Hata ikithibitika Fedha za Escrow ni za Wizi, Nawahakikishia, Hakuna Yeyote wa Kuwajibika

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,543
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa ku declare my interest, Mimi Paskali, sijapata mgawo wowote wa fedha za escrow, hata senti tano!.

Hii ni kufuatia mtu ukitoa tuu mawazo yako huru tofauti na maoni ya wengi, huchelewi kunyooshewa kidole kuambiwa umelipwa!.

Nimeangalia kikao cha Bunge leo asubuhi, waheshimiwa wabunge wetu, huku wakiwa wamehamanika sana, wameishupalia sana ripoti ya ukaguzi wa Escrow Account, huku wakizungumza kwa jazba sana, kuwa kama kuna wahusika, wawajibishwe bila huruma!.

Akijibu swali katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza Peter Pinda, amesema safari hii, hakuna cha Mswalie Mtume!, yoyote atakayetajwa, anakwenda na maji!.

Watu wamehamanika sana na uwajibishwaji, as if ikithibitika escrow ni wizi, basi inaonekana kana kwamba ni bonge la sikandali!, ni bonge la wizi, ni bonge la kashfa!.

Ukweli ni kuwa fedha za escrow sio big deal kihivyo!, kumeishatokea maskandali makubwa ya wizi mkubwa kama uchotaji fedha za EPA kutoka BOT, escrow ni cha mtoto, na hakuna chochote kilichofanyika!, mfano EPA, TanGold, Deep Green, Meremeta, Import Support, DCP, etc, etc, wahusika walifanywa nini?!.

Moja ya viashiria vya utawala bora, ni pamoja na consistence katika utoaji wa maamuzi, ili kuepuka "double standards", na maamuzi na hatua zilizochukuliwa katika similar nature, ni lazima ziwe applicable kwa matukio mengine yote ya aina hiyo, yatakayofuatia, hii kisheria inaitwa "precedence!".

Kwa vile kuliwahi kutokea wizi mkubwa wa fedha za umma za EPA kupitia BOT, ambao uliibuliwa na ripoti ya CAG!, na maadamu wahusika wa wizi ule, walisamehewa kwa kutakiwa kurejesha fedha walizoiba!, na hivyo kutokufikishwa kwenye vyombo vyovyote vya sheria!, then hii ni "precedence" ambayo ni lazima utaratibu huo huo wa kurejesha utumike!. Zile kesi za EPA mlizosikia zikiunguruma, ni kesi za wale walioshindwa kurejesha!.

Miongoni mwa wanaotajwa tajwa kumegewa mgao huo, ni pamoja na mawaziri wetu, akiwemo waziri mmoja mwanamke ambaye ni maadilifu sana kwa viwango wa kimataifa, aliyeomba mchango kwa nia njema kuwasomesha watoto yatima na akapewa B.1.6. Sasa ikija kutokea huko mbele kuwa fedha hizi za Escrow ni fedha za umma, hivyo ni fedha za wizi, kwanza yeye aliyepewa, hana kosa lolote kupokea misaada kutoka kwa wasamaria wema bila kujua kumbe yule msamaria ameziiba mahali!, pili yeye amezitumia fedha hizo for a good cause!, hivyo upokeaji wa fedha hizo ni justified hapa duniani hadi mbinguni!.

Japo pensheni yake, inamuwezesha kuzirudisha over night!, naomba kumtoa wasiwasi huyo waziri wetu mpendwa kuwa asiwe na shaka wala wasiwasi kabisa, ikitokea ni kweli ni fedha za escrow zikathibitishwa ni fedha za wizi, na yeye kutakiwa kuzirejesha! asihangaike kabisa kuigusa hata senti moja ya pensheni yake!, sisi wadau wa uadilifu wake, wenye mapenzi mema na yeye, tutamfanyia harambee ya siku moja tuu, na fedha zote zitarudi!.

Watanzania tupunguze kuhamanikia, escrow sio big deal kihivyo!, EPA ndio ilikuwa big deal na wizi mkubwa!, kama mijizi ile wizi mkubwa wa EPA, ilisamehewa!, why not watu safi hawa waliopokea mgao wa escrow bila kujua ni fedha za wizi, wasisamehewe?!.

