Hasira za Naibu spika kwa upinzani kuligharimu taifa kiasi kikubwa

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Nashindwa kuelewa ni kwanini baadhi ya mambo hasa yanayolihusu taifa tunatanguliza ushabiki na hisia zisizokua na msingi wowote kwa taifa.

Nimejaribu kufuatilia kisa hasa cha Naibu spika pamoja na kamati yake ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge kiilichopelekea kuwatimua wabunge wa upinzani sio kutofuata kanuni na taratibu za bunge bali ni hasira, hisia za kiitikadi, hofu na kukosa busara za kiongozi. Kwa mtu mweledi kiuongozi huwezi kutatua matatizo yako kwa kuwaadhibu wakosaji wako wote, hiyo haipo duniani kote! busara hua inatakiwa kutangulia wakati wa maamuzi siku zote.

Nina uhakika kwa kiongozi makini mwenye busara asingeweza kuwatimua wabunge kama akina Lissu, Zitto na Mdee, alitakiwa kwanza kuwachukua kama wapinzani angetafuta namna nzuri ya kuishi nao vizuri, hawa ni wasomi wazuri kuwatumia kwa maslahi ya kitaifa, michango yao ingeweza kusaidia kung'amua mambo magumu sana kama ambavyo tuliona awamu ya tano.
Matokeo yake hasira na hisia za kisiasa zisizokua na maana ndizi zilizotumika.

Kwa hakika pamoja Naibu spika kama msomi wa sheria pamoja na uwepo wa mwanasheria mkuu bungeni ni hakuna anayemfikia Mh Tundu Lissu, Mwanasheria alikuwepo wakati wa awamu ya tano meishoni, Naibu spika alikuwepo bunge la katiba pia wote hawa hawakua na uwezo wa kung'amua mambo kumpita Tundu LISSU na hata Mh Zitto Kabwe.

Nina imani kabisa mambo kama haya ya miamala ya pesa kwenye taasisi za kifedha na mitandao ya simu na lile suala la kukatwa viinua migongo kwa viongozi wakuu wa kisiasa wangekuwepo wabunge hawa wa upinzani wangeweza kuishauri vizuri serikali, angalia sasa kuhusu suala la miamala ya fedha linataka kufanana na suala la sukari.

Ni ukweli usiopingika kutokuwepo kwa wapinzani bungeni kutaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana, tutegemee mengi kujitokeza baadaye zaidi kutokana na maamuzi yaliyofanywa na wabunge wa CCM peke yao.

Pasina shaka yeyote uwezo wa Tundu Lissu na Mh Zitto ni mkubwa sana kuliko wabunge wengi wa CCM. Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo. Juzi juzi tu serikali aliwasilisha bungeni hoja ya walichokiita mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano lakini kwa macho ya Lissu na Zitto walikataa kabisa bungeni kwa kudai kua ule haukua mpango wa maemdeleo! Lakini wakati huo Naibu spika alikuwepo, Mwanasheria mkuu wa serikali alikuwepo lakini pia waziri wa katiba na sheria nae alikuwepo kwanini hawakuiona kasoro hiyo? Asingekuwepo Zitto na Lissu ni mpango upi ambao ungejadiliwa?

Ikumbukwe kwa kiasi kikubwa kwenye bunge la jamhuri ya Muungano awamu ya tano Spika wa bunge la wakati huo Mh Anne Makinda aliwatumia sana Lissu, Mdee, Zitto na Change kwa masuala mbalimbali yaliyokua na tija kwa taifa letu! Naibu spika Dkt Tulia ameamua kuachana na busara za mama Makinda, yeye ameona kila anayeomba mwongozo ni kumuadhibu tu kwa kutohudhuria vikao hadi mpaka wapinzani wote waishe bungeni.

Nina uhakika kukosekana kwa upinzani wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya serikali kutakua na madudu mengi Sana, tutegemee mkanganyiko wa kauli na sheria mbali mbalimbali serikalini pindi utekelezaji utakapoanza.
 
Ni ngumu sana kujenga uchumi imara kwa kuwatimua wapinzani bungeni.

Nyerere hakuwa mpuuzi kuikubali ile 20% ya maoni ya wananchi kuruhusu vyama vingine nchini.

Wabunge wengi wa ccm wapo bungeni kwa ushabiki tu, hawana fikra pana za maendeleo.
 
hata kama ni kweli hayo uliyo yabandika hapo!! hawana haki ya kuvunja kanuni, taratibu na sheria walizo weka wao wenyewe!!!

shida kuu nchii mnapenda jadili individuals!! nakuamini hawakosei ni binadam na wanakosea!!! sheria ikate kotekote!!
 
Nafikiri ukisoma vizuri mada ukakutana neno "Upinzani" na"Busara" ndipo utakapo elewa nini kinajadiliwa humu.
 
Ni ngumu sana kujenga uchumi imara kwa kuwatimua wapinzani bungeni.
Nyerere hakuwa mpuuzi kuikubali ile 20% ya maoni ya wananchi kuruhusu vyama vingine nchini.
Wabunge wengi wa ccm wapo bungeni kwa ushabiki tu, hawana fikra pana za maendeleo.
Hakuna anayelielewa hilo na kama linaeleweka basi limepuuzwa!
 
"Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo." Mkuu nimekutana na hii kauli yako naenda kulala kwanza kwa sababu nimepata kizunguzungu nikirudi nakuja kuimalizia thread yako.Nikifa na hichi kizunguzungu atakuja kumalizia kuisoma mwanangu.
 
Ni ngumu sana kujenga uchumi imara kwa kuwatimua wapinzani bungeni.
Nyerere hakuwa mpuuzi kuikubali ile 20% ya maoni ya wananchi kuruhusu vyama vingine nchini.
Wabunge wengi wa ccm wapo bungeni kwa ushabiki tu, hawana fikra pana za maendeleo.
Huwezi kuwa na wabunge wanaoenda bungeni kitukana wabunge wenzao halafu unataka wachekewe hilo halipo.
 
"Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo." Mkuu nimekutana na hii kauli yako naenda kulala kwanza kwa sababu nimepata kizunguzungu nikirudi nakuja kuimalizia thread yako.Nikifa na hichi kizunguzungu atakuja kumalizia kuisoma mwanangu.
Sio tatizo lako, inawezekana ukawa hulijuli hili na inawezekana ndio mara yako ya kwanza kilisikia hili.
 
busara kuvunja kanuni na taratibu?? upinzani kuna mahala wanakosea sana na ni kutafuta kiki kipind hiki!! busara gani unayeizungumzia wakati wao hawana??
Kwanzia lini kupmba muongozo ni kuvunja kanuni aua ndo siasa uchwara mahaba yakizidi nayo shida
 
Nashindwa kuelewa ni kwanini baadhi ya mambo hasa yanayolihusu taifa tunatanguliza ushabiki na hisia zisizokua na msingi wowote kwa taifa.

Nimejaribu kufuatilia kisa hasa cha Naibu spika pamoja na kamati yake ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge kiilichopelekea kuwatimua wabunge wa upinzani sio kutofuata kanuni na taratibu za bunge bali ni hasira, hisia za kiitikadi, hofu na kukosa busara za kiongozi. Kwa mtu mweledi kiuongozi huwezi kutatua matatizo yako kwa kuwaadhibu wakosaji wako wote, hiyo haipo duniani kote! busara hua inatakiwa kutangulia wakati wa maamuzi siku zote.

Nina uhakika kwa kiongozi makini mwenye busara asingeweza kuwatimua wabunge kama akina Lissu, Zitto na Mdee, alitakiwa kwanza kuwachukua kama wapinzani angetafuta namna nzuri ya kuishi nao vizuri, hawa ni wasomi wazuri kuwatumia kwa maslahi ya kitaifa, michango yao ingeweza kusaidia kung'amua mambo magumu sana kama ambavyo tuliona awamu ya tano.
Matokeo yake hasira na hisia za kisiasa zisizokua na maana ndizi zilizotumika.

Kwa hakika pamoja Naibu spika kama msomi wa sheria pamoja na uwepo wa mwanasheria mkuu bungeni ni hakuna anayemfikia Mh Tundu Lissu, Mwanasheria alikuwepo wakati wa awamu ya tano meishoni, Naibu spika alikuwepo bunge la katiba pia wote hawa hawakua na uwezo wa kung'amua mambo kumpita Tundu LISSU na hata Mh Zitto Kabwe.

Nina imani kabisa mambo kama haya ya miamala ya pesa kwenye taasisi za kifedha na mitandao ya simu na lile suala la kukatwa viinua migongo kwa viongozi wakuu wa kisiasa wangekuwepo wabunge hawa wa upinzani wangeweza kuishauri vizuri serikali, angalia sasa kuhusu suala la miamala ya fedha linataka kufanana na suala la sukari.

Ni ukweli usiopingika kutokuwepo kwa wapinzani bungeni kutaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana, tutegemee mengi kujitokeza baadaye zaidi kutokana na maamuzi yaliyofanywa na wabunge wa CCM peke yao.

Pasina shaka yeyote uwezo wa Tundu Lissu na Mh Zitto ni mkubwa sana kuliko wabunge wengi wa CCM. Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo. Juzi juzi tu serikali aliwasilisha bungeni hoja ya walichokiita mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano lakini kwa macho ya Lissu na Zitto walikataa kabisa bungeni kwa kudai kua ule haukua mpango wa maemdeleo! Lakini wakati huo Naibu spika alikuwepo, Mwanasheria mkuu wa serikali alikuwepo lakini pia waziri wa katiba na sheria nae alikuwepo kwanini hawakuiona kasoro hiyo? Asingekuwepo Zitto na Lissu ni mpango upi ambao ungejadiliwa?

