Hasira za Wazanzibar kuchoshwa na Muungano

mtu akitaka kuelewa mantik ya mabadiliko ya katiba ya zanzibar ni muhim kwake kwanza afaham nature ya huu muungano wetu..walichofanya wanzazibar ni kuunda katiba yao inayofuata matakwa ya muungano...so mabadiliko ya katiba ya zanzibar ni halali sana sana

Ndugu yetu hebu msome vizuri Sh Awadh hapo

Katiba ya Muungano 1977 kujenga hoja yake. Mbona amekinukuu nusu?
"Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka…."
Lakini kwa mshangao utagundua kuwa kifungu hicho kinaendelea kumalizia kama ifuatavyo (lakini mwandishi ameona hiyo sehemu ya mwisho ya kifungu hicho asiinukuu, kwa nini, haieleweki)
"… na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka
."

na pitia hapa

Lissu anaposema ilikuwa vema mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yakafuata misingi ya sheria anaonyesha kuwa sheria zimevunjwa. Hilo si kweli. Kwanza, yapasa atambuwe kuwa ni fikra potofu kuamini katiba ya Muungano ndio katiba mama na ile ya Zanzibar ni mtoto. Katiba zote hizi ni sawa kisheria. Katiba ya Zanzibar ina nguvu juu ya mambo yote ya Zanzibar (yasiyokuwa ya Muungano) wakati ya Muungano ina nguvu kwa mambo ya muungano na yale ya Tanganyika.
 
Tanganyika haijafa bali imelala ..... itazinduka usingizini siku moja

Mi nafikiri Tindu Lisu angetumia taaluma yake kuhakikisha mnalirudisha jina na utaifa wa Tanganyika badala ya kukuupuka na kuingilia mambo ya Zanzibar.

Ashindwe na alegee
 
wabara tunaitaka Tanganyika yetu.
Dah kijana nakuonea huruma ,,,nashangaa sana munadai katiba wakati tanganyika haipo, chadema kama kweli walikuwa ni watetezi wenu basi walete mjadala wa tanganyika irudi,,,,,

