Hata ikiwashwa, mitambo ya Dowans haitazalisha umeme. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata ikiwashwa, mitambo ya Dowans haitazalisha umeme.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkeshaji, Apr 3, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Habari wana jamvi,
  Hivi karibuni kumekuwa na mijadala mingi mno kuhusu matatizo na kashfa zinazoikumba sekta ya nishati na madini, kipekee sekta ya umeme. Mambo mengi yamezungumzwa kuhusu sababu za matatizo hayo na wakati mwingine ushauri umetolewa wa nini kifanyike kutatua matatizo hayo.

  Nikiwa mmoja wa wanajamvi niliwahi kutoa mchango wangu wa mawazo kwenye thread kadhaa zilizozungumzia matatizo tajwa ambazo zilianzishwa na wanajamvi wengine. Mimi binafsi pia niliwahi kuanzisha thread iliyoelezea mojawapo ya matatizo katika sekta hiyo ya nishati ya umeme. Thread ilisomeka: "Wanaosababisha mgawo wa umeme hawa hapa". Thread hii si mwendelezo wa thread hiyo niliyoitaja lakini ukiwa na ufahamu wa nini nilikiandika huko, utapata mtiririko mzuri katika thread hii, japo hii yenyewe inajitosheleza.

  Kwa kuwa tayari mambo mengi yameshazungumzwa, ni vizuri nikaenda moja kwa moja kwenye hoja ambayo naamini watanzania wengi kama si wote wameisahau.

  Katika jitihada za kutaka kutatua tatizo la mgawo wa umeme, hivi karibuni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. January Makamba alishauri kuwa aidha serikali au Tanesco iingie mkataba japo wa muda mfupi na kampuni ya kuzalisha umeme wa dharula ya Dowans, wazo ambalo pia liliungwa mkono na Waziri kivuli wa Nishati na Madini Mh. John Mnyika ambaye alipendekeza mitambo hiyo ya Dowans itaifishwe kwa kutumia sheria ya uhujumu uchumi. Vilevile "impliedly" Mh. Waziri Mkuu alipendekeza kuwashwa kwa mitambo hiyo ya Dowans ili kupunguza mgawo wa umeme.

  Suala la Dowans limezungumzwa mara kadhaa kisheria na kisiasa na watu waliobobea kwenye masuala hayo. Mh. January, Mh. Mnyika, Mh. Waziri Mkuu na wengineo wamelizungumzia kisiasa, mimi nitalizungumzia kiufundi kuonesha kuwa wazo lao halitafanya kazi.

  Dowans
  Dowans ina jumla ya mitambo minne ambapo mitatu kati ya hiyo ni mobile (ya kukokotwa na gari), hii si ya kudumu ni ya muda yaani emergence na kila mmoja una uwezo wa kuzalisha 20MW (megawati). Pamoja na hiyo upo mtambo mmoja mkubwa ambao ni wa kudumu (una harufu ya kifisadi kwani walitakiwa kufunga mitambo ya muda na si ya kudumu kama huu ambao ukiufunga leo na kuuondoa ndani ya miaka miwili au mitatu ni hasara kubwa, nani analipia gharama hizo?-not economically viable). Mtambo huu una uwezo wa kuzalisha 40MW. Kiujumla mitambo ya Dowans ina uwezo wa kuzalisha 100MW. Mitambo hii yote inazalisha umeme kwa kutumia nishati ya gesi asilia kutoka Songosongo.

  Historia fupi ya gesi asilia ya Songosongo
  Matao mengi ya gesi asilia huko Songosongo yaligundulika mwanzoni mwa miaka ya 70 na uendelezaji wake ulianza katika miaka hiyo hiyo. Kazi ya uendelezaji wa gesi hiyo ilisitishwa katika miaka hiyo hiyo (sababu za kina bado sijazipata).

  Uendelezaji wa mradi wa gesi ya Songosongo ulianza tena mwaka 1998 ukihusisha ujenzi wa visima vya gesi, mtambo wa kusafishia gesi na bomba la kusafirishia gesi kutoka Songosongo wilayani Kilwa hadi Dar es Salaam. Primarily, lengo kuu la mradi huu lilikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme katika kituo cha umeme cha Songas-Ubungo ambacho wakati huo kilikuwa kikimilikiwa na Tanesco (sasa hivi Tanesco hawamiliki kituo hiki-utata mwingine) na kilikuwa kikitumia mafuta ya kuendeshea ndege kwa ajili ya kuendeshea mitambo hiyo (Mitambo hii inafanana kwa kiasi kikubwa na injini za ndege). Kwa mantiki hiyo Tanesco walikuwa wanahisa wakubwa waliowekeza fedha zao katika kuendeleza mradi huo.

  Matumizi ya gesi ya Songosongo
  Kwa kuwa lengo kuu la gesi hii lilikuwa ni kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kuzalishia umeme, hivyo hata design ya visima, mtambo wa kusafishia na bomba la kusafirishia ilijikita katika wingi wa gesi itakayotumika katika kuzalishia umeme bila kuangalia kuwa baadaye kungeweza kujitokeza uwezekano wa gesi hiyo kutumika vinginevyo. Uwezo wa mitambo ya kuzalishia, kusafishia na kusafirishia gesi kwa sasa ni 104mcf kiwango ambacho kiliaminika kuwa kingeweza kuzalisha umeme kwa kadri ilivyokuwa imetarajiwa.

  Baada ya kukamilika kwa mradi huo ilionekana kuwa gesi hiyo ingeweza pia kutumika kwa matumizi ya viwanda vya kuzalishia mfano sementi, bati, bia, n.k. kwa hiyo viwanda zaidi ya 40 vikaunganishwa kwenye mtandao wa gesi hiyo ingawa havikuwemo kwenye mahesabu. Songas, ndiyo kampuni iliyopewa dhamana ya kuendesha mitambo ya kuzalisha, kusafishia na kusafirishia gesi.

  Matumizi ya gesi makubwa kuliko uzalishaji
  Katika kile kile tulichokizoea cha kuporwa rasilimali za nchi yetu na wajanja kutoka nje kupitia utata wa mikataba, Songas imetengeneza mkataba unaotoa kipaumbele kwa viwanda ambavyo awali havikuwa kipaumbele katika kupatiwa gesi. Katika mkataba huo ile gesi iliyokusudiwa kwa ajili ya kuzalishia umeme wameiita "Protected gas" na kiwango kilichobaki wakakiita "Unprotected gas". Katika mkataba huu Songas ndio wenye mamlaka yote ya "unprotected gas" ikiwemo kutafuta masoko, kuuza na kuchukua sehemu kubwa ya faida itokanayo na mauzo hayo. Hii inawapa wao Songas fursa ya kuuza gesi nyingi kwa bei kubwa kwenye viwanda vya uzalishaji na kujisombea pesa kibao. Ikumbukwe kuwa mikataba kati ya serikali na Songas ipo 21 na yote inasemekana ina utata mkubwa sana.

  Kwa kutumia mkataba huo wa "Unprotected gas", Songas inatoa kipaumbele cha mgawo wa gesi kwa viwanda vya uzalishaji na kiwango kinachobaki ndicho kinachopelekwa kwenye kuzalisha umeme. Hii imesababisha matumizi kuwa makubwa kuliko uwezo wa mitambo ya kuzalisha, kusafisha na kusafirishia gesi na hivyo kusababisha sehemu kubwa ya mitambo ya kuzalisha umeme kukosa gesi ya kuendeshea mitambo yao. Ukijumlisha na matumizi ya viwandani, gesi inayozalishwa inatosha kuzalisha umeme kiasi cha 325MW. Hii ni mitambo mitatu tu ya kuzalisha umeme ambayo ni Songas yenyewe ambayo kwa mujibu wa mikataba inapewa kipaumbele cha kwanza cha kupata gesi (180MW), Wartsilla Tegeta (45MW) na mtambo mwingine wa 100MW ambao kwa sasa ni Wartsilla Ubungo (100MW).