Ikumbukwe kwa kiasi kikubwa kwenye bunge la jamhuri ya Muungano awamu ya tano Spika wa bunge la wakati huo Mh Anne Makinda aliwatumia sana Lissu, Mdee, Zitto na Change kwa masuala mbalimbali yaliyokua na tija kwa taifa letu! Naibu spika Dkt Tulia ameamua kuachana na busara za mama Makinda, yeye ameona kila anayeomba mwongozo ni kumuadhibu tu kwa kutohudhuria vikao hadi mpaka wapinzani wote waishe bungeni.

Nina uhakika kukosekana kwa upinzani wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya serikali kutakua na madudu mengi Sana, tutegemee mkanganyiko wa kauli na sheria mbali mbalimbali serikalini pindi utekelezaji utakapoanza.

Naona umeeleza kishabiki bila mantiki zenye hoja za maana. ifike wakati sasa ushabiki tuweke pembeni na tuelezane ukweli kama wapinzani. usije kutudanganya danganya hapakama watoto wadogo. tumeshadanganywa sana sasa hivi sio wakati wake. nikuulize kitu. hivi Naibu spika ndie

1)Mwenye maamuzi ya kuadhibu wabunge?

2) Ni kwa nini wabunge wa upinzani walitoka nje karibu kipindi chote

3) Je wabunge hawa walishindwa kujenga hoja kwa kutumia kanuni aalizozitunga wao wenyewe bungeni?

4) Nini hasa faida sasa ya kipindi chote kwa wabunge hawa kukaa nje ambayo mwananchi wa kawaida ataipata.

5) Wabunge hawa wataenda kusimamia bajeti gani sasa mwaka huu wa fedha kama katika kuipitisha hawakuwepo. wataijuaje kwani hawakushiriki. wataisimamiaje, wataihoji vipi ikiwa itatumika ndivyo sivyo. na wataikosoaje utekelezaji wake.

Nashauri katika mwaka huu mpya wa fedha, wakae kimya kwa sababu mipango ya utekelezaji hawakuwepo bungeni. hawataweza isimamia. wasubiri mwaka ujao wa fedha 2017/18. mwaka huu imekula kwao. ni ujinga tu
 
Tatizo lako ni mihemko! Kwenye nchi ya vyama vingi huwezi kuongoza hivyo.
The Private Bar:

The Private Bar is composed of private legal practitioners known as advocates. The Advocates Ordinance requires the Registrar of the High Court to keep a Roll of Advocates.

Any person who has the qualifications prescribed by the ordinance is entitled to be registered.

These qualifications are: either a law degree of the University of Dar es Salaam (formerly the University of East Africa) or such other University or legal training institution as recognised by the Council for Legal Education; or the applicant must be a legal practitioner with a right of audience before any court of unlimited civil and criminal jurisdiction in any Commonwealth country or any other country designated by the Minister for Legal Affairs; or a Solicitor of the Supreme Court of England, Northern Ireland or the Republic of Ireland; a Writer to the Signet; a Solicitor of the Supreme Court of Scotland and holders of other legal offices in the United Kingdom.

In addition, the applicant must satisfy the Chief Justice that he has adequate knowledge of the language of the court which is English and must also produce testimonials of character. A person wanting to be registered as an advocate in Tanzania must petition the Chief Justice.
 
Unaelewa maana ya busara lakini?
busara lazima i balance pande zote mbili. acha upuuzi. kwa hiyo unataka waendelee kuchekewa tu kwa kufanya upuuzi kisa eti busara itumike. nchi gani inayakubali haya. tubadilike wajameni. tujifunze kujenge hoja zenye faida kwa taifa na sio kutafuta kiki za kisiasa. wenzako wanapalilia shamba lao. wanajitengenezea uhalali wa kuendelea kula vizuri wao na familia zao. wewe mishipa ya shingo inakutoka bila kujijua unatumika kwa faida yao.
 
Ndugu kumbukeni niliwahi kusema hapo awali kwamba kupitishwa kwa bajeti kuu ya serikali bila kuwepo wabunge wa upinzani italeta shida sana kiutendaji kwa sababu wabunge waliobaki ndani hawakuwa na hoja za msingi kuikosoa serikali nakuishauri ipasavyo zaidi ya kuongea kishabiki bila uchambuzi makini wa hoja....Mfano mzuri jana makampuni ya simu na taasisi za fedha zimetoa maelekezo kwa makato yatakayolipwa na mlaji yaani 18% VAT kwa gharama za miamala ya fedha,,,.LAKINI cha ajabu serikali leo imekuja na kauli kinzani yakusema ni marufuku kutoza gharama za miamala ya fedha...sasa nani atakaye fidia hasara hizo kama sio mlaji??????????????????? jambo hili litakuja kufanana sana na kupiga marufuku uagizaji wa sukari nje ya nchi lakini mwisho wa siku upungufu mkubwa wa bidhaa hiyo umeonekana nchini kitu ambacho kimepelekea bei kuwa juu hadi leo!! nini serikali inafanya????????? kuitwa mpinzani sio kwamba hana haki yakutoa ushauri mzuri kwa manufaa ya taifa,,,, kasumba ya kufuata maamuzi ya kisiasa ndo yanaligharimu taifa kwa kulivuruga taifa badal ya kuliongoza kwa njia nyoofu!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom