi ni mafisadi.

  Unajua Nyoka (Sorry, jina lilipendekezwa na JK mwenyewe) angeweza kuwa mkali kidogo tu katika kuongoza nchi (pamoja na ufisadi uliojaa ndani) yake rushwa ingepungua sana miongoni mwa watumishi wasiokuwa wanasiasa. Tatizo wanasiasa karibu wote wana kashfa. Wataweza vipi kuwakemea wataalamu na watumishi wengine?
   
 6. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45


  Nashukuru kwa mawazo yako. Sijajua though, nimewapoteza wapi wasomaji wa thread hii. Sina lengo la kubariki ufisadi wowote ninachosisitiza ni kwamba wakati Nape na watu wa aina yake wanalalamika na ufisadi wa CDM mimi naona wanamiss point kwa kuwa ukweli ni kwamba hali ilipofikia si swala la kukumbatia ufisadi tu linalomtesa "nyoka wa magamba" bali ameshindwa hata kujenga unity miongoni mwa wanachama wake ili kushughulikia mambo mengi mengine ya msingi pia. Imagine kama Magufuli anadaiwa kubomoa mabango barabarani kwa ajenda binafsi na mwana CCM mwenzie na wote wanatumikia serikali, tutarajie nini? ... Ndiyo maana nasema; hata kama hao wengine (sijawatetea) ni wachafu bado haimaanishi CCM ni bora kwa kuwa failures zao haziishii ktk kushughulikia ufisadi tu bali hata simple management imewashinda na hivyo hawawezi hata kuwa na vision kwa nia ya kulisaidia taifa.
   
Loading...