Ingiie bara bani vijanaa
 




Na Awadh A. Said
MAKALA ya Tundu Lissu iliyochapishwa na gazeti hili chini ya kichwa cha habari, Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi imenishawishi kutoa maoni kwa kuona inaelekeza watu sivyo.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mwenzangu, anasema mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yamedhoofisha muungano wa Tanzania kwa “kumong’onyoa misingi karibu yote ya muungano huo, kubadili sura ya muungano wenyewe, mipaka yake na muundo wake.” Ana khofu mabadiliko hayo “yanaweza kuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa Muungano na hata tishio kwa usalama wa mipaka ya Taifa.”
Anaamini mabadiliko hayo yaliitangaza Zanzibar ‘‘kuwa nchi yenye mipaka kamili” na kwamba “Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa.” Anaegemea kifungu cha kwanza cha Katiba ya Zanzibar kabla ya marekebisho, kinachosema, ‘‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Hapa kuna mambo mawili: Kwanza kuwa mabadiliko hayo ndio yaliyoitangaza Zanzibar nchi, na pili ndiyo yaliyobainisha mipaka ya Zanzibar ambayo mwanzo haikutajwa. Yote haya si kweli.
Zanzibar ilianza kuwa na katiba yake ya kwanza baada ya Mapinduzi ya 1964. Ilikuwa mwaka 1979. Baadaye ilifutwa na kuandikwa upya mwaka 1984 ilipoandikwa inayoendelea mpaka sasa. Ndiyo iliyofanyiwa marekebisho mara 10 yakiwemo haya yanayojadiliwa sasa. Je, Katiba hiyo haikutaja Zanzibar kama nchi hadi yalipokuja mabadiliko ya kumi? Ni kweli Katiba ya Zanzibar ya 1984 kabla ya marekebisho ya kumi ilieleza katika kifungu cha 1 kuwa “Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Lakini ukiwacha kifungu hicho, vifungu kadhaa au tuseme katiba yote inaitaja Zanzibar ni nchi.
(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …
(10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:
(10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.
(12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.
(21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…
(23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…
Inaonyesha Lissu alitazama tu kifungu hicho cha kwanza, akapuuza vingine. Katiba ya Zanzibar imebaki na idadi ileile ya vifungu 135 hata baada ya marekebisho ya kumi.
Msingi mkuu wa katika kanuni za kutafsiri sheria, ni kuwa ili uweze kupata tafsiri sahihi kwa waraka wowote (iwe ni Katiba, Sheria, Mkataba n.k.) unapaswa kusoma waraka wote ndipo upate maana, tafsiri au dhamira inayopatikana katika waraka huo kuhusiana na jambo husika. Ni dhahiri huwezi kuchopoa kifungu kimoja tu ukapata usahihi.
Hebu tuangalie hichohicho kifungu cha kwanza kisemacho ‘‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano.” Ni sawa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri Ya Muungano, lakini inasimama katika utambulisho upi? Ni sehemu kama Mkoa, Wilaya, Tarafa, Jimbo, Kata au kitongoji? Zanzibar ina katiba yake, ina Rais wake, ina Mahkama zake, ina mawaziri wake, ina Baraza lake la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi), ina watu wake (tena wana vitambulisho), ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Mamlaka yake ya serikali za mitaa, ina magereza yake (Vyuo vya Mafunzo), ina vikosi vyake maalum vya ulinzi, ina mapato yake na bajeti yake n.k. Jee kuna Mkoa au Wilaya yenye yote hayo? Na yamekuwepo kabla ya mabadiliko yaliyofanywa.
Lissu anasema, “Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa.” Kabla ya mabadiliko ya kumi, Katiba ya Zanzibar 1984, kifungu cha 2(i) kinasema:
2(i) “Eneo la Zanzibar ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.” Baada ya mabadiliko ya kumi, kifungu hicho kinaendelea kuwepo kikisema: Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.”
Hoja ya pili ya Lissu ni mabadiliko haya yanadhoofisha Muungano kwa vile yameondoa mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika mikoa kutoka mikononi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kuweka mamlaka hayo kwa Rais wa Zanzibar. Hili ni kweli limefanyika katika mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar. Tujiulize sababu. Inaeleweka wazi kuwa ni Rais wa Zanzibar ambae kipindi chote tokea Muungano wa Tanzania uasisiwe 1964, ndie anayeigawa Zanzibar katika mikoa na wilaya.
Hakuna kumbukumbu inayoonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano amewahi kuigawa Zanzibar katika Mikoa au Wilaya. Sasa kwa takriban miaka 47 mamlaka hayo yalikuwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kikatiba lakini kiutendaji na kiutekelezaji Rais wa Zanzibar ndiye aliyekuwa anatekeleza mamlaka hayo. Mabadiliko yametambua hilo na kurekebisha. Haiwezekani tukadumisha vifungu ndani ya katiba ambavyo vinaonekana ni pambo tu. Bali hili litoshe kuonesha mkanganyiko unaozikumba katiba zetu mbili.
Hoja ya tatu ya Lissu ni kuwa mabadiliko ya kumi yamepunguza mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Anasema: “Mabadiliko yamekiuka katiba kwa kuinyang’anya Mahakama ya Rufaa mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.”
Hata mara moja tangu ianzishwe, haijawahi kutokea kwa Mahkama ya Rufaa kuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahkama Kuu ya Zanzibar. Katiba ya Zanzibar iliipa mamlaka mahkama hiyo kwa baadhi ya kesi tu.
Kifungu cha 99 cha Katiba ya Zanzibar kinasema, Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kusikiliza rufani toka Mahkama Kuu ya Zanzibar isipokuwa kesi zozote zinazohusika na:
Tafsiri ya katiba hii
Mambo ya kiislamu ambayo yameanza katika Mahkama za Kadhi.
Mambo mengine yoyote yaliyoainishwa katika katiba hii na sheria nyengine yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
Ndio kusema mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar hayakuongeza kitu kwani pamoja na ukweli kwamba mahakama hiyo haitokuwa na uwezo wa kusikiliza rufani kutoka Mahkama Kuu ya Zanzibar iliyotokana na mambo kuhusiana na vifungu vya haki za binadamu, inajulikana mamlaka ya Mahkama ya Rufaa ya Tanzania kwa Zanzibar ni kwa baadhi ya kesi tu.
Ieleweke kuwa kifungu cha 99(b) cha Katiba ya Zanzibar kimetaja kwa ufupi tu “mambo yaliyoanzia Mahakama ya Kadhi” lakini kwa mujibu wa Sheria Na. 3 ya mwaka 1985 iliyounda Mahakama ya Kadhi, mambo yote yanayohusu ndoa, talaka, mirathi na haki stahiki za mtoto yanasikilizwa katika mahakama za kadhi endapo wahusika wote ni waumini wa dini ya Kiislamu.
Hivyo pamoja na ukweli wa kuwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar kwa kutumia kifungu cha 99(c) yameondoa uwezo wa Mahkama ya Rufaa kusikiliza masuala ya haki za binadamu, hakuna jipya. Lakini hata kama tukihoji busara iliyotumika katika kuliondoa suala la haki za Binadamu katika mamlaka ya Mahakama ya Rufaa bado si sahihi kujenga hoja kama kwamba hili la kuondoa baadhi ya mambo katika mamlaka ya Mahkama ya Rufaa ni jambo jipya lililokuja kwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar.
Lissu anasema mabadikilo ya Katiba ya Zanzibar yamekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano na kudhoofisha Muungano kwa vile sasa Zanzibar “imehalalisha uwepo wa vikosi vya Jeshi vya SMZ inavyoviita Idara Maalum.” Idara Maalum imekuwepo hata kabla ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ikijumuisha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (cha wahalifu) na kifungu hichi hakikubadilishwa hata nukta wala namba za vifungu.
Lakini tujiulize hivi Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina uwezo wa kuunda majeshi? Tena tutumie hiyohiyo katiba ya Jamhuri ya Muungano aliyozungumzia Lissu.
Ni kweli, kama alivyosema kuwa ibara ya 147(i) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema ‘‘ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania Jeshi la aina yoyote.”
Laitani mwandishi angeangalia kifungu cha 151 cha katiba hiyo akaona neno “Serikali” lilivyotafsiriwa angeondoa shaka yoyote juu ya uwezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweza kuunda na kuweka jeshi. Neno serikali linatafsiriwa kama:
“Serikali maana yake ni pamoja na serikali ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Halmashauri ya Wilaya au Mji, na pia mtu yeyote anaetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali au Halmashauri.”
Tafsiri hii katika Katiba ya Muungano 1977 yenyewe inatoa fursa kwa serikali (ikiwemo SMZ) kama zilivyotafsiriwa na katiba hiyohiyo zilivyo na uwezo wa kuunda na kuweka jeshi.
Lissu amegusia vyeo vipya vya Zanzibar vya Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar vilivyoundwa na mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Anasema nayo yamekiuka katiba ya Muungano na hivyo ni ‘‘batili na hayana nguvu yoyote ya kisheria.” Ananukuu kifungu cha 64(3) cha Katiba ya Muungano 1977 kujenga hoja yake. Mbona amekinukuu nusu?
“Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka….”
Lakini kwa mshangao utagundua kuwa kifungu hicho kinaendelea kumalizia kama ifuatavyo (lakini mwandishi ameona hiyo sehemu ya mwisho ya kifungu hicho asiinukuu, kwa nini, haieleweki)
“… na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka.”
Hivi muundo mzima wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vyeo vya viongozi wa Serikali hiyo na watendaji wake ni jambo lililo chini ya mamlaka ya Bunge? Hamna popote katika katiba au sheria yoyote inayotoa mamlaka kwa Bunge juu ya kuunda vyeo au muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vyeo hivi vya makamo wawili wa Rais wa Zanzibar vimetokana na kundwa kwa Serikali yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa lakini kama vyeo hivi ni batili basi kwanza huo muundo wenyewe uliopelekea kuwepo kwa vyeo ungekuwa ni batili!
Muundo wa SMZ na vyeo katika Serikali tangu Aprili 1964 ni mambo yaliyo kwenye mamlaka ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na yanaongozwa na Katiba ya Zanzibar.
Lissu anaposema ilikuwa vema mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yakafuata misingi ya sheria anaonyesha kuwa sheria zimevunjwa. Hilo si kweli. Kwanza, yapasa atambuwe kuwa ni fikra potofu kuamini katiba ya Muungano ndio katiba mama na ile ya Zanzibar ni mtoto. Katiba zote hizi ni sawa kisheria. Katiba ya Zanzibar ina nguvu juu ya mambo yote ya Zanzibar (yasiyokuwa ya Muungano) wakati ya Muungano ina nguvu kwa mambo ya muungano na yale ya Tanganyika.
Hata kama baadhi ya taasisi, vyombo na vyeo vya Zanzibar vinatambuliwa katika katiba ya Muungano, hiyo haimaanishi kuwa katiba ya Muungano ndio inayosimamia mambo hayo. Juu ya yote haya, bado ninaamini mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ni muhimu kwani iliyopo haitoshelezi wakati.

