Hassan Kinyozi na Ahmed Seif Waajiriwa wa Kwanza wa TANU Southern Province, 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,839
30,168
HASSAN KINYOZI NA AHMED SEIF: WAAJIRIWA WA KWANZA WA TANU SOUTHERN PROVINCE 1955
Bingwa wa historia ya Tanganyika John Iliffe amepata kusema kuwa historia ya TANU iko mikononi mwa watu binafsi.

Iliffe alisema maneno haya katika miaka ya 1960 alipokuwa mwalimu wa historia Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki, Dar es Salaam.

Historia ya TANU ndiyo kama hivi lazima uitafute kwa wenyewe waliounda chama hicho na kukitumikia hadi uhuru ukapatikana na hawa walikuwa watu wa kawaida sana.

Kwa sasa historia hii inapatikana kutoka kwa familia za wazalendo hawa.
Nimefarajika kuona ndugu wa marehemu Hassan Kinyozi wanaojua historia ya mzee wao wameniletea hadi picha ya matayarisho ya mazishi nyumbani kwa marehemu ambako pia ndipo ilipokuwa madrasa aliyokuwa akisomesha.

Madrasa hii iliasisiwa na baba yake Sheikh Mohamed Said Kinyozi.

P:icha ya kwanza ni Hassan Kinyozi ya pili Ahmed Seif na ya tatu ni nyumba ya Sheikh Hassan Kinyozi.

1668574016599.png
1668574040524.png
1668574070091.png
 
Back
Top Bottom