Hassan Moyo Mwasisi Muungano alipua jipu Muungano ulivyozunguka Mbuyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hassan Moyo Mwasisi Muungano alipua jipu Muungano ulivyozunguka Mbuyu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 22, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Shamsha Vuai Nahodha
  akila kiapo cha uwaziri Serikali ya Muungano

  Moyo, Shamsi wavutana suala la Muungano

  Mwanasiasa Mkongwe Zanzibar Hassan Nassor Moyo, amesema kwamba wakati mazungumzo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanafanyika, Msaidizi Mkuu wa Rais wa Kwanza Zanzibar, Salum Rashid alikuwa kwa kinyonzi akinyoa ndevu zake. Tamko hilo amelitoa wakati akiwasilisha mada kuhusu uzoefu wa viongozi waliopita katika masuala ya Muungano katika semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW) huko Chukwani Zanzibar jana.

  Alisema kwamba Rashid, alikuwa Katibu Mkuu (Ikulu) wakati wa uongozi wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Sheikh Abeid Amani Karume, baada ya kumuondoa katibu wake kutokana na kuhudhuria mazungumzo hayo akiwa hajanyoa ndevu zake.

  Alisema Aprili 14, 1964 aliyekuwa Rais wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alimwita Rais wa Zanzibar Ikulu ya Dar es Salaam, kufungua mazungumzo ya mpango wa Muungano wa Tanganyika Zanzibar. Hata hivyo alisema baada ya Karume kufika Ikulu alimkuta msaidizi wake amewasili akiwa hajashevu ndevu na kumtaka achukue gari na kwenda kwa kinyonzi. “Baada ya kurudi kutoka kushevu ndevu kwa kinyonzi alikuta wanaendelea ndani na mazungumzo lakini kwa kuzingatia itifaki hakuweza kuingia ndani.”alisema Mzee Moyo.


  Alisema kwamba Aprili 22, mwaka huo Mwalimu Nyerere alikuja Zanzibar kukamilisha mazungumzo ya Muungano lakini wasaidizi wake wa muhimu mzee Karume aliwatenga na kuwaweka katika ‘korido’ wakati waziri wake wa Nchi Ofisi ya Rais wakati huo Aboud Jumbe Mwinyi akiwa safari ya kikazi Pemba.


  “Baada ya mazungumzo Karume alimwita msaidizi wake Salum Rashid na kumpatia waraka wa muungano amsomee kifungu kwa kifungu na kutafsiri kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ulikuwa umeandikwa kizungu kabla ya kusainiwa”. Hata hivyo alisema Mjumbe wa BLM Khamis Abdallah Ameir, alitaka kufahamu kwa nini mpango huo unafanyika harakaharaka lakini Karume alimuondoa wasiwasi na kuwaeleza wajumbe kama hawataki yupo tayari kumrejeshea makaratasi yake Nyerere lakini Wajumbe wote waliunga mkono mpango wa Zanzibar kuungana na Tanganyika.


  Alisema Baraza la Wawakilishi (BLW) lina mamlaka kamili ya kukubali kuendelea kuwepo kwa Muungano au kukataa kwa sababu ni chombo cha wananchi kama Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM). Moyo alisema kwamba chimbuko kubwa la muungano huo ulitokana na hofu ya vitisho vya Zanzibar kupinduliwa iliyokuwa ikitolewa na baadhi ya viongozi kutoka Afrika Mashariki.


  Moyo alisema kero za Muungano zimeanza kuibuka muda mrefu na kutoa mfano mwaka 1970 kulitokea kishindo baada ya Zanzibar kupendekeza waraka wa kutaka baadhi ya mambo kurekebishwa katika orodha ya mambo ya Muungano ikiwemo kuondoa Jeshi la Polisi.


  Wajumbe waliochangia mada hiyo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, ambaye alivutana kwa muda mrefu kutaka maelezo ya kina, Hamza Hassan Juma, (Kwamtipura) Ismail Jussa ladhu, (Mji Mkongwe) Makame Mbarouk Mshimba (Kitope) Salim Abdalla Hamad, (Mtambwe) na Fatma Mbarouk, (Amani).


  Hata hivyo Mzee Moyo, alishindwa kujibu maswali mazito ya Nahodha aliyetaka kujua kwa nini nafasi ya Zanzibar kiulinzi na kiusalama iwe nje ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Shamsi alisema kwamba miaka 7 baada ya Mapinduzi Zanzibar kumefanyika majaribio 14 ya kutaka kuinagusha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Semina hiyo imeandaliwa na Baraza la Wawakilishi (BLW) na kudhaminiwa na serikali ya Norway, ambapo pia elimu juu ya Katiba inatarajiwa kutolewa katika majimbo 50 ya Zanzibar.
   