Hapo kwenye red hapo, .....notice the difference sir...
 
...Lakini tujiulize hivi Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina uwezo wa kuunda majeshi?

Halafu ukishapata jibu naomba pia unijibu AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ZANZIBAR ni nani?
 
ni TANGANYIKA na ZANZIBAR sio TANZANIA NA ZANZIBAR, kwanini watu wanalikwepa hili neno TANGANYIKA? au Watanganyika,
Watanganyika
 
...Lakini tujiulize hivi Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina uwezo wa kuunda majeshi?

Halafu ukishapata jibu naomba pia unijibu AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ZANZIBAR ni nani?

Zanzibar haina jeshi kutokana tumetawaliwa kimabavu,tukiangalia katika history kivipi tumeungana na tanganyika,ni kwamba baada ya mapinduzi zanzibar nyerere alileta wanajeshi mia tatu,kuja kulinda urais wake karume,sasa nyerere alichofanya kumshawishi kwarume kuwa wazinganishe nchi au ataondowa wanajeshi wake zanzibar,hapo karime alihofia kuja wahafidhina wengine kuja kumpindua.

Pia karume hakusoma,nyerere kasoma,kwa hiyo alimpiku kwa kutumia mbinu,sasa mbinu alotumia,kuwa tumeungana kijeshi kuwa jeshi litakuwa la muungano,na mengine mengi katika katiba hiyo ambayo ilikuwa na mabo 11 ya muungano,lakini tukiangalia muungano huu ulikuwa ni wa miaka kumi tu,sasa siku zilivyokwenda kukawa na mtafaruku baina ya nyerere na karume,wakawa hawaelewani,baada ya hapo kulifnyika njama zaidi ili kumuuwa karume,na badala ya kufa ya karume hakupitiwa tena mkataba wa muungano,na karume alikufa kabla ya mika kumi kutimia,so tumejikuta kuwa muungano haukuwa sahili,pia zanzibar ikamezwa kwa kijeshi.

ndio ukaona kila baada ya uchaguzi tunalazimishwa na tunaekewa raisi kutoka ccm ambae watanganyika wanae muhitaji,,ili kumtumilia, mistake ilifanyika hapoo,hivi sasa hatuwezi kuunda jeshi hadi pale katiba itakapofanyiwa marekebisha baadhi ya mabo ya mamlaka ya zanzbar yarudishwe moja ni jeshi na mambo ya njee kimataifa,ili zanzibar iwe kama taifa huru lenye kujitengemea japokuwa kuna muungano.
 
