Hassan Ngoma: Musiba ni spika tu inayotoa sauti, Dr. Bashiru ashughulike na waya wa spika!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,615
141,439
Mtangazaji wa Clouds tv Hassan Tanzanite Ngoma amemponda mwandishi C. Musiba kwamba anatumika kama spika tu lakini "wanaojua" kinachoendelea ni waya wa spika na mwenye radio.

Ngoma amemtahadharisha Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru kuacha kuwaita ofisini viongozi wastaafu kwa kutumia taarifa zisizo rasmi za mitaani.

Ngoma anahoji endapo ataibuka chizi mwingine huko kilabuni na kudai Mwenyekiti mstaafu anaendesha vikao vya siri je atamwita kumhoji?

Na kama atamwita je kwa fitna hizi atawaita watu wangapi ofisini kwake?!

Ngoma alikuwa anazungumzia sintofahamu ya Dr. Bashiru na Mstaafu Membe iliyotawala mitandaoni kwa sasa.

Source Clouds 360!
 
Mtangazaji wa Clouds tv Hassan Tanzanite Ngoma amemponda mwandishi C. Musiba kwamba anatumika kama spika tu lakini "wanaojua" kinachoendelea ni waya wa spika na mwenye radio.
Ngoma amemtahadharisha Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru kuacha kuwaita ofisini viongozi wastaafu kwa kutumia taarifa zisizo rasmi za mitaani. Ngoma anahoji endapo ataibuka chizi mwingine huko kilabuni na kudai Mwenyekiti mstaafu anaendesha vikao vya siri je atamwita kumhoji?.......na kama atamwita je kwa fitna hizi atawaita watu wangapi ofisini kwake?!!!!
Ngoma alikuwa anazungumzia sintofahamu ya Dr Bashiru na Mstaafu Membe iliyotawala mitandaoni kwa sasa.

Source Clouds 360!
Swala ni je anayoongea Musiba ni sahihi au sio sahihi?Kama musiba kuna mtu anamtuma, je yale anayomtuma ni sahihi au sio sahihi?Je Bashiru kama kiongoz wa juu CCM ambao ndio serikali yenyewe hana taarifa sahihi kuhusu Membe nje ya taarifa kutoka kwa Musiba?Sioni mkihoj usahihi wa taarifa za musiba zaidi ya kumshambulia kuwa ni muongo, huu uongo umethibitishwa na nani?Sijaona mtuhumiwa yyt kutoka hadharani na kumtaka musiba akathibitishe zaid ya kumtia mikwara na kutuma vijana wao jf kuwasafisha. Tumeona mikwara ya zito kumroga, tumeona mikwara ya bulembo kumpeleka mahakaman. Je hii mikwara na kelele za Humu jf zinatosha kusema musiba ni muongo?
 
Hujaona mtu aliyetoka hadharani? Membe si kaomba siku akienda kumuona Dr. Bashiru na Musiba awepo ili aweke ushahidi katibu mkuu amegoma. Musiba kawataja wengi hadi Kinana na Diallo hadi naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mbona hao wengine hawajaitwa? La mwisho who is Musiba hadi ayasemayo yaonekane ni kweli? Anautofauti gani na gazeti la mwanahalisi halisi liliofungiwa kwa kuandika kwa style ya Musiba? Why na hili lisifungiwe?
 
Hivi bado unaangalia huo ujinga na kumuelewa huyo Aliyekuwa kwenye list.namba tatu ya Nkonk Nkonk Nkonk Nkonk Nkonk Nkonk master.
💪💪💪💪💪💪
Ashukuru haikutajwa
 
Hujaona mtu aliyetoka hadharani? Membe si kaomba siku akienda kumuona Dr. Bashiru na Musiba awepo ili aweke ushahidi katibu mkuu amegoma. Musiba kawataja wengi hadi Kinana na Diallo hadi naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mbona hao wengine hawajaitwa? La mwisho who is Musiba hadi ayasemayo yaonekane ni kweli? Anautofauti gani na gazeti la mwanahalisi halisi liliofungiwa kwa kuandika kwa style ya Musiba? Why na hili lisifungiwe?
Membe kaitwa public kwasababu sim zake zote hazipatikani.
Hao wengine wameitwa kimya kimya.....hata Yeye mawasiliano yake yangepatikana angeitwa kimya kimya
 