  Mitambo ya Wartsilla Ubungo na Tegeta ni mitambo mipya kabisa (ina umri wa miaka 2). Yote kwa pamoja ilichukua nafasi ya Dowans (100MW) na Aggreko (40MW). Baada ya mitambo hii ya Wartsilla kukamilika ujenzi wake, ilishindwa kuzalisha umeme kutokana na upungufu wa gesi ya kuendeshea na ilibidi kusubiri kwa takribani mwaka mzima hadi mkataba wa Dowans ulipositishwa na ule wa Aggreko kuisha. Kwa hiyo kiwango cha uzalishaji umeme kilichoingia ni sawasawa na kile kilichotoka (Na hili ni tatizo lingine kwa wizara ya nishati na madini kwani hakuna kiwango cha umeme kilichoongezeka baada ya kipindi cha umeme wa dharula). Kwa mantiki hiyo hata kama kutakuwa na mtambo mwingine ambao utaongezeka mbali ya hiyo niliyoitaja, gesi iliyopo sasa haitoshelezi kwa uzalishaji wa umeme kwa mitambo zaidi ya hii inayozalisha sasa.

  Kuongeza kiwango cha uzalishaji wa gesi
  Kutokana na sababu kuwa mahitaji ya gesi kwa sasa ni makubwa kuliko kiwango kinachopatikana, imeonekana kuna umuhimu wa kuongeza uzalishaji wa gesi. Ongezeko hilo litahusisha kuboresha mitambo ya kuzalisha, kusafishia na kusafirishia gesi. Ili kukidhi mahitaji kwa sasa na baadae na kwa kuzingatia sababu za kiufundi katika miundombinu ya gesi, uzalishaji unatakiwa ufikie 140mcf kutoka 104mcf ya sasa.

  Kwa kuwa kampuni ya Songas imeshaona utamu wa gesi (wameonja asali sasa wanataka kuchonga mzinga), bila kuambiwa na mtu iliandaa proposal ikihitaji kuwa mbia mkuu wa kufanya maboresho hayo. Hiki ni kitu kizuri kwani hatuwezi kuficha ukweli kuwa gesi inahitajika mno viwandani, lakini zaidi kama nishati ya kuzalishia umeme ukizingatia kuwa mafuta ni gharama mbali ya kuwa si rafiki mzuri wa mazingira, na umeme utokanao na nguvu ya maji umeonesha matatizo makubwa sana hasa wakati wa ukame.

  Tatizo lililopo hapa ni lile lile kuwa Tanzania ni shamba la bibi kila mtu anavuna atakavyo bila wasiwasi wowote. Katika proposal yake, Songas ilipendekeza kubadili mfumo wa malipo ya gesi yaani "Tarrifs". Katika mfumo huo inaonekana wazi kuwa Songas inataka kufaidika zaidi kwani wanataka kupandisha bei ya gesi kwa kiwango kikubwa mno. Hii itasababisha bei ya umeme kupanda hivyo mzigo kuzidi kumwelemea mlalahoi. Ndiyo maana proposal hiyo ya Songas imekataliwa na Ewura zaidi ya mara tano kwa miaka minne mfululizo katika public hearing pale Karimjee. Mara zote hizo Ewura imekuwa ikiishauri Songas ikabadilishe viwango vyake vya Tarrifs lakini jamaa hawa wanaonekana kupunguza kiwango kidogo mno kutoka kile wanachopendekeza. Inasemekana Songas hawajachoka na sasa wanataka kupeleka proposal yao kwa mara nyingine ambayo aghlabu itakuwa ya kumwumiza mlalahoi. Je Ewura nao hawatachoka kuwarudisha au ndo watakata tamaa kama walivyofanya wakati wa kuongeza bei ya umeme? Wakichoka na kuipitisha hiyo proposal, TUMEUMIA.