strategy za wakristo Zanzibar
.ExternalClass .EC_hmmessage p { padding: 0px; }.ExternalClass body.EC_hmmessage { font-size: 10pt; font-family: Verdana; }
Waraka maalum kwa Wakristo Zanzibar

Wapendwa katika Bwana,


NDUGU Wakristo umefika wakati tumeonelea kuwa ipo haja ya kuwaelezeni
machache ili kuona maendeleo yetu na mafanikio tuliokwisha yapata hapa
Zanzibar, yanaendelezwa na hayarudi nyuma kwa namna yoyote. Hapana
shaka kuwa munaelewa kuwa idadi yetu hadi sasa ni ndogo sana na wengi
wetu tungali katika kiwango na hadhi ya wahamiaji na sio Wazanzibar
kama wanavyosema wenyewe.



MAFANIKIO YETU


KABLA kugusia yale ambayo tunahisi ndio lengo la waraka huu hapana
budi kuwatajieni mambo machache ambayo tumefanikiwa kuyapata hadi
sasa. Pamoja na jitihada zetu za muda mrefu bado tunapaswa tumsifu
Bwana kwa msaada wake mkubwa kwetu dhidi ya maadui zetu. Tunaamini
kuwa kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, Bwana atatupa ushindi na
mafanikio makuu zaidi ya haya na atawafumba macho maadui zetu wazidi
kulala ili mipango yetu yote ya kuibadilisha Zanzibar kidemografia
ifanikiwe katika kipindi kifupi kijacho. Mafanikio yetu yameenea
katika kila upande - katika uchumi, siasa, huduma za jamii, umiliki wa
ardhi, ujenzi, elimu na kadhalika ili kupata picha kamili ni vyema
tuorodheshe kwa ufupi mafanikio hayo:


Nafasi yetu kwa upande wa elimu imekuwa ya kuridhisha kupitia nafasi
za serikali. Hivi sasa ni rahisi na limekua jambo la kawaida katika
kila matangazo ya wito wa masomo kusikia majina ya Wakristo. Kati ya
vijana 7 hadi 10 ni lazima upate vijana wawili hadi watatu kutoka
katika makanisa yetu.


Sambamba na matangazo ya elimu, vijana wetu wamekuwa wanapata nafasi
nyingi za ajira katika serikali ya Zanzibar.


Hali ya kutoelewana kisiasa baina ya Wazanzibari imetoa mwanya kwetu kuingiza vijana wa
Kikristo wenye asili ya bara kwa wingi kwani wamekuwa wanaaminika
zaidi kuliko vijana wa Zanzibar.


Hali tulioieleza juu imetuwezesha kuwa na Wakristo wengi katika nafasi
za juu serikalini na katika chama tawala. Hali hii ni lazima
iendelezwe katika ngazi zote kwani ndiko kunako mambo mengi ya kila
siku.


Tumepata fursa ya kutumia Taasisi za serikali kwa uendeshaji wa ibada
zetu. Hali hii imefanya tuzidi kukubaliwa na Waislamu na kuvumiliwa na
inaweza kutupa nafsi ya kuwavuta katika NENO LA BWANA.


Kwa upande wa mashamba (vijijini) tumepata wasaa mzuri wa kununua
ardhi toka kwa Waislamu ambao hadi sasa bado hawajashtuka. Ardhi hizi
zimetuwezesha kujenga makanisa kadhaa ambayo hapo awali hayakuwepo.

Idadi ya skuli na vituo vyetu (ambavyo licha ya picha ya juu kuwa
haviendeshwi kwa misingi ya Kikristo lakini kiukweli ni vituo vya
kimisionari) vimeongezeka kwa hali ya kuridhisha. Skuli hizi ni
kuanzia kwa watoto wadogo hadi vituo kama hichi kilichopo mji mkongwe
(Stone Town Youth Centre) na zinafanya kazi vizuri katika kupandikiza
mila za Kikristo.


Sera zilizopo hivi sasa kwa upande wa uingiaji na utokaji Zanzibar
imetusaidia sana katika uingizaji wetu (Wakristo) kutoka Bara na hivyo
kusaidia kufuta ile imani ya kuwa Zanzibar ni kisiwa cha Waislamu eti
Wazanzibari kwa zaidi ya asilimia 99 ni Waislamu.


Ujaji wa Wakristo kwa wingi kutoka Bara umewezesha kuongezeka kwa
idadi ya mabaa na kilabu za pombe. Hivi sasa ni jambo la kawaida kuona
magari ya aina mbalimbali yanayomilikiwa na eti Waislamu yamebeba
kreti za bia na pombe kali.


Kujiingiza kwetu katika taasisi za dola katika ngazi za mitaa
kumetuwezesha kupata nafasi ya kutangaza Ukristo kwa njia ya mihadhara
na wakati huo huo kudhibiti mihadhara ya wazi ya Waislamu kwa kutumia
madai ya kashfa na kutatanisha maelewano mazuri baina ya watu wa dini
tofauti.

Tumefanikiwa kupata viwanja vingi katika maeneo ya mjini ambayo
yangali mapya. Maeneo haya ni kama Tomondo, Mombasa, Mwanakwerekwe na

kadhalika ambayo tayari tumeshajenga makanisa yetu ingawaje kwa sasa
hayajawa na waumini wengi wa kuyatumia na bado yanaonekana ni matupu.