Paskali

Update.
Niliyoyasema, yameanza kutokea!, na hata ningekuwa mimi sikubali hata kido!, kwenye EPA, mijitu imeiba bilioni 40!, haijafanywa chochote!, leo watu wamemegewa tujisenti twa bilioni 1.6, alafu wabunge wanapiga kelele wahusika wawajibike!, wawajibike kwa lipi?!, angalieni Prof. Muhongo anavyo komaa!.
Katika kikao cha ndani ya CCM, Waziri wa nishati Sospeter Muhongo amesema bayana kwamba hatishwi na wabaishwaji na kamwe hawezi kujiuzulu kutokana na chuki za mafisadi wanapigania vitalu vya gesi na kama atalazimika kujiuzulu siyo tu bunge litayumba, bali ardhi ya Tanzania itatikisika, kwa sababu anazo data za uhakika kuonyesha hili swala la IPTL ni mpango uliosukwa na madalali walionyimwa vitalu vya gesi na wale walivuliwa uwakilishi wa tanesco kisheria
Naunga mkono msimamo wa Prof. Mhongo, mijitu yenye ma confidence kama hii, ndio inayohitajika!. Hili nimeikuta hapa!.

Muhongo: Sijiuzulu sakata la Escrow vinginevyo ardhi ya Tanzania itatikisika !

Paskali

Up Date: Niliamini hakuna atakaye wajibishwa, kwa vile Werema amejiwajibisha mwenyewe na Tibaijuka amewajibishwa, hivyo nakiri I was wrong kusema hakuna atakayewajibika!. Nili under estimate ignorance ya top leadership yetu!, they are more ignorant kuliko hata nilivyodhani mwanzo, kwangu kutomwajibisha yoyote ndio ingekuwa busara!.

Sisi Watanzani ni mijitu mijinga ajabu!, kwa sababu kosa la Tibaijuka sio kupokea pesa za wizi, bali ni kitendo cha kujulikana alipokea pesa za wizi!, lakini viongozi wetu waliopokea kuanzia fedha za Rada, Meremeta, Deep Green, Tan Gold etc, they are ok kwa vile hawajulikani!.

Hili lidudu IPTL linajulikana fika tangu lilipoanza ni kwa rushwa mwanzo mwisho!. Wakati linafanyiwa lobbying, aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, aligoma kupokea rushwa, akaletewa bulungutu la minoti mpaka nyumbani kwake, kwa vile tangu mwanzo alikataa, this time wakamtaim katoka, 'Mzee wa Kazi' akabisha hodi, house boy akafungua mlango, akakabidhiwa mzigo siku ya 24 December, kesho yake ni Krismas!. Ujumbe huo ukaletwa kama 'zawadi' ya Krismas, ukaambatanishwa na kadi ya Krismas!, na kusainiwa na Bwana Mtoa Sadaka!", akitegemea demand za sikukuu na muambo wa January, lazima atashukuru!. Rutabanzibwa aliporudi nyumbani akakabidhiwa zigo lile!.

Kwa jinsi ile ile alivyokabidhiwa, tarehe 27, akalibeba zigo lile vile vile lilivyo na kulirudisha kwa 'mwenyewe". TISS walijua kila kitu, TAKUKURU walijua kila kitu, serikali ilijua kila kitu, they were all well taken care off, why only Tibaijuka?!.

Aliyekuwa Mkuu wa nchi alipokea ile zawadi ya Krismasi, Waziri wake pia alipokea!. 'Mtoa Zawadi' akawaarifu 'wakubwa", kuwa Rutabanzibwa alikataa zawadi ile na kuirudisha, na yeye ndiye kikwazo pekee anayekwamisha 'mradi!', huwezi amini kilichotokea!, Rutabanzibwa aliondolewa, na mradi ukapitishwa!. Jee mnamjua waziri wake ilikuwa nani?!.

Nasema Watanzani ni mijitu mijinga, tunapigia kelele matokeo badala ya chanzo!, tujisenti twa escrow, ambayo sio chanzo ni matokeo tuu!, malipo hayo ya IPTL yanayobishaniwa ni kiwango kidogo tuu cha capacity charges, mkumbuke hili lidudu IPTL bado linameza mabilioni ya utility daily kwa kila siku iendayo kwa Mungu!, who cares?, nobody cares!. Kushadadia fedha za escrow tuu ni ignorance ya hali ya juu!.