. Ngoma anahoji endapo ataibuka chizi mwingine huko kilabuni na kudai Mwenyekiti mstaafu anaendesha vikao vya siri je atamwita kumhoji
Nadhani hapa ndipo Ngoma amejikita zaidi whether to inform or not sijui.Ila nafikiri hoja yake kubwa Ngoma ni kuwa Katibu mkuu ndie officially official communicator.Mawasiliano yake na awaye yeyote hasa walioshika nyadhifa kuwaita ni vizuri kuwa official zaidi kuliko majukwaani kwenye hotuba za hadhara kama katibu!
 
Membe kaitwa public kwasababu sim zake zote hazipatikani.
Hao wengine wameitwa kimya kimya.....hata Yeye mawasiliano yake yangepatikana angeitwa kimya kimya
kulikuwa kuna uharaka sanaa kuwa apatikane? Yuko nje ya nchi kwa mujibu wa yeye mwenyewe.Si angeandikiwa barua ikapelekwa nyumbani kwake ya kuitwa? Hana nyumba na nyumbani kwake hamna watu?
 
Hujaona mtu aliyetoka hadharani? Membe si kaomba siku akienda kumuona Dr. Bashiru na Musiba awepo ili aweke ushahidi katibu mkuu amegoma. Musiba kawataja wengi hadi Kinana na Diallo hadi naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar mbona hao wengine hawajaitwa? La mwisho who is Musiba hadi ayasemayo yaonekane ni kweli? Anautofauti gani na gazeti la mwanahalisi halisi liliofungiwa kwa kuandika kwa style ya Musiba? Why na hili lisifungiwe?
Umekuja vizur, Huyo Membe alikua na nafasi ya kumtaka musiba athibitishe before hajaitwa na KM.Nimehoji je Bashiru hana source nje ya Musiba?Nafikiri Bashiru anataarifa zote na sahihi kuhusu Membe na hao wengine. Nakubaliana na wanaosema Musiba ni kipaza sauti tu,yote anayoyatoa yanatoka kwenye system. Je si ya kweli?Membe anajua nini anafanya na hizi tuhuma anajua ukweli wake. Aende huko kwa Bashiru tu.

Swala la Tanzanite kutofungiwa linatokana na wahusika wenyewe kutochukua hatua stahiki dhidi ya gazeti. Zito kaambiwa anatembea na mke wa marehem badala ya kumshtaki musiba akathibitishe ye anakimbilia kumtia mikwara ya kumroga. Je mamlaka inalifungiaje hili gazeti kwa mazingira haya?Gazeti linafungiwa pale walalamikiwa wanaposhindwa kuthibitisha kile walichoandika. Sio jukumu la serikali kumhoji musiba coz serikali sio mtuhumiwa. Gazeti la mwanahalisi lilifungwa coz serikali kama mtuhumiwa waliomba uthibitisho na gazeti likashindwa kuthibitisha.

Serikali haiwez kufunga gazeti eti kuna watu wametuhumiwa. Serikali inafunga gazeti baada ya wahusika kulalamika na gazeti kushindwa kuthibitisha. Huwa tunasema hao wote wanaotuhumiwa na musiba kwanini wasifuate taratibu zaid ya kutuma vibaraka wao humu jf kuwatetea?Mtu anakwambia oooh musiba anatumiwa, kutumiwa sio hoja hata kidogo. Hoja ni je anayotumiwa ni KWELI?Mi naamin wengi wanaotuhumiwa na musiba wanajua ukweli wake na wanajua wakisema wapambane naye basi watabaki uchi. Alikuwepo Kubenea, naye alikua anaandika vitu nyeti sana lkn kwakua wahusika walikua wanajua ukweli wa kile anachoandika nao pia walikua hawajitokez kujibu zaid ya kukimbilia kumwagia tindikali na kutuma vijana wao jf kuwasafisha.
 
Back
Top Bottom