Ndugu wapendwa katika Bwana,


Mafanikio hayo yasitufanye tukalewa na kusahau jukumu la kanisa la
kuona kuwa utawala wa Bwana unashuka Zanzibar haraka iwezekanavyo.
Kosa lolote utakalofanya hivi sasa litaweza kuturudisha hatua kadhaa
na huenda nafasi hii tuliyonayo hivi sasa tusiipate kwa karne mpya
ijayo.


Mambo ya kufanya yanayotukabili ili kuimarisha nafasi yetu ni kuona
yale tuliyokwisha yapata hayatutoki na kuyafanya dira kwa karne ijayo
ni haya yafuatayo:


Tusahau tofauti zetu dhidi ya adui


Ingawaje tupo madhehebu nyingi lakini tunawajibika kuelewa kuwa
Waislamu na Uislamu wao ni adui yetu namba moja ambaye hatutofaulu
kupambana nae mmoja mmoja. Uislamu hapa Zanzibar ni dini iliofungamana
na mila na utamaduni hivyo kila itakavyowezekana tusahau tofauti zetu
ndogo ndogo na hata kubwa kukabiliana nao, vingienvyo tutarudi kama
wakati wa Karume.


Tuhakikishe tunapata ardhi


Hii ni mbinu kongwe katika usambazaji wa Ukristo. Wazee wetu
walipoleta Ukristo Zanzibar na katika Afrika, jitihada waliyofanya ni
kupata ardhi kuwa kwa ajili ya ujenzi wa maeneo yetu, majengo ya
hospitali, shule, zahanati na vituo vya chekechea, makanisa na
kadhalika. Tunahitaji ardhi kubwa ili kuziweka huduma hizo mahala
pamoja kwa ajili ya kueneza injili ya Bwana na Muokozi wetu.


Tununue nyumba na viwanja kwa ujenzi wa Makanisa


Inaonekana Waislamu wenye siasa kali na baadhi ya watendaji kwenye
serikali wameanza kushtuka na ongezeko kubwa la makanisa katika kisiwa
cha Unguja. Kuna dalili kuwa tunaweza kupata ugumu katika kupata
viwanja kwa ajili ya makanisa. Njia tunayoweza kuitumia kwa muda huu
ni kununuwa viwanja vitupu au nyumba za Waislamu kwa bei kubwa
itakayowashawishi kuziuza na baadaye tukaweza kuvijenga au kugeuza
nyumba hizo kuwa makanisa.


Tujenge shule na hospitali kwa wingi


Hizi ni taasisi ambazo tunaweza kueneza neno la Bwana kwa Waislamu
walio wengi hapa Zanzibar. Kwa kutumia umaskini unaowakabili wengi ya
Wazanzibari na uchache wa huduma hizo tunaweza kujitangaza vizuri,
tujitahidi kutoa huduma nzuri kuweka vifaa vya kisasa kuweka bei
ndogo, kuweka upendo ili vituo vya Waislamu au hata vile vya serikali
visiweze kuvikaribia vyetu. Shule ni sehemu muhimu ya kupandikiza
mafundisho yetu zaidi kwa watoto wadogo (Nursery).


Tunadai muda zaidi katika vyombo vya habari (TV na Radio)


Kwa muda mrefu sasa Uislamu na Waislamu wamehodhi vyombo hivi vya
habari mbali na kuwa siku ya Ijumaa ambayo yote humilikiwa na vipindi
vya Kiislamu vyombo hivyo hutenga siku nyingine kadhaa kwa vipindi vya
Kiislamu na hata kuthubutu kutia adhana kila wakati wa sala hali hii
inaudhi na inatoa picha ya wazi ya serikali kupendelea Uislamu
ingawaje inadai kuwa haina dini. Wakati wa kusherehekea miaka 25 ya
TVZ tulizungumzia suala hili lakini halikupata mtu wa kulifanyia kazi.
Sasa tuhakikishe kuwa Ukristo unapata muda zaidi katika vyombo hivyo
au Uislamu nao upunguziwe nafasi.


Tuongeze mhadhara wa wazi


Wakati Waislamu wamezuiliwa kufanya mihadhara ya wazi, sisi tujitahidi
kuhakikisha kuwa mihadhara yetu inaongezeka kwa kiwango kikubwa. Kwa
kuwa Waislamu hawahudhurii mihadhara hiyo, lazima tuone Wakristo wa
mjini na mashamba wanahamasishwa na kupatiwa nyenzo ili kuhudhuria.
Vipaza sauti vitumike kuhakikisha kuwa neno la Bwana linafika kila
pahala. Mihadhara ifanyike karibu na nyumba, Misikiti na kwenye
viwanja vya wazi.


Tuendelee kutumia shule na sehemu za umma


Ili kuwafanya Waislamu watuzoee na kuondosha chuki yao kwetu ni lazima
kuendelea kutumia mashule na sehemu za umma zilizo wazi kwa mambo yetu
ya ibada kwa kipindi kirefu hali hii inaweza kuwafanya washindwe kuona
tofauti yetu na wao.


