Hasira za Naibu spika kwa upinzani kuligharimu taifa kiasi kikubwa

huwezi linganisha hayo mawili. kila moja lina sensitivity yake katika taifa. mwingozo wa UDOM ulikuwa hauna maana pale kwa sababu hatua zilishaanza kuchukuliwa na serikali. ingekuwa ni kupiteza fedha za walipa kodi bure. je nikuulize hatua iliyochukuliwa na serikali kwa sasa ina mantiki au haina. jibu hili nikuone uelewa wako kama umesoma vya kutosha. na ukijibu vizuri utatambua sasa je mwongozo ulikuwa na maana ama la.ifike mahala tutenganishe siasa na masuala nyeti ya utaifa.tusiende kibubu bubu tu wajameni.
mwingozo ndo nini nyie ndo mnataka sanamu la damond
 
Tutarajie utumbo mwingi kwenye hii bajeti.. Si wanataka kuendesha bunge kutokea magogoni,sasa ngoja tuone vioja.
 
Mleta uzi unajichanganya mno!!Ulikuwa una mawazo mazuri sana ila jinsi ulivyoyawasilisha ndio imeharibu mawazo yako yote,mara raisi anachagua mawakili wa mahakama kuu, mara majina ya wahusika unayakosea mfano Change badala ya Chenge, kiufupi hukujiandaa kuandika hii thread.Ulikuwa una wazo zuri sana ila jinsi ulivyoliwasilisha limeharibu kila kitu. First impression last longer.
 
Mimi nawapongeza wabunge wa CCM kwa kupigania nchi tupate masanamu ya Diamond na Magufuli akipiga push up, na ninampongeza yule aliyelia kwa bunge kuonyeshwa live kwani ameonyesha ukomavu wa hali ya juu kwa taifa lake, vilevile naomba serikali ikubali ombi la mbunge kessy kuwa hata wanaofuga kuku na waendesha baiskeli walipe kodi kwani hamna kitu cha bure hapa serikali inakosa mapato
Umemsahau na yule aliye iomba serikali iruhusu mirungi
 
Tutarajie utumbo mwingi kwenye hii bajeti.. Si wanataka kuendesha bunge kutokea magogoni,sasa ngoja tuone vioja.
kama unalijua hilo basi wasingekimbia bunge. wangekomaa mpaka mwisho. kukimbia kwao kunamaanisha wameshindwa na hawana hoja mbadala. ukitaka kulijua hilo angalia baada ya bajeti ya serikali, ukafuata bajeti ya kambi ya upinzani kama bajeti mbadala. itafute kama utaipata. na kama ukiipata iangalie kama kweli inaweza kidhi matakwa na uendeshaji wa nchi hii. yaani ndio maana tuliitwa malofa na wapumbaf.
 
Sikilizieni budget iliyopitishwa na wabunge wa maccm wazee wa ndiyooooo!
 
naona umeeleza kishabiki bila mantiki zenye hoja za maana. ifike wakati sasa ushabiki tuweke pembeni na tuelezane ukweli kama wapinzani. usije kutudanganya danganya hapakama watoto wadogo. tumeshadanganywa sana sasa hivi sio wakati wake. nikuulize kitu. hivi Naibu spika ndie 1)mwenye maamuzi ya kuadhibu wabunge?
2) ni kwa nini wabunge wa upinzani walitoka nje karibu kipindi chote
3) je wabunge hawa walishindwa kujenga hoja kwa kutumia kanuni aalizozitunga wao wenyewe bungeni?
4) nini hasa faida sasa ya kipindi chote kwa wabunge hawa kukaa nje ambayo mwananchi wa kawaida ataipata.
5) wabunge hawa wataenda kusimamia bajeti gani sasa mwaka huu wa fedha kama katika kuipitisha hawakuwepo. wataijuaje kwani hawakushiriki. wataisimamiaje, wataihoji vipi ikiwa itatumika ndivyo sivyo. na wataikosoaje utekelezaji wake.
nashauri katika mwaka huu mpya wa fedha, wakae kimya kwa sababu mipango ya utekelezaji hawakuwepo bungeni. hawataweza isimamia. wasubiri mwaka ujao wa fedha 2017/18. mwaka huu imekula kwao. ni ujinga tu
Hivi ni nini haswa kilichopelekea hawa jamaa kutoka nje. Kiini cha tatizo ni nini? Tuanzie hapo itatusaidia
 
Serikali ya kukurupuka. Ukawa wajipange 2020 nchi yao. Yoyote atayeteuliwa ntampa kwa Ukawa.
unazungumzia ukawa hii yenye watuhumiwa wa ufisadi au ukawa asilia. usituchanganye. !kwanza Lowasa alishatamka wakati wa kampeni kuwa nchi tukiikosa kipindi hiki basi tena. hatutaweza ipata tena kamwe. kwa hiyo kamanda usijipe moyo usiokuwepo. kama kiongozi mkuu alisema hivyo wewe nani na kubadilisha fikra hizo sahihi za kiongozi mkuu
 
Huwezi kuwa na wabunge wanaoenda bungeni kitukana wabunge wenzao halafu unataka wachekewe hilo halipo.
Je wanatukana ni wapinzani tu? Huwezi kufanya maamuzi ilihali umefungwa nira ya chama.
Ndio maana hata Wakenya wanatukebehi kwa kusema, Naibu Spika kuteuliwa na Raisi ni kana kwamba Bunge linaongozwa kwa kivuli cha Raisi
 
Tunataka demokrasia ya kuwaruhusu wabunge kutukana bungeni bila kuchukuliwa hatua.
Tunataka demokrasia ya kuruhusu kanuni za bunge zivunjwe bila kuchukuliwa hatua.
Tunachokitetea ni domoghasia sio demokrasia.
 
