Hasira za Naibu spika kwa upinzani kuligharimu taifa kiasi kikubwa

naona umeeleza kishabiki bila mantiki zenye hoja za maana. ifike wakati sasa ushabiki tuweke pembeni na tuelezane ukweli kama wapinzani. usije kutudanganya danganya hapakama watoto wadogo. tumeshadanganywa sana sasa hivi sio wakati wake. nikuulize kitu. hivi Naibu spika ndie 1)mwenye maamuzi ya kuadhibu wabunge?
2) ni kwa nini wabunge wa upinzani walitoka nje karibu kipindi chote
3) je wabunge hawa walishindwa kujenga hoja kwa kutumia kanuni aalizozitunga wao wenyewe bungeni?
4) nini hasa faida sasa ya kipindi chote kwa wabunge hawa kukaa nje ambayo mwananchi wa kawaida ataipata.
5) wabunge hawa wataenda kusimamia bajeti gani sasa mwaka huu wa fedha kama katika kuipitisha hawakuwepo. wataijuaje kwani hawakushiriki. wataisimamiaje, wataihoji vipi ikiwa itatumika ndivyo sivyo. na wataikosoaje utekelezaji wake.
nashauri katika mwaka huu mpya wa fedha, wakae kimya kwa sababu mipango ya utekelezaji hawakuwepo bungeni. hawataweza isimamia. wasubiri mwaka ujao wa fedha 2017/18. mwaka huu imekula kwao. ni ujinga tu
Wewe jibu swali moja tu!
Hivi mwongozo wa kuhusu wanafunzi waliotimuliwa UDOM bila utaratibu na mwongozo wa mtu aliyevuliwa kofia ni upi unapaswa kusikilizwa? Lipi lenye maslahi kwa umma? Huna jibu rudi shule.
 
Ni ngumu sana kujenga uchumi imara kwa kuwatimua wapinzani bungeni.
Nyerere hakuwa mpuuzi kuikubali ile 20% ya maoni ya wananchi kuruhusu vyama vingine nchini.
Wabunge wengi wa ccm wapo bungeni kwa ushabiki tu, hawana fikra pana za maendeleo.

ni ngumu pia kujenga siasa bora na kupanga mipango ya mendele! kwa kutumia matusi na kejeli za wabunge wa upinzani. kila mtu anamtegemea mwenzake.

wakati umefika sasa kutumia rungu la sheria na taratibu za bunge kuadabisha maozo yote. libaki bunge lenye kujenga hoja na mantiki zenye faida kwa taifa.

sio matusi. eti Sugu ananyooshea wabunge alama ya dole. khaaa ! hata mimi leo mtu akinionyesha hivyo nitakula nae sahani moja. ni uhuni wa kitoto sana na aibu kwa taifa. hawa ndio wapinzani tunaowategemea. na haya yote ndio yameleteleza serikali kukata tamaa ya kulifadhili bunge kuonyeshwa live. hatutaki kufundisha watoto wetu na kizazi kijacho akili za kihuni kama hizi. wajifunze maadili mema katika kuishi na kutenda.
 
naona umeeleza kishabiki bila mantiki zenye hoja za maana. ifike wakati sasa ushabiki tuweke pembeni na tuelezane ukweli kama wapinzani. usije kutudanganya danganya hapakama watoto wadogo. tumeshadanganywa sana sasa hivi sio wakati wake. nikuulize kitu. hivi Naibu spika ndie 1)mwenye maamuzi ya kuadhibu wabunge?
2) ni kwa nini wabunge wa upinzani walitoka nje karibu kipindi chote
3) je wabunge hawa walishindwa kujenga hoja kwa kutumia kanuni aalizozitunga wao wenyewe bungeni?
4) nini hasa faida sasa ya kipindi chote kwa wabunge hawa kukaa nje ambayo mwananchi wa kawaida ataipata.
5) wabunge hawa wataenda kusimamia bajeti gani sasa mwaka huu wa fedha kama katika kuipitisha hawakuwepo. wataijuaje kwani hawakushiriki. wataisimamiaje, wataihoji vipi ikiwa itatumika ndivyo sivyo. na wataikosoaje utekelezaji wake.
nashauri katika mwaka huu mpya wa fedha, wakae kimya kwa sababu mipango ya utekelezaji hawakuwepo bungeni. hawataweza isimamia. wasubiri mwaka ujao wa fedha 2017/18. mwaka huu imekula kwao. ni ujinga tu