Tufanye suala la uhamiaji Zanzibar kuwa jepesi


Uzoefu unaonesha kuwa ni jambo gumu kuwabatiza Wazanzibari Waislamu.
Hali hii inafanya ongezeko la Wakristo kuwa dogo au halipo kabisa
ukitoa wale wanaozaliwa katika familia za Kikristo.


Njia pekee ya kuhakikisha ongezeko la makanisa na taasisi zetu ni
kuongezeka kwa Wakristo. Jambo hili litawezekana kwa kuingiza Wakristo
wengi kutoka Tanzania Bara au wapagani ambao tutaweza kuwabatiza kwa
kutumia udugu wetu wa kikabila au asili ya Bara. Kwa kuwatumia ndugu
zetu waliomo serikalini (SMZ au SMT) tuhakikishe kuwa suala la
uhamiaji linabakia wazi na rahisi na linaendelea kwa kila hali.


Tuzuie jaribio lolote la kadi za uraia au vitambulisho


Wakrsito tunapaswa kuelewa kuwa iwapo serikali ya Zanzibar itaamua
kufanya chochote ili, kuwa na vitambulisho au kadi za uraia kwa
Wazanzibari basi jambo hilo litaathiri sana mipango yetu ya muda mrefu
kwa Zanzibar. Jitihada zozote za kuiimarisha Zanzibar kama Zanzibar na
nje ya Utanzania ni lazima tuelewe kuwa Uislamu utapata nguvu na kuwa
tishio kwa hapa Zanzibar na hata Bara. Iwapo tutawajibika kuunga mkono
ni kadi za Uraia na vitambulisho vya Watanzania kwa ujumla na sio
Zanzibar peke yake.


Tujipenyeze na kushika nafasi muhimu


Lazima tuelewe kuwa chama chochote cha siasa kinalenga kukamata
serikali ili kiweze kutekeleza yale yanayoaminika kuwa mazuri kwa
chama hicho. Tunapozungumzia vyama vya siasa kwa Zanzibar tunahusisha
zaidi kwenye CCM na CUF. Watu wetu wamefaulu kuingia kwa wingi katika
chama tawala na katika jumuiya zake.


Tuunge mkono sera za utalii


Hadi sasa wengi wa watalii wanaoingia Zanaibar hutokea nchi za
Kikristo. Desturi za watalii hupingana na zile za Kizanzibari na hata
za Kiislamu. Watalii wanasaidia kuongezeka kwa mabaa na vivazi ambavyo
Waislamu wanataka visivaliwe hasa na wanawake.

Tujenge mabaa na kuongeza pombe


Waislamu wengi huchukia pombe na huweza kuhama iwapo duka la pombe au
baa ipo karibu nao. Waislamu hatari ni wale wanaosoma na kupata muda
wa kujishughulisha na dini yao.

Pombe ni kitu ambacho humtoa Muislamu katika Uislamu wa vitendo na
kumkaribisha na Ukristo.


Uwafuate Wakristo waliosilimu ili warudie Ukristo


Watu wa aina hii wanakuwa bado hawajatulia na mara nyingi huwemo
katika matatizo. Pana haja ya kuwalenga watu hawa ili kuwarudisha
kabla hawajatulia au kupata elimu nzuri. Matatizo yao ndipo mahala pa
kuanzia ili Bwana atawateremshie roho ya utulivu. Uzima wa Ukristo ni
kuwa na wafuasi wengi kadiri iwezekanavyo.


Tuwafuate wanawake kwa misaada


Jumuiya zisizo za kiserikali zinaungwa mkono duniani kote na hasa zile
za wanawake na watoto tujiweke pamoja ili tuweze kuwavutia kwa jina la
kuwasaidia.


Tuongeze vituo vya mafunzo ya Kikristo


Kituo cha vijana cha mji mkongwe (Stone Town Youth Center) kimekuwa
kikifanya kazi yake vizuri kwani hadi sasa lengo lake la ndani bali
halijaeleweka na vijana wanaohudhuria hapo kwa shughuli mbalimbali,
jitihada zifanyike ili kuwa na vituo vya aina hii katika maeneo
mengine. Lengo kuu liwe ni vijana na wanawake bila ya kuonesha dalili
za kidini.


Tuwaoe wanawake wao kwa kusilimu kimajina


Jitihada za makusudi zifanyike ili kila itakapowezekana kuwaoa
wanawake wa Kiislamu ili tuweze kuwabatiza baadae, njia nzuri iwapo
patakuwa na ugumu ni kusilimu kiuongo ili kuruhusiwa kuwaoa wanawake
wao.

Tuanzishe NGOs na sisi tuwe viongozi


Kwa kuwa hivi sasa wafadhili wengi wameonesha hamu ya kuzisaidia NGOs
moja kwa moja badala ya serikali ni lazima tujitahidi kuunda jumuiya
zetu ambazo zitawashirikisha Waislamu lakini uongozi wa juu ni lazima
uwe mikononi mwetu. Hii itatuwezesha kuona sera zetu na malengo
yanatelekezwa kwa kivuli hicho.


Tujenge ukaribu na viongozi ili kuwadhibiti Waislamu


Mambo yetu mengi yamekuwa yanakwenda vizuri katika maeneo mbalimbali
baada ya wenzetu kuwemo katika kamati za masheha, na matawi ya vyama,
na kamati za maendeleo za maeneo mbalimbali. Hali hii ni lazima
iongezeke ili udhibiti wa shughuli za Waislamu uwe mzuri zaidi na
wakati huo huo kuona kuwa mambo yetu yanakwenda yakiwa na baraka ya
vyombo vya dola na vyama vya siasa.


