Hasunga: Sababu inayopelekea ripoti ya CAG kutochambuliwa Bungeni kwa wakati ni muingiliano wa Bunge la Bajeti

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Marco Maduhu
DODOMA
Habari
Nipashe
PAC yataja sababu Ripoti ya CAG kutochambuliwa kwa wakati bungeni

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Japhet Hasunga, amebainisha sababu inayosababisha Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutochambuliwa bungeni kwa wakati, kuwa inatokana na muingiliano wa bunge la bajeti.

CAG.jpg

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Japhet Hasunga, akizungumza kwenye mjadala huo.Kushoto ni aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Prof, Musa Assad.
Hasunga ambaye pia ni Mbunge wa Vwawa, amebainisha hayo jana kwenye mjadala wa ukaguzi wa mahesabu unaofanywa na Taasisi kubwa za ukaguzi wa fedha kwenye Sekta ya uziduaji Barani Afrika, mjadala ambao ulihusisha pia Mkaguzi Mkuu Mstaafu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof; Mussa Assad, na Mratibu wa miradi ya Uziduaji kutoka Shrika la Oxfam, Adella Msemwa, ambao walifanya utafiti wa Ofisi za ukaguzi katika nchi 10 Barani Afrika, katika wiki ya AZAKI ambayo inafanyika Dodoma.

Amefafanua kuwa kuchelewa kujadiliwa kwa Ripoti hiyo ya CAG Bungeni, hua inasababishwa kupelekwa mwezi Aprili, ambapo kipindi hicho hua ni kipindi cha Bunge la Bajeti, na Wabunge hua wanakosa nafasi ya kuichambua hadi wanamaliza Bunge la Bajeti June 30, ambapo bado wanakuwa hawajapanga muda kuichambua Ripoti hiyo.

“Mwaka huu tulitaka kuichambua Ripoti ya CAG mapema, lakini tuliwasiliana na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akatuomba hatuwezi kujadili sababu yeye hajapitia majibu kutoka kwa Maofisa Masuhuli, ili kuthibitisha majibu aliyoyasema kwenye Ripoti yake, na baada ya hapo ndipo tunapata fursa ya kuichambua, mfano Ripoti ya mwaka jana ya CAG ndiyo tumeanza kuichambua Agost, hivyo tatizo linalocheleshwa kusomwa ni muda tu,”alisema Hasunga.

Akizungumzia kwa upande wa Ripoti za TEITI kutochambuliwa bungeni, alisema taratibu na kanuni za kibunge Ripoti hiyo haiingii bungeni kujadiliwa, isipokuwa mbunge mmoja mmoja anaweza kupata hiyo ripoti akaisoma, na kuitumia kutoa mchango wake bungeni na kuonyesha kama sehemu ya utafiti wake, kwamba kuna ripoti hii imeonyesha hiki na hiki na kisha kuishauri Serikali kuchukua hatua.

Pia alizungumzia mapungufu ya sheria na taratibu ambazo zilikuwa zikizuia kuingia kufuatilia kupata Ripoti zote kwenye Makampuni, alibainisha kuwa mwaka 2017 Bunge lilifanya Marekebisho ya Sheria za Madini, kuwa katika kampuni yoyote inayokuja kuchimba madini au kuwekeza kwenye utafiti, lazima Serikali iwe na Hisa kuanzia asilimia 16 hadi 50, kutokana na Thamani ya ardhi na madini yaliyopo.

Katika hatua nyingine Hasunga alisema kuwa kwa sasa bunge lipo kwenye mjadala wa kupitia mapungufu ambayo yapo kwenye taaluma kwa kupitia mashirika ambayo serikali ina hisa zaidi ya 50, pamoja na maeneo mengine ambayo Serikali ina Hisa chini ya asilimia 50, na kutolea mfano Bomba la Mafuta ambalo linatoka Hoima Uganda, na kueleza kuwa wale wanauwezo wa kukaguliwa na Mkaguzi yoyote yule, ambapo kwa sasa wanafikilia kubadilisha utaratibu ili CAG aanze kuwa anakagua na mashirika hayo yaliyo na Hisa chini ya asilimia 50.

Aidha, akiuliza Swali na kutoa mchango wake juu ya Ripoti za TEITI Mkurugenzi wa Taasisi Hakirasilimali Racheal Chagonja, alisema mpaka sasa zimezalishwa Ripoti 11, na katika Ripoti za Mliganisho Tanzania imepoteza zaidi ya Sh. bilioni 90, fedha ambazo zilipaswa kufanyiwa ukaguzi maalumu wa Mahesabu, na kuishauri Serikali kuwa inapaswa kuwekwa jitihada za maksudi kuhakikisha kwamba Ripoti hizo (Special Auditing) ziwe zinapelekwa kwenye Kamati, ili kupata ufumbuzi kujua wapi mapato hayo yalipotea.
 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Japhet Hasunga, amebainisha sababu inayosababisha Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutochambuliwa bungeni kwa wakati, kuwa inatokana na muingiliano wa bunge la bajeti. :oops: :oops: :oops:
 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Japhet Hasunga, amebainisha sababu inayosababisha Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutochambuliwa bungeni kwa wakati, kuwa inatokana na muingiliano wa bunge la bajeti. :oops: :oops: :oops:
kuchambua ripoti ya CAG inahitaji akili. Bunge la sasa ni la mazuzu wakiongozwa na kubwa la mazuzu.
 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Japhet Hasunga, amebainisha sababu inayosababisha Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutochambuliwa bungeni kwa wakati, kuwa inatokana na muingiliano wa bunge la bajeti. :oops: :oops: :oops:
Mkuu haya MAZUZU kungekuwa na namna sasa Mwenyezi MUNGU akatusaidia...dah
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tanzania inaweza kwenda bila Bunge na tukaokoa pesa kibao sioni cha maana wakijadili huko kwa sasa...
 
Back
Top Bottom