Mleta uzi unajichanganya mno!!Ulikuwa una mawazo mazuri sana ila jinsi ulivyoyawasilisha ndio imeharibu mawazo yako yote,mara raisi anachagua mawakili wa mahakama kuu, mara majina ya wahusika unayakosea mfano Change badala ya Chenge, kiufupi hukujiandaa kuandika hii thread.Ulikuwa una wazo zuri sana ila jinsi ulivyoliwasilisha limeharibu kila kitu. First impression last longer.
Mkuu ni bahati mbaya kidogo hakufanya kuhariri, lakini ujumbe wake umeeleweka vizuri
 
Tunataka demokrasia ya kuwaruhusu wabunge kutukana bungeni bila kuchukuliwa hatua.
Tunataka demokrasia ya kuruhusu kanuni za bunge zivunjwe bila kuchukuliwa hatua.
Tunachokitetea ni domoghasia sio demokrasia.
Kanuni zinaanza kuvunjwa na CCM then zigo wanabebeshwa upinzani,.

Ni nani atakuballi huo upuuzi?
 
Nashindwa kuelewa ni kwanini baadhi ya mambo hasa yanayolihusu taifa tunatanguliza ushabiki na hisia zisizokua na msingi wowote kwa taifa.


Nimejaribu kufuatilia kisa hasa cha Naibu spika pamoja na kamati yake ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge kiilichopelekea kuwatimua wabunge wa upinzani sio kutofuata kanuni na taratibu za bunge bali ni hasira, hisia za kiitikadi, hofu na kukosa busara za kiongozi. Kwa mtu mweledi kiuongozi huwezi kutatua matatizo yako kwa kuwaadhibu wakosaji wako wote, hiyo haipo duniani kote! busara hua inatakiwa kutangulia wakati wa maamuzi siku zote.

Nina uhakika kwa kiongozi makini mwenye busara asingeweza kuwatimua wabunge kama akina Lissu, Zitto na Mdee, alitakiwa kwanza kuwachukua kama wapinzani angetafuta namna nzuri ya kuishi nao vizuri, hawa ni wasomi wazuri kuwatumia kwa maslahi ya kitaifa, michango yao ingeweza kusaidia kung'amua mambo magumu sana kama ambavyo tuliona awamu ya tano.
Matokeo yake hasira na hisia za kisiasa zisizokua na maana ndizi zilizotumika.

Kwa hakika pamoja Naibu spika kama msomi wa sheria pamoja na uwepo wa mwanasheria mkuu bungeni ni hakuna anayemfikia Mh Tundu Lissu, Mwanasheria alikuwepo wakati wa awamu ya tano meishoni, Naibu spika alikuwepo bunge la katiba pia wote hawa hawakua na uwezo wa kung'amua mambo kumpita Tundu LISSU na hata Mh Zitto Kabwe.


Nina imani kabisa mambo kama haya ya miamala ya pesa kwenye taasisi za kifedha na mitandao ya simu na lile suala la kukatwa viinua migongo kwa viongozi wakuu wa kisiasa wangekuwepo wabunge hawa wa upinzani wangeweza kuishauri vizuri serikali, angalia sasa kuhusu suala la miamala ya fedha linataka kufanana na suala la sukari.


Ni ukweli usiopingika kutokuwepo kwa wapinzani bungeni kutaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana, tutegemee mengi kujitokeza baadaye zaidi kutokana na maamuzi yaliyofanywa na wabunge wa CCM peke yao.


Pasina shaka yeyote uwezo wa Tundu Lissu na Mh Zitto ni mkubwa sana kuliko wabunge wengi wa CCM. Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo. Juzi juzi tu serikali aliwasilisha bungeni hoja ya walichokiita mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano lakini kwa macho ya Lissu na Zitto walikataa kabisa bungeni kwa kudai kua ule haukua mpango wa maemdeleo! Lakini wakati huo Naibu spika alikuwepo, Mwanasheria mkuu wa serikali alikuwepo lakini pia waziri wa katiba na sheria nae alikuwepo kwanini hawakuiona kasoro hiyo? Asingekuwepo Zitto na Lissu ni mpango upi ambao ungejadiliwa?


Ikumbukwe kwa kiasi kikubwa kwenye bunge la jamhuri ya Muungano awamu ya tano Spika wa bunge la wakati huo Mh Anne Makinda aliwatumia sana Lissu, Mdee, Zitto na Change kwa masuala mbalimbali yaliyokua na tija kwa taifa letu! Naibu spika Dkt Tulia ameamua kuachana na busara za mama Makinda, yeye ameona kila anayeomba mwongozo ni kumuadhibu tu kwa kutohudhuria vikao hadi mpaka wapinzani wote waishe bungeni.

Nina uhakika kukosekana kwa upinzani wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya serikali kutakua na madudu mengi Sana, tutegemee mkanganyiko wa kauli na sheria mbali mbalimbali serikalini pindi utekelezaji utakapoanza.

Wakuu
kabla ya kumhukumu Dr.Tulia nadhani tutafute uzoefu wake ktk mambo ya siasa, pia tuangalie amefikafikaje hapo alipo je amewahi kukutana au kuongoza taasisi nyeti kama hizo.
Nimesoma kuwa ameendesha video kwa siku 22 mfululizo je wenzie kwa nini huwa wanaa achia kuna Zungu n.k yeye hakufanya hivyo. Ukitafakari sana unaweza pata picha ni kiongozi wa jinsi gani na kwa nini yuko hapo.
 
Huwezi kuwa na wabunge wanaoenda bungeni kitukana wabunge wenzao halafu unataka wachekewe hilo halipo.
Lusinde huwa anaongea maneno gani anapowazungumzia wapinzani? Mababy je ni neno zuri? Malofa je ni jina zuri?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom