"Hassan Dilunga" ameonekana ameitwa kimakosa timu ya Taifa hivi hapa ni nani mwenye matatizo?

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,492
188,640
Habari.

Duniani hata siku moja hakukosi vituko kabisa hasa TFF.

Kuna taarifa hapa imeleta taharuki kwa wapenda soka baada ya mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi Hassan Dilunga kutemwa nje ya kikosi cha timu ya taifa baada ya masaa machache kupita.

Mwanzoni alionekana yumo kwenye orodha iliyotangazwa kwa umma ila baada ya mijadala sehemu mbalimbali kutokea, TFF wametoka kifua mbele na kusema jina la mchezaji huyu, Hassan Dilunga liliandikwa kimakosa.

Walikusudia kumuita mchezaji wa Azam Mudathiri Yahya na si Hassan Dilunga.

Sasa kwa tukio hili tumtazame nani aliyekosea ni kocha au TFF?

Kama ni kocha basi nini kilitokea au kuna tafsiri hakuna ushirikiano wa kutosha kutoka kwa TFF?

Pia tujiulize mbona jina limebadirika baada ya gumzo kwenye vyombo vya habari na social media?

Hivi hawa TFF wanasimamia majukumu yao vyema maana kwa taarifa hii ni aibu sana kwa viongozi wote na safu nzima.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu

View attachment 1800486
 
Unafahamu vzr maana ya TAHARUKI?
 
TFF ni tatizo sana....pale wanachowaza ni mechi ya Simba na Yanga tu...nje ya hapo ni sifuri ......
Kuna tatizo kubwa sana pale ila naamini mwisho umekaribia wa haya madudu maana dalili zimeanza kuwa nyingi.
 
Mwanzoni alionekana yumo kwenye orodha iliyotangazwa kwa umma ila baada ya mijadala sehemu mbalimbali kutokea, TFF wametoka kifua mbele na kusema jina la mchezaji huyu, Hassan Dilunga liliandikwa kimakosa.
Ni ishu ndogo na imeshatolewa ufafanuzi, ila kwa kuwa kuna wabongo wanapenda vijiwe vijiwe, itakuzwa ionekane kama stori. Tuache mpira uchezwe uwanjani, walioitwa wacheze, wasioitwa wacheze mazoezini, timu za vilabu zicheze mpira uwanjani, ujanja ujanja wa kuhamishia mechi za uwanjani kwenye mijadala ya vijiwe uishe! Tupeleke timu uwanjani, tuache visingizio
 
Huwenda walimpa nafasi kisha wakabadili maamuzi ya kumtema,ila kwenye kujipanga kutoa maelezo ndo hawakujipanga,kusema walimpendekeza kimakosa walikusudia Mudathir wakakosea na kuandika Dilunga wanaonyesha utahira uliokita mizizi kwenye kuongoza soka.
 
Hamna lolote jina hawakuandika kimakosa Wala nn walidhamiria tuu jamaa aitwe kwenye timu baadae nafsi zikawasuta wakaamua wasingizie jina lake limekosewa
 
Wallace atakuwa alilazimisha wamuandike halafu baadae akajistukia akawaambia wamchomoe fasta!
 
Back
Top Bottom