Tuwachonganishe Mashehe wenye msimamo mkali


Mashehe wenye misimamo mikali wamekuwa ni tatizo kwa Ukristo kwani
wana wafuasi wengi na wamekuwa wakisema wazi na kushutumu maendeleo
yetu. Mashehe hao ni lazima wachonganishwe na serikali ili hali
ikiruhusu wazuiliwe kuendesha shughuli zao. Wakati tukifanya hivyo
hatuna budi kuwaunga mkono Mashehe wote ambao wamekuwa wakitusaidia
kwa njia mbalimbali.


Tulenge kuifuta Tabligh


Pamoja na kuwa na Tabligh sio hatari moja kwa moja kwa Ukristo lakini
bado inastahili kupigwa vita kwa sababu ina aina pekee ya mihadhara ya
Waislamu inayoruhusiwa humu Zanzibar. Tabligh inaweza kuwazindua
baadhi ya Waislamu ambao ni vema kubaki bila ya kuzinduliwa.

Tudai turudishiwe taasisi zetu


Serikali ya Zanzibar bado inaonekana kuwa ngumu katika milki ya
makanisa, ardhi na taasisi zetu. Dalili za huko nyuma zilionekana
nzuri kwani tulifanikiwa kupata hospitali yetu Walezo na eneo la
Kiugani hata hivyo panakuwepo na ugumu wa kurudishwa shule zetu. Kwa
kuwatumia wenzetu waliomo serikalini na baraza la wawakilishi
tuzidishe harakati na madai ya taasisi zote zilizobaki.


Tulete waumini kutoka mashamba kuanza makanisa

Hivyo sasa pameibuka wasi wasi kuhusiana na wingi wa makanisa ambayo
hayajapata waumini wa kuyajaza. Ili kuficha dosari hii na hoja kadhaa
utaratibu uliopo hivi sasa chini ya baadhi ya makanisa ni lazima
uungwe mkono. Wakristo wahamiaji wengi hufikia mashamba hivyo pawekwe
na utaratibu wa kuwaleta mjini ili kujaza makanisa.

Neno la mwisho


Wapendwa katika Bwana.


Miongozi hii ni mikubwa na inaweza kuwatisha baadhi ya waumini wa
Kikristo hasa wale ambao bado hawajampokea Roho Mtakatifu vizuri. Hata
hivyo, kwa uwezo wa Bwana Mungu wetu ni mpango rahisi. Suala la muhimu
ni haya kufahamika na kila Mkristo apendae kumtumikia Bwana. Pia
hatuna budi kuishukuru awamu ya nne ya serikali ya Mapinduzi ambao
imefungua milango kwa Ukristo na kushuhudia ongezeko la makanisa.



Bwana awe nasi!
 
Hakuna mkristo wa kweli atakayeandika utumbo kama huu. Hizi ni chuki za kidini tu na huwezi kudanganya watu wewe si mkristo ni mdini unaetaka kupandikiza chuki. Ni lazima uelewe Zanzibar ndiyo wanatakiwa nchi lakini hakuna maendeleo kwasababu hizi za ujinga kama huu wa kufikiria shule ikijengwa na wa kristo si nzuri, hospital ikijegwa na wakisto ni udini. Agha Khan mbona kila mtu anaenda kama kuna shule na inatoa elimu soma au bakia mjinga. Kiwango cha elimu ni kidogo sana zanzibar kwasababu ya maneno na tabia ya kusingizia Tanganyika kila siku. Wanzanzibar mnatakiwa kuacha lawama na kujitahidi kama watu wengine.
 
Zanzibar haina jeshi kutokana tumetawaliwa kimabavu,tukiangalia katika history kivipi tumeungana na tanganyika,ni kwamba baada ya mapinduzi zanzibar nyerere alileta wanajeshi mia tatu,kuja kulinda urais wake karume,sasa nyerere alichofanya kumshawishi kwarume kuwa wazinganishe nchi au ataondowa wanajeshi wake zanzibar,hapo karime alihofia kuja wahafidhina wengine kuja kumpindua.

Pia karume hakusoma,nyerere kasoma,kwa hiyo alimpiku kwa kutumia mbinu,sasa mbinu alotumia,kuwa tumeungana kijeshi kuwa jeshi litakuwa la muungano,na mengine mengi katika katiba hiyo ambayo ilikuwa na mabo 11 ya muungano,lakini tukiangalia muungano huu ulikuwa ni wa miaka kumi tu,sasa siku zilivyokwenda kukawa na mtafaruku baina ya nyerere na karume,wakawa hawaelewani,baada ya hapo kulifnyika njama zaidi ili kumuuwa karume,na badala ya kufa ya karume hakupitiwa tena mkataba wa muungano,na karume alikufa kabla ya mika kumi kutimia,so tumejikuta kuwa muungano haukuwa sahili,pia zanzibar ikamezwa kwa kijeshi.

ndio ukaona kila baada ya uchaguzi tunalazimishwa na tunaekewa raisi kutoka ccm ambae watanganyika wanae muhitaji,,ili kumtumilia, mistake ilifanyika hapoo,hivi sasa hatuwezi kuunda jeshi hadi pale katiba itakapofanyiwa marekebisha baadhi ya mabo ya mamlaka ya zanzbar yarudishwe moja ni jeshi na mambo ya njee kimataifa,ili zanzibar iwe kama taifa huru lenye kujitengemea japokuwa kuna muungano.