Turudi kwenye mgao wa Escrow, PAP amegawa 'sadaka' kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia Stanbic Bank, kwa vile majina hayajatajwa, then its ok!. JR amegawa sadaka kubwa kubwa nene nene, kwa 'wanene' kupitia account yake iliyoko Uholanzi, majina yapo na viwango vipo, na wanajulikana!, ila kwa vile hawajatajwa then its ok, lakini Watanzania mazuzu, na bunge letu lililojaa mazuzu, tunashadadia majina ya Mkombozi tuu, au tunashangilia Tibaijuka tuu amewajibishwa!, huu ni uzuzu wa kiasi gani?, kwenye list ya Mkombozi kuna viongozi wangapi wametajwa wakiwemo waheshimiwa majaji!, why only Tibaijuka?.

Nahisi sio wengi wanaojua kuwa IPTL/PAP bado inaidai Tanesco fedha nyingi kuliko fedha zote zilizokuwemo ndani ya account ya escrow!, na kwa vile bado IPTL inazalisha umeme, deni hilo linaongezeka siku hadi siku, na malipo yake yatafanyika direct kutoka Tanesco into IPTL/PAP kimya kimya!, and life goes on!, nobody cares!.

Kwenye IPTL/Escrow, Tanzania kama taifa, tumejikwaa, lakini watu wanashangilia ujinga kwa kuangalia tulipoangukia baada ya kuangalia tulipo jikwaa, hivyo kuendelea kujikwaa pale pale na kuanguka tena na tena!.


Paskali
 
Unachokisema ni "pure political satire"!! nakushangaa leo umebadilisha tone unaanza kusense gharika!! ningekuwa nakufahamu ningeweka mzigo; KuBet; USD 200; nakuhakikishia Pasco this time for sure some heads will roll! mbuzi wa kafara hapa hakosekani, tulia uone!
 

ikitokea ni kweli ni fedha za wizi, na yeye kutakiwa kuzirejesha!, asihangaike kuigusa hata senti moja ya pensheni yake!, sisi watu wenye mapenzi mema, tutamfanyia harambee ya siku moja tuu, na fedha zote zitarudi!.
Pasco.

Pasco kwanini usi organize harambee sasa ya kuchangia pesa za maabara za sekondari ili kuwaepushia wananchi wa kule vijijini balaa la kuchangishwa pesa hizo na watendaji wa vijiji kwa ngumi na mateke?
 
what are you saying Pasco?tujiandae kiakili kukubali kusamehe tena,simply because na wengine waliombwa kurudisha walichichita na kusamehewa?tutaendelea na misamaha na kuwa na double standards katika kudeal na uhalifu mpaka lini?mbona wengine wanafungwa kila kukicha na kufilisiwa?
 
Wanabodi,

Naomba kuanza kwa ku declare my interest, Mimi Pasco wa JF, sijapata mgawo wa fedha za escrow, hata senti tano!.
Hii ni kufuatia mtu ukitoa mawazo yako huru tofauti na maoni ya wengi, huchelewi kuambiwa umelipwa!.

Nimeangalia kikao cha Bunge leo asubuhi, waheshimiwa wabunge wetu, huku wakiwa wamehamanika sana, wameishupalia sana ripoti ya ukaguzi wa IPTL huku wakizungumza kwa jazba sana, kuwa kama kuna wahusika, wawajibishwe bila huruma!.

Akijibu swali katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza Peter Pinda, amesema safari hii, hakuna cha Mswalie Mtume!, yoyote atakayetajwa, anakwenda na maji!.

Watu wamehamanika sana na uwajibishwaji, as if ikithibitika escrow ni wizi, basi inaonekana kana kwamba ni bonge la sikandali!, ni bonge la wizi, ni bonge la kashfa!.

Ukweli ni kuwa fedha za escrow sio big deal kihivyo!, kumeishatokea maskandali makubwa zaidi ya uchotaji fedha BOT, escrow ni cha mtoto, na hakuna chochote kilichofanyika!, mfano TanGold, Deep Green, Meremeta, Import Support, DCP, etc, etc, wahusika walifanywa nini?!.

Moja ya viashiria vya utawala bora, ni pamoja na consistance katika utoaji wa maamuzi, ili kuepuka "double standards", na maamuzi na hatua zilizochukuliwa kati similar nature, na lizima zichukuliwe kwa matukio yote ya aina hiyo, yatakayo fuatia, hii kisheria inaitwa "precedence!".

Kwa vile kuliwahi kutokea wizi kama huu, ule wa EPA, ambao nao uliibuliwa na ripoti ya CAG!, na maadamu wahusika wa wizi ule, walitakiwa kurejesha fedha walizoiba!, na kutofikishwa kwenye vyombo vyovyote vya sheria!, then hii ni "precedence" ambayo ni lazima utaratibu huo huo wa kurejesha utumike!. Zile kesi za EPA mlizosikia zikiunguruma, ni kesi za wale walioshindwa kurejesha!.