sema mwaka huu imekula kwetu , jingalao
 
Ni ngumu sana kujenga uchumi imara kwa kuwatimua wapinzani bungeni.
Nyerere hakuwa mpuuzi kuikubali ile 20% ya maoni ya wananchi kuruhusu vyama vingine nchini.
Wabunge wengi wa ccm wapo bungeni kwa ushabiki tu, hawana fikra pana za maendeleo.
Mbona Rwanda wameweza. Na Kenya ya Moi mbona uliweza?
 
Wewe jibu swali moja tu!
Hivi mwongozo wa kuhusu wanafunzi waliotimuliwa UDOM bila utaratibu na mwongozo wa mtu aliyevuliwa kofia ni upi unapaswa kusikilizwa? Lipi lenye maslahi kwa umma? Huna jibu rudi shule.
huwezi linganisha hayo mawili. kila moja lina sensitivity yake katika taifa. mwingozo wa UDOM ulikuwa hauna maana pale kwa sababu hatua zilishaanza kuchukuliwa na serikali. ingekuwa ni kupiteza fedha za walipa kodi bure. je nikuulize hatua iliyochukuliwa na serikali kwa sasa ina mantiki au haina. jibu hili nikuone uelewa wako kama umesoma vya kutosha. na ukijibu vizuri utatambua sasa je mwongozo ulikuwa na maana ama la.ifike mahala tutenganishe siasa na masuala nyeti ya utaifa.tusiende kibubu bubu tu wajameni.
 
Sita aliwahi kuwaasa kuwa ni vyema serikali na hata uongozi wa bunge ukawa na ngozi ngumu. Maana yake sio kila kitu ni cha kutoa adhabu! Katika bunge hili NS amekuwa analiongoza kwa hadira zaidi badala ya kutafuta maridhiano!

Na inaonekana bado wabunge wengi wa ccm wana hasira za uchaguzi.

Kwa hiyo kwa sasa inatafutwa sababu yoyote ili kuukomoa upinzani kwa sababu waliwatesa sana mwaka jana. Ukimsikiliza Mwakyembe anavyoongea huwezi kuamini ni mwanasheria wa kiwango cha Phd . siasa tupu! Weledi umewekwa kando.

Bunge la vyama vingi haliwezi kwenda smoothly. Ni mtifuano mwanzo mwisho. Viongozi wa bunge wanapaswa kulielewa hilo sio kukazana kuwafukuza wabunge wa upinzani.
 
leo nimejisikia tu kusoma historia ya Pyongyang......
 
Naanza kuamini sura ya mtu ni tafsiri ya moyo na tabia yake; angalia kauli na matendo ya hawa watu wawili Dr. Tulia & Donald Trump then slightly drag into their appearance
 
Nashindwa kuelewa ni kwanini baadhi ya mambo hasa yanayolihusu taifa tunatanguliza ushabiki na hisia zisizokua na msingi wowote kwa taifa.

Nimejaribu kufuatilia kisa hasa cha Naibu spika pamoja na kamati yake ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge kiilichopelekea kuwatimua wabunge wa upinzani sio kutofuata kanuni na taratibu za bunge bali ni hasira, hisia za kiitikadi, hofu na kukosa busara za kiongozi. Kwa mtu mweledi kiuongozi huwezi kutatua matatizo yako kwa kuwaadhibu wakosaji wako wote, hiyo haipo duniani kote! busara hua inatakiwa kutangulia wakati wa maamuzi siku zote.