 2. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,386
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  je Mzee Nassor yeye aliingia kwenye mazungumzo hayo? kama hakuingia nadhani na yeye anachosema si cha kuamini sana.
  kikubwa hapo ni hati ya mwanzo ya muungano inasemaje na iko wapi? hiyo inaweza tafsiriwa na watu kuupata ukweli
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Shamsi Vuai ni mjumbe wa BLW (kwa kuchaguliwa), wakati huo huo ni mbunge kwenye bunge la muungano (kwa kuteuliwa)!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hassan Moyo alikuwa mmojawapo wa viongozi wa juu serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Karume alikuwa na mfumo wa kidictata ndio maana hata katibu wake tu alitolewa nje ili wajadili na Nyerere peke yao

  Wakati huo huo Karume alikuwa mbumbumbu wa kimombo, alihitaji mtu wa kumtafsiria.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Shamsha Vuai ana usongo na Muungano, kwani bila Muungano alishakuwa Rais wa Zanzibar, lakini Muungano hasa wajumbe toka bara walimpitisha Shein. Hilo ni moja wapo kero kubwa la Muungano ambao unawaudhi wazanzibar kuchaguliwa mgombea wao wa Rais wao na wabara.
   
 6. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Mjumbe kwa kuchagaliwa sidhani. Nakumbuka (if i may recall) kama alipigwa chini na wananchi uchaguzi uliopita.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Very interesting...but I have some faith on Nahodha, weather muungano utakuwepo au utaishia mitini. Wengine wamekaa kama wapiga story zaidi.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama Vuai alipigwa chini na wananchi wa Zanzibar, kwani alikuwa kipenzi chao sana tu.

  Ukweli ni kwamba CCM ilikusudia kumpitisha Shein wa Pemba ili kuvuta watu wa Pemba wampigie kura ili kumgaragaza Maalim seif. Angepitishwa Vuai maana yake Pemba yote ingempigia kura Maalim na ungekuwa mwanguko babu kubwa wa CCM visiwani.

  Ikumbukwe kwamba uteuzi wa jina la Mgombea wa Urais Visiwani hupigiwa kura na wajumbe wote wa mkutano Mkuu wa CCM bara na visiwani, wengi wa wajumbe wakiwa ni wa kutoka Bara. Nakumbuka ililalamikiwa mara kadhaa kwamba wabara ndio wanaowachagulia mgombea urais.
   
 9. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muungano wa Tanzania, Haukuja kwa kutania,
  Viongozi wake walidhamiria, kuimarisha udugu wa asilia;
  Hata uamsho wakilia, na hasan nasor moyo kuwasaidia;
  BLW pia likiwasaidia, hapatakua na maridhia;
  Juliasi Mwalimu alituambia, na Sheikh Karume alituusia;
  Tumeungana kwa nzuri nia, kutengana kutaleta udhia;
  Tuuenzi Muungano wetu, Bara na Visiwani PIA.

  MIMI nasema kuna KERO ZA MUUNGANO

  KERO hizi za MUUNGANO zinahusu ZAnzibar na Zinahusu TaNganyika.


  TUZIFANYIE KAZI KERO HIZO

  SIO KUVUNJA MUUNGANO


  KAMA KUNA KICHAA ANASEMA MUUNGANO UPO UPO TU; HUYO LAZIMA NI MGONJWA WA MIREMBE.


  Tuna Miaka 48 ya Muungano

  Marais wa Muungano Wanne

  Marais wa Zanzibar Saba

  Mawaziri Wakuu 12.


  JAMANI
   
 10. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Vuai aligombea uwakilishi bana! nafikiri jimbo la mwanakwereke jambo ambalo limawakera wazanzibar kweli kwa kuonyesha uchu wa madaraka/waziri kiongozi hadi uwakilishi!
   
 11. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  karume alikuwa sahihi kumwambia msaidizi wake akanyoe ndevu kwani hata vurugu za sasa hivi zinasababishwa na watu wasionyoa ndevu
  kama msaidizi wake alipewa kazi ya kutafsiri ni wazi alikuwa na uwezo wa kutoa maoni kwa kile alichokishuhudia kwani bado mkataba ulikuwa haujasainiwa mi nawashauri wazanzibar wasizunguke sana kama hawataki muungano wajitoe kelele zote za nini
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Utetezi wako unaweza kuwa sawa na pia una mapungufu kadhaa katika kutoa taswira ya hali ya Muungano.

  Hali ya Muungano wa Tanzania ni sawa na shamba ukishalilima na kupanda miche unakaa tu na kusubiria mazao kukomaa bila kuangalia mambo mengine ambayo yanaweza kusitisha ukuaji na upatikanaji wa matunda yanayotazamiwa.

