Hassan Bumbuli na Haji Manara 'mnagombania' nini hadi 'mnatukanana' Matusi ya Nguoni katika 'WhatsApps' zenu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
GSM binafsi tena hapa hapa JamiiForums nakumbuka nilianzisha Uzi Kuwaonya kuhusu Kumleta Yanga SC Haji Manara nikawaambia kuwa mmeandaa Bomu ambalo litakuja Kulipuka na Kuwagharimu Yanga SC na sasa yametimia.

Kamarada (Comrade) wangu (Kitasnia) Msomi Mwerevu Hassan Bumbuli nawe nilikuonya hapa hapa JamiiForums kuwa kutokana na ule ujio wa Haji Manara hapo Yanga SC kwa Uweledi wako na Hadhi yako ungeachana tu na Yanga SC na urejee zako MWANANCHI ( MCL ) hasa katika Gazeti lako la Mwanaspoti lakini ukanipuuza na sasa yametimia kwani nilichokitabiri Kwenu kimetimia.

Hopeless ( Mpuuzi ) Haji Manara wala sitopoteza muda mwingi nawe kwani nawe nilikuonya na Kukuambia kuwa Kitendo chako cha Kuwashambulia (tena personally kabisa) akina Mohammed Dewji (Mwekezaji Simba SC) na Barbara Gonzalez (CEO Simba SC) halafu Wao wanakunyamazia ni Ishara tosha ya Laana Kubwa na Mbaya itakayokutafuna na sasa nilichokitabiri Kimetimia.

Kamarada (Comrade) Hassan Bumbuli hivi unajisikiaje Nwenzako Haji Manara Kununuliwa Gari jipya aina ya PRADO, kuhamishwa kutoka Mikocheni alikokuwa akiishi mwanzo na sasa akipangiwa Nyumba Slip Way Masaki na akikuzidi Mshahara mara 15 wakati Kazi Kubwa na Nyingi za Yanga SC (hasa zile za Kiutendaji) zinafanywa na Wewe tu?

Huenda pia (Kamarada Hassan Bumbuli) ile laana ya Kumtukana vibaya Mtendaji Mwenzako (aliyekuwa Mhamasishaji) wa Yanga SC Antonio Nugaz ikawa inaanza Kukutafuna na Kukuumiza kwani kiukweli hukupaswa Kumtusi vile na nakumbuka pamoja na Kumtukana kote kule (Nugaz) bado alikuomba Radhi yaishe ukakataa na mwishowe akasema anamuachia Mwenyezi Mungu na sasa Mola/ Maulana nae ameanza Kumjibia.

Hata hivyo Kamarada (Comrade) Hassan Bumbuli nikushukuru tu kwa zile Video Mbili ulizomtumia (mpostia) Hajj Manara akiwa Dubai (Uarabuni) Kwao na Gharib Said Mohammed (GSM) huku Kaka yake 'akiupiga mwingi' kwa Manara wakiwa Wamesimama katika Hafla ya Kifamilia na ile ya Juzi kule Kisiwani Zanzibar aliyokuwa akimlazimisha Kumvuta karibu Injinia Hersi Said na Injinia akawa anakataa hali iliyopelekea jana katika Mchezo wenu dhidi ya Azam FC Injinia Hersi amkimbie na amkwepe Manara kwa Kukaa nae karibu.

Niliwahi kuwaambieni wana Yanga SC (wa hapa Jamvini JamiiForums) kuwa kama kuna Kazi rahisi na nyepesi Kwangu basi huwa ni kupata Habari Ngumu na zilizojificha kabisa za Kuihusu Yanga SC kama Timu, Wachezaji wake na mpaka Watendaji wake kwani huko nina Watu wengi wengi 'very Loyal' Kwangu na huwa hawanifichi Jambo lenu kama hili la Leo na yaliyopita.

Najua Kesho au Keshokutwa au huko mbeleni mtajitahidi Kukanusha hili ila nami GENTAMYCINE nawaambia kuwa nina 'Skendo' yenu nyingine ila kwa sasa naiweka (nawaweka) Kiporo nasubiri ama Mfungwe au Mtoke Sare na Coastal Union FC Jumapili hii (ijayo) kule Mkoani Tanga ili mkianza Kuvurugana (Kugombana) tu basi nami nikoleze Moto wangu kwa Kuiweka hadharani kwani 'Unyama Unyaman' kwa sasa.
 
Bumbuli mjanja sana. Alijua ile Prado ni mtego. Akaikaushia. Msaliti wetu akaipokea fasta hivi sasa anaitumikia.

Yaliyojiri Dubai anayajua mwenyewe

Maana hata Kabwili alianza hivihivi kimasihara.

NGUVU MOJA.

Hakuna mwiko wala nini.... mwiko hukohuko nyuma yao
 
Uongee mara ngapi tena Mkuu wakati unaambiwa kuna bonge la Fukuto huko Yanga SC hasa kwa hawa Watendaji Wawili Bumbuli na Manara na kuna lingine hilo la Wanachama na Injinia Hersi Said kutokana na Kauli yake ya Kuwadharau?

Tegeni tu Sikio Wakuu kuna Moto huko.
Mkuu mwaga tu hilo fukuto ili watifuane sisi huku tunachukua kombe la mapinduzi wao wawe wanautoa mwiko nyuma
 
Nakuaminia kwa kuchimbua yalio nyuma ya pazia
Asante Mkuu ila hii mbona ndogo tu kuna Kubwa lao subiria Jumapili ama Wafungwe au watoke Sare na Coastal Union FC ya Tanga pale Mkwakwani Stadium ambapo najua Watavurugana na Mgogoro kuanza ambapo nami sasa ndipo hapo hapo naiweka Hadharani ili Waparaganyike zaidi kisha Waharibu Mechi zao zote za NBC Premier League na zile za ASFC.
 
Asante Mkuu ila hii mbona ndogo tu kuna Kubwa lao subiria Jumapili ama Wafungwe au watoke Sare na Coastal Union FC ya Tanga pale Mkwakwani Stadium ambapo najua Watavurugana na Mgogoro kuanza ambapo nami sasa ndipo hapo hapo naiweka Hadharani ili Waparaganyike zaidi kisha Waharibu Mechi zao zote za NBC Premier League na zile za ASFC.
Alaaaa! Kumbe Mkuu lengo lako ni kuiona timu yao IKIHARIBIKIWA tu?
 
Back
Top Bottom