Hata Gharika enzi za Nuhu ilianza kama Korona kumbe ndiyo ilikuwa mwisho wa dunia

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Enzi za Nuhu gharika ilivyoanza!
Ilianza kama mzaha!
Walianza kusombwa watoto na walemavu wale wenye mbio walijihesabia kupona!!

Baadae maji yaliingia ndani na kuanza kujaa mabondeni (Mithili ya Bonde I we ni Huko WUHAN- CHINA) Wale wa milimani (mfano AFRIKA) waliwachungulia wa mabondeni na kuwashangaaa na kuwananga Kwa maneno lukuki "walitumwa na nani kuishi huko ", Nani kawatuma kula konokono" acha mafuliko ya mvua yawanyooshe"

Siku zikasonga maji yakajaa; mabakuli,mabeseni,mabwawa na mabonde!
Maji yakaanza kupanda mlimani! Na mataifa (ULAYA NA AFRIKA)

Kilio kikaongezeka, sauti ikawa kubwa zaidi, lakini kulikuwa na mabingwa wa kukwea minazi wakaanza kuwacheka wasojua kupanda minazi! ( mfano" ETI OOH SIYE WAAFRIKA NGOZI NGUMU HAINA MADHARA)

Maji yakazidi kimo cha minazi na mikaratusi! Viumbe wakamezwa. (Kilio cha mataifa kikazidi)

wakabakia wapiga mbizi wakifurahia na kuwashangaa washamba wasojua kuogelea!

Siku zikasonga! Waogeleaji wakaishiwa nguvu na kumezwa wote wakaisha!

Enzi hizo kungekuwa na mitandao ya kijamii tungeona leo selfie za watu wa kale wakiwa juu ya minazi na caption za maudhi huko Instagram!

Hivyo ndivyo ilivyo kwa korona!

Mataifa wanawashangaa wachina wanavyokufa na kuongezeka kila siku! bila Maandalizi huko kwao!

Wapo wanaozarau korona wakiamini haipo ni story tu!
Wapo wanafikili Korona itaishia WUHAN PEKEE!
Korona inaendelea kuuwa hadi madaktali bingwa wa korona lakini dunia haishutuki inaona ni upepo tu utapita!

Korona itavuka Mipaka kimataifa na kuyasogelea mataifa!
Korona itapaa kupitia pesa na sarafu hizi tunazobadilishana kwa mikono katika taasisi za kipesa na mabenki hadi kwa machinga wa mwisho!

Korona itapenya hadi kwa kahaba na makanisani!
Je; umejiaandae kuipokea korona!?

Wa mabondeni wanapofulikwa usishangilie; chukua tahadhali kwasababu hata walio juu na wapiga mbizi walifunikwa na gharika Enzi za Nuhu!

AFRIKA TUJIPANGE MAPEMA!
Alamsiki 29 Feb 2020
 
Enzi za Nuhu gharika ilivyoanza!
Ilianza kama mzaha!
Walianza kusombwa watoto na walemavu wale wenye mbio walijihesabia kupona!!
Baadae maji yaliingia ndani na kujaa mabondeni Wale wa milimani waliwachungulia wa mabondeni na kuwashangaaa walitumwa na nani kuishi huko "acha mvua iwabondoe"

Siku zikasonga maji yakajaa mabakuli,mabeseni,mabwawa na mabonde!
Maji yakaanza kupanda mlimani!
Kilio kikaongezeka, sauti ikawa kubwa zaidi, lakini kulikuwa na mabingwa wa kukwea minazi wakaanza kuwacheka wasojua kupanda minazi!
Maji yakazidi kimo cha minazi na mikaratusi! Viumbe wakamezwa.

wakabakia wapiga mbizi wakifurahia na kuwashangaa washamba wasojua kuogelea!
Siku zikasonga! Waogeleaji wakaishiwa nguvu na kumezwa wote wakaisha!

Enzi hizo kungekuwa na mitandao ya kijamii tungeona leo selfie za watu wa kale wakiwa juu ya mnazi na caption za maudhi!

Hivyo ndivyo ilivyo kwa korona!

Mataifa wanawashangaa wachina wanavyokufa na kuongezeka kila siku!

Wapo wanaozarau korona wakiamini haipo ni story tu!
Korona inaendelea kuuwa hadi madaktali bingwa wa korona lakini dunia haishutuki inaona ni upepo tu utapita!
Korona itavuka kimataifa na kuyasogelea mataifa!
Korona itapaa kupitia pesa na sarafu hizi tunazobadilishana kwa mikono katika taasisi za kipesa na mabenki hadi kwa machinga wa mwisho!

Korona itapenya hadi kwa kahaba na makanisani!
Je; umejiaandae kuipokea korona!?

Wa mabondeni wanapofulikwa usishangilie; chukua tahadhali kwasababu hata walio juu na wapiga mbizi walifunikwa na gharika!
Kwani we umepanga kuishi milele mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaposema mataifa yanawashangaa Uchina inaonyesha hujui kinachoendelea,

Mataifa mengi yametoa misaada ya kifedha na ni juzi tu WHO imetoa wataalamu zaidi ya 500 kwenda Wuhan kuongeza nguvu kupambana na Corona, USA wenyewe wanasubiri tu kuwa invited ili kupeleka wahudumu zaidi wa afya kusaidia kulitokomeza ili jibwana COVID-19.

Huko kenya leo imetokea taharuki kuna mchina alihisiwa anaumwa kumbe siyo
 
Unaposema mataifa yanawashangaa Uchina inaonyesha hujui kinachoendelea,

Mataifa mengi yametoa misaada ya kifedha na ni juzi tu WHO imetoa wataalamu zaidi ya 500 kwenda Wuhan kuongeza nguvu kupambana na Corona, USA wenyewe wanasubiri tu kuwa invited ili kupeleka wahudumu zaidi wa afya kusaidia kulitokomeza ili jibwana COVID-19.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mgeni kashaingia east coast
 
Back
Top Bottom