  Kupalilia shamba, kung'oa magugu, na kuua wadudu au kulinda wanyama waharibufu ni mambo muhimu katika kulinda shamba lako lizalishe matunda stahiki.

  Matatizo mengi yaliyotikea na yanayotokea na kuwa kero zisizovumilika kwa wakati huu ni kutokana na kasoro ambazo zimelalamikiwa miaka kadhaa na kuzikwepa kuzitatua, leo ni donda ndugu. Hii ni kutokana na funikafunika.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sorry, Shamsha Vuai Nahodha alikuwa mmojawapo candidate wa Urais Visiwani Zanzibar pamoja na Makamu wa Rais wa sasa Serikali ya Muungano.

  Kama unakumbuka Kule Dodoka kwenye Mkutano Mkuu wa CCM kuteua wagombea urais Zanzibar na Muungano, Shamsha Vuai alisindikizwa na Rais wa zamani wa Zanzibar Komandoo ikiwa ni nadra sana Komandoo kutua Dodoma tangu amalize muda wake wa utumishi wa urais Zanzibar.

  Pata shika ilikuwa Dodoma ambapo Wazenj walizidiwa kete na wabara kwa hoja kwamba kupigia kura wagombea kulifanywa na wajumbe wote wa bara na visiwani huku wajumbe wa bara wakiwe wengi kuliko wa visiwani.

  Bara walimfahamu zaidi Shein na walifanya kila kinachowezekana kumpisha huyu kwani wagombea wengine walionekana kuwa hawako karibu zaidi na bara na pengine wanaweza kuibua yanayoshindiliwa na serikali ya Muungano kuhusu matatizo ya Muungano. Shein alionekana atakuwa tayari kulipa fadhila kwa kuwa msikivu na mtulivu kuliko akina Vuai.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo la wasio na elimu mara nyingi katika kuongoza hutumia zaidi mamla kuliko argument. Karume alikuwa na mfumo wa kiutawala wa kiimla na wa kisultani. Muungano ulikuwa niridhaa yake na Nyerere kwa kuahidiwa kuwa anatakuwa Makamu wa Rais akiwa na nguvu za kisiasa hadi bara ikamfanya Karume aingie kichwa kichwa.
   
 15. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna hata moja lisiloweza kutatulika na lililofikia hadi kusema uvunjike.

  Hilo halipo

  na huo kamwe sio utetezi wangu, ni mtazamo

  juliasi

  na abedi

  lazima tuwaenzi

   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni kweli hakuna lisilowezekana kutatulika, lakini je tunapokwepa kuzitatua kero hizo za Muungano tusingefikia kiwango cha leo. Tatizo ni kukwepa matatizo na kuyafunikafunika kusubiria watakaofuata ndio watakaoyatatua na ndio mbio za kupokezana vijiti kila anayefuata nakwepa kutatu hadi kufikia uozo wa donda ndugu kutovumilika.

  Karume na Nyerere historia itawaenzi, lakini si kigezo cha kuacha kutatua matatizo na kurekebisha kasoro zake.
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kichekeso kisicho cha kawaida kumtoa mtu kikaoni kwa ajili ya kunyoa ndevu wakati kikao kinaendelea, dalili tosha ya kukosekana ustaarabu na kuendesha mambo kisultani. Kwa nin hawakumsubiri arudi baada ya kunyoa ndevu ndopo kkao kiendelee? Maana yake ilikuwa mbinu ya kumwondoa asijue nini kinaendelea katika mazungumzo yao na Nyerere.
   
 18. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  If the truth be told wenye CCM are not passionate about the union they are passionate about protecting the status quo, that is bound to be severely shaken should the union break-up. CCM wili loose relevance or put more poignatly nnje ya muungano hamna CCM ipo TANU na ASP at best. If wenye CCM were Pan Africanist at heart how do you explain their dogged resistance to establishment of EA federation?
   
 19. N

  Njele JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Una point nzuri. Kuanzishwa kwa CCM ilikuwa ni njia ya kuzika ASP na TANU ili kuziba zaidi matatizo yaliyokuwa yanajitokeza katika utendaji wa serikali ya vyama tofauti kutoka nchi zilizoungana. Tatizo lililobadilika ni kuwa na bendera moja ya chama cha siasa wakati Zanzibar ingali ni ASP. Maana ya Muungano ilikuwa kufanya taifa moja, lakini kwa namna moja au nyingine waliodhoofisha zaidi Muungano ni wazanzibar ambao wanataka haki kimataifa.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hapa nadhani watu wanahasira ya juzi kupigwa waislam wenzao. Nchimbi anatumia vibaya madaraka yake
   
Loading...