Miongoni mwa wanaotajwa tajwa kumegewa mgao huo, ni mmoja wa mawaziri wetu waadilifu sana, aliyeomba mchango kwa nia njema kuwasomesha watoto yatima!, ikitokea fedha ni za wizi, kwanza yeye hana kosa lolote kupokea misaada kutoka kwa wasamaria wema!, pili amezitumia fedha hizo for a good cause!, hivyo upokeaji wa fedha hizo ni justified hapa duniani hadi mbinguni!.

Japo pemsheni yake, inamuwezesha kuzirudisha over night!, naomba kumtoa wasiwasi huyo waziri wetu mpendwa kuwa asiwe na shaka wala wasiwasi, ikitokea ni kweli ni fedha za wizi, na yeye kutakiwa kuzirejesha!, asihangaike kuigusa hata senti moja ya pensheni yake!, sisi watu wenye mapenzi mema, tutamfanyia harambee ya siku moja tuu, na fedha zote zitarudi!.

Tupunguze kuhamanikia, escrow sio big deal kihivyo!, EPA ndio ilikuwa big deal na wizi mkubwa!, kama mijizi ile ilisamehewa!, why not wezi wa escrow wasisamehewe?!.

Pasco.

Sisi Waafrika ni mtakataka sana na tutaendelea kuwa Masikini mpaka mwisho wa Dunia hii, hizi kelele zote ni kwa sababu tu humo ndani kuna fedha ya Mzungu, hata EPA ilikuwa hivyo hivyo wanapiga kelele kwa maana Mzungu anataka fedha yake, lkn Madini yetu yanaibiwa kila siku, Gesi yetu inachotwa juu kwa juu huko baharini, Huko Same nasikiaMadini ya Bauxite kwa wasio jua ndiyo yanayotumiwa kutengezewa Aluminium yanachimbwa na kuuzwa nje ya Nchi Mkuu wa Wilaya anajua hilo, Mkuu wa Polisi anajua hilo, Mbunge wa huko analijua hilo kwa Kifupi Serikali inajua lkn kimya, kesho wazungu wakiliongelea Utasikia UKAWA wanaanza kulivalia njuga...

Mbona Serikali wamegoma kutoa mikataba ya Madini na gesi na hakuna Mwamko wowote juu ya hilo? Kwa maana kama ni fedha, fedha inayochotwa na Wazunzu/wahindi kutoka kwenye Madini na gesi haya mambo ya sijui EPA, escrow ni cha mtoto!

tuwekeze nguvu zote kwenye Madini yetu na SIYO sijui EPA au escrow!


 
Pascaoooooo!Wewe acha woga!Usiwe kama kalai lazege jengo likiisha thamani yako kwisha!
 
Issue siyo nani alifanya nini akasamehewa Paschal issue ni kwamba tunataka uwajibikaji na si maneno na kiburi cha PESA ZETU, wanachomekea suruali nzuri, wanakula vizuri,wanaheshimika kwenye familia zao na wake zao kama waume/wake bora kumbe ni pesa za wizi na si za jasho lao,wakati MTANZANIA wa kawaida akinyanyasika kulipa kodi kila bidhaa anayonunua na tayari wameshaanza mpango hadi barabara tulipie NASEMA wamezidi hapana wawajibike na kurudisha pesa zetu.Jaribu kufikiri kidogo tu mwalimu ama mtumishi wa umma analipwa kiasi gani na kwa nini analipwa hivyo wakiambiwa wapandishe walau kima cha chini kifike 315,000/= ni wakali kama MBOGO aliyejeruhiwa na risasi kumbe pesa zipo na wanakula wenye AKILI WACHACHE na Watanzania akitaabika.
 
Pasco,

You're my barometer in pertaining to media (in general) & journalists (in particular) deliberate misinforming the masses both systematically and consistently.

But deep inside I'm still confounded on how weirdo some creatures are really are!
 
na hata mimi nianze kwa kusema hata mimi hata sent moja sijagaiwa.
pili
kama kafulila alivyosema leo bungen huu ni mtihan kwa hili bunge kama kweli wanaishauri na kuisimamia serikali.yetu macho na maskio tuone kama wana hio dhati kutoka moyoni kuisimamia serikali.
 
Back
Top Bottom