  Proposal ya Songas ikikubaliwa
  Ukiachilia mbali viwango vya tozo "tarrifs" watakavyokubaliana Songas na Ewura, endapo proposal ya Songas itakubaliwa basi mradi huo wa kuongeza uzalishaji na usafirishaji wa gesi utachukua muda wa angalau miaka miwili mara baada ya upanuzi wake kuanza. Kwa hiyo kama mradi utaanza leo basi tutarajie kupata gesi ya kutosha kuendeshea mitambo ya umeme zaidi ya hii inayotembea sasa miaka miwili baadae. Hii ina maana kuwa kama hakuna chanzo kingine cha kuzalisha umeme, basi suala la kuongeza mtambo mwingine unaotumia gesi haupo kwa sasa, na hata kama utaongezwa basi hautazalisha kwani gesi haitoshi, na hili ndilo suala ambalo wanasiasa akiwemo Mh. January hawalifahamu.

  Bila shaka wanajamvi na wale wageni wasio wanajamvi wamenielewa kuwa hata kama kisiasa na kisheria itakubaliwa kuwashwa, kiufundi mitambo ya Dowans haitaweza kuzalisha umeme. Hata kama kuna mtu haamini ninachokisema, naamini atakuja kuamini siku chache zijazo.

  Kinachoweza kufanyika kwa dharura
  Hivi sasa kuna hali inayooonekana kana kwamba "makali ya mgawo wa umeme yamepungua". Hii inaweza ikawa inatokana na ukweli kwamba mvua nyingi zimenyesha katika nyanda za juu kaskazini na kusini na hivyo kujaza mabwawa ya kuzalishia umeme ambayo yalikuwa "yamekauka". Hii imesababisha kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji wa umeme wa nguvu za maji na hivyo kuongezeka kwa kiwango cha umeme katika gridi ya taifa.

  Ni matarajio yangu mvua hizi za masika zitakapoisha, takribani miezi miwili kutoka sasa tutarudi katika hali ile ile iliyotukumba katika miezi zaidi ya miwili iliyopita yaani mgawo mkubwa wa umeme, kama hakutakuwa na hatua stahiki za makusudi zitakazochukuliwa sasa.

  Hatua za muda mfupi zinazoweza kuchukuliwa ni kuweka mitambo ya kutumia nishati ya dizeli ambayo itakuwa na uwezo wa kuzalisha kiwango cha umeme ambacho kinatarajiwa kupungua kutoka gridi ya taifa. Tayari tumeshasikia nia na mipango ya tanesco na serikali katika hili. Wasiwasi wangu ni kuwa isije kuwa ni mipango tu ya kwenye makaratasi kama ile ambayo ipo kwa takribani miaka 20 iliyopita bila utekelezaji huku tanesco na serikali wakitusomea mipango hiyo kila kukicha wakati hatuoni hata jiwe la msingi la miradi hiyo. Wasiwasi wangu mwingine ni kuwa mipango hii isije ikatekelezwa miaka 10 ijayo na hivyo kuondoa maana ya udharula.

  Hatua za muda wa kati na muda mrefu za kumaliza tatizo hili ni kuendeleza miradi ya gesi ya Songosongo, Mkuranga na Mnazi bay-Mtwara. Uendelezaji huu unatakiwa ufanyike kwa tahadhari kubwa hasa katika suala la mikataba ambayo ni lazima inufaishe taifa na si wawekezaji pekee.