Ukiingiya ndowa ya kulazimishwa na hatimaye ukazaa watoto kibao, watu wataconclude kuwa ulinogewa na hiyo ndowa! So hekma apo inakutaka ulinde ndowa yako ili mlee wajukuu! Ah nilikuwa napita tu!
 
:wink2:
Waraka hata haujulikani umeandikwa na nani utamfanya nani aamini?

Acheni upuuzi wa kujitungia mavitu yasiyokuwa n amaana. Kwa nini badala ya kutumia muda kufanya kitu chenye maana mnawaza kuandika uppuzi wa ku-justify ujinga wenu (baadhi najua sio waislam wote)

Hakuna kiongozi makini chini ya mwamvuli wa Ukristo atakaeandika upupu kama huu, labda awe amerukwa na akili na ameweka pembeni maadili na misingi ya Ukristo

By the way, CHADEMA hapa wanaingiaje? Ndio wanaojenga mashule, mahospitali ya makanisa au?

This is simply abyss of despair from you people na mnakosea kutafuta pa kupumulia na namna ya kupumua...
 
:wink2:
Waraka hata haujulikani umeandikwa na nani utamfanya nani aamini?

Acheni upuuzi wa kujitungia mavitu yasiyokuwa n amaana. Kwa nini badala ya kutumia muda kufanya kitu chenye maana mnawaza kuandika uppuzi wa ku-justify ujinga wenu (baadhi najua sio waislam wote)

Hakuna kiongozi makini chini ya mwamvuli wa Ukristo atakaeandika upupu kama huu, labda awe amerukwa na akili na ameweka pembeni maadili na misingi ya Ukristo

By the way, CHADEMA hapa wanaingiaje? Ndio wanaojenga mashule, mahospitali ya makanisa au?

This is simply abyss of despair from you people na mnakosea kutafuta pa kupumulia na namna ya kupumua...
Pengine itasaidi zaidi ukifafanua hiyo bold !
 
Hizi Chuki Nyingine bwana!

Kila Dini[Islamu na Ukiristo] ina jukumu la kuvutia Waumini, kama Kanisa lina mipango ya kuifanya Zanzibar iwe ni ya Kikristo, Ni jukumu la Waislamu nao kufundisha dini yao ili ikubalike zaidi na pia kuwafanya hao Wakiristo wawe waislamu!.
 
Bila shaka mtoa hoja ni Mzanzibari na Lisu tunajua ni Mtanganyika. Kila mtu hapa ana hofu juu ya kupoteza utaifa wake ambao umeletwa na muungano ulioizaa Tanzania.

Ni kweli Zanzibar ilikuwa na katiba yake kabla ya Muungano, na Tanganyika pia ilikuwa na yake.

Baada ya Muungano katiba zote hizi zisingetakiwa kuwepo au kama vipi ziwepo zote. Tatizo linaanza pale panapokuwa na katiba ya Zanzibar wakti ya Tanganyika haipo. Kuna rais wa Zanzibar lakini hakuna wa Tanganyika.

Wengi wetu tulikuwa tunajua Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na zamani kulikuwa na mikoa miwili ya Tanzania kwa upande wa Zanzibar kama sijakosea.

Tena tunaona mabadiliko ya katiba baada ya waziri mkuu kutamka kuwa Zanzibar si nchi ila sehemu ya muungano.

Mheshimiwa Lisu ana haki ya kusema kuwa muungano unaelekea kudhoofika, kwa kuangalia mambo haya ya kubadilishwa kwa katiba ya Zanzibar baadaya ya waziri mkuu kusema zanzibar ni sehemu ya nchi ya Tanzania.

Kwa kumsoma Lisu unaona Zanzibar ni nchi inayojitegemea, yenye mipaka yake, rais, mahakama na bunge.

Kwa muundo wa zamani Zanzibar wala Tanganyika zilikuwa sio nchi, bali sehemu za Muungano.
Ila sasa kama Zanzibar ni nchi, Lisu anatakiwa kutafuta nchi yake na katiba ya nchi yake iwepo. Usiwepo ugomvi kati yetu. Kama tunataka muungano wa Tanzania ulioimara, kila mtu lazima aukane uzanzibari au utanganyika. Sio Zanzibar nchi, huku Tanganyika haipo. Hapo tunadanganyana
Nashangaa hutaki uona ukweli. Wamezoea hawa kuandika vitu nusu nusu wakitegemea majina yao yatawalinda!
 
Ukiingiya ndowa ya kulazimishwa na hatimaye ukazaa watoto kibao, watu wataconclude kuwa ulinogewa na hiyo ndowa! So hekma apo inakutaka ulinde ndowa yako ili mlee wajukuu! Ah nilikuwa napita tu!

Ni wakati wa uhuru wa wanawake pengine anaetaka huruma hapa ni mwanmke1 Usijidanganye kuwa lazima hiyo ndowa yako iwe wewe ni mwanamme1
 
Back
Top Bottom