  Mipango mingine ya muda wa kati na muda mrefu imeandikwa vizuri katika "Power masterplan-2025".
  [FONT=&quot]Muda wa hadithi umekwisha na sasa umefika wakati wa kubadili maandishi hayo kuwa umeme.[/FONT]
   
 2. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,260
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Umenielimisha vizuri, its another disaster waiting to happen they politicians will keep on talking and never walk the walk, time of action is now before the level of rain fall dramatically.
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa mkuu. Watu wamejikita katika kuzungumzia habari ya kuilipa ama kutoilipa Dowans lakini tunasahau kuangalia kwa kina msingi wa tatizo. Kwa hali ninayoiona mimi ni vigumu kupata suluhu ya kudumu ya tatizo la umeme. Ngoja tuone.
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Duh!!!!!!!
   
 5. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kaka mkeshaji uko sawa kwenye songas lakini hujaona proposal yao nyingine ya 're_basin' hii inaongeza gas availability

  Nakubaliana na wewe mambo mengi ila hili naomba nikuweke sawa:

  Mpango wa dharura wa thermal plant ya mafuta mazito ya dizeli utaongeza gharama maradufu, wakati bei ya gesi ni cent 4, mafuta ni shs 700

  Umeona kooote kwenye thermal plants shirika la umeme linaendesha kihasara? Mafuta yana bei kubwa sana, ndio maana IPTL ilikuwa haitembezwi to full capacity its just so expensive, na guess who is going to get the bill if govt won't subsidize?
   
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada anajua kushawishi kwa uongo/ukweli@50:50. Angalizo- kwa sasa watsilla ubungo hawatumii gas, je mitambo ya dowans pia haiwezi kutumia nishati nyingine?, why getting worried kuwa ikiwashwa haitawaka bcos of insufficient gas?! Are we so static?! Mbona watsila ubungo walibadli nishati tumika in a flash?!, hapa mi naona mawazo mgando + chuki+ kukosa uzalendo hivyo kuamua kuidanganya jamii kuwa planned interventions haziwezekani kana kwamba mtoa mada ndo muelewa kuliko watu wote. Any way hongera kwa bandiko lenye ushawishi.
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Sometimes I wonder what people keep between their ears:A S cry:
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu acha kuchanganya mada;
  Mimi sina chuki bali nataka kueleza vile nijuavyo. Suala la kuamini au kutoamini libaki kwa msomaji.
  Mtambo wa 100MW wa Tanesco ambao kwa sasa unaendeshwa na kampuni ya Wartsilla haujawahi kuendeshwa kwa nishati ya mafuta na wala haujawa designed kutumia nishati hiyo.
  Sitaki kusema sana lakini nadhani kwa haya yanayotokea "Mgawo wa umeme" utakuwa umeanza kuniamini. Na makali zaidi yanakuja, pindi yatakapotokea unaweza kurudi kwenye hili bandiko then tutakwenda sawa. Kwani kwa watanzania tulio wengi Hatuamini mpaka tuone.
   
 9. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nsiande,
  Hilo la mitambo ya mafuta nimeliweka katika mpango wa muda mfupi wa tatizo tulilonalo ambao pia ni mpango wa Tanesco. Kuhusu gharama ni kweli kuwa mafuta yana gharama kubwa lakini katika mazingira tuliyonayo huenda hilo ndo suluhisho kwa sasa.
   
 10. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,098
  Trophy Points: 280
  Na muvi yetu inaendelea
   
 11. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umeona eeh!
  Hili bandiko lilikuwa la tarehe 3 April wakati huo hali ya umeme ilikuwa si mbaya kama sasa. Watu wakajisahau wakidhani mambo yataendelea kuwa poa. Yanayotokea sasa ni muendelezo wa matatizo ambayo tuliyasahau huko nyuma, na mengine huwa hatupendi kuyazungumzia hadi yatakapotokea. Wengine huwa hawaamini wanapoambiwa hadi yatokee.
  Nadhani sasa wengi wameamini kwani suala la uhaba wa gesi limeshawekwa bayana na Mkurugenzi wa Songas.
   
Loading...