Nina uhakika kwa kiongozi makini mwenye busara asingeweza kuwatimua wabunge kama akina Lissu, Zitto na Mdee, alitakiwa kwanza kuwachukua kama wapinzani angetafuta namna nzuri ya kuishi nao vizuri, hawa ni wasomi wazuri kuwatumia kwa maslahi ya kitaifa, michango yao ingeweza kusaidia kung'amua mambo magumu sana kama ambavyo tuliona awamu ya tano.
Matokeo yake hasira na hisia za kisiasa zisizokua na maana ndizi zilizotumika.

Kwa hakika pamoja Naibu spika kama msomi wa sheria pamoja na uwepo wa mwanasheria mkuu bungeni ni hakuna anayemfikia Mh Tundu Lissu, Mwanasheria alikuwepo wakati wa awamu ya tano meishoni, Naibu spika alikuwepo bunge la katiba pia wote hawa hawakua na uwezo wa kung'amua mambo kumpita Tundu LISSU na hata Mh Zitto Kabwe.

Nina imani kabisa mambo kama haya ya miamala ya pesa kwenye taasisi za kifedha na mitandao ya simu na lile suala la kukatwa viinua migongo kwa viongozi wakuu wa kisiasa wangekuwepo wabunge hawa wa upinzani wangeweza kuishauri vizuri serikali, angalia sasa kuhusu suala la miamala ya fedha linataka kufanana na suala la sukari.

Ni ukweli usiopingika kutokuwepo kwa wapinzani bungeni kutaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana, tutegemee mengi kujitokeza baadaye zaidi kutokana na maamuzi yaliyofanywa na wabunge wa CCM peke yao.

Pasina shaka yeyote uwezo wa Tundu Lissu na Mh Zitto ni mkubwa sana kuliko wabunge wengi wa CCM. Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo. Juzi juzi tu serikali aliwasilisha bungeni hoja ya walichokiita mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano lakini kwa macho ya Lissu na Zitto walikataa kabisa bungeni kwa kudai kua ule haukua mpango wa maemdeleo! Lakini wakati huo Naibu spika alikuwepo, Mwanasheria mkuu wa serikali alikuwepo lakini pia waziri wa katiba na sheria nae alikuwepo kwanini hawakuiona kasoro hiyo? Asingekuwepo Zitto na Lissu ni mpango upi ambao ungejadiliwa?

Ikumbukwe kwa kiasi kikubwa kwenye bunge la jamhuri ya Muungano awamu ya tano Spika wa bunge la wakati huo Mh Anne Makinda aliwatumia sana Lissu, Mdee, Zitto na Change kwa masuala mbalimbali yaliyokua na tija kwa taifa letu! Naibu spika Dkt Tulia ameamua kuachana na busara za mama Makinda, yeye ameona kila anayeomba mwongozo ni kumuadhibu tu kwa kutohudhuria vikao hadi mpaka wapinzani wote waishe bungeni.

Nina uhakika kukosekana kwa upinzani wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya serikali kutakua na madudu mengi Sana, tutegemee mkanganyiko wa kauli na sheria mbali mbalimbali serikalini pindi utekelezaji utakapoanza.
Mkuu tayari mkaganyiko umeanza tazama tra wanamuagiza gavana kusitisha utozwaji wa 18%vat kwenye miamala ya mabenki,gavana anasema tra hawajui walisemalo!
 
Ni ngumu sana kujenga uchumi imara kwa kuwatimua wapinzani bungeni.
Nyerere hakuwa mpuuzi kuikubali ile 20% ya maoni ya wananchi kuruhusu vyama vingine nchini.
Wabunge wengi wa ccm wapo bungeni kwa ushabiki tu, hawana fikra pana za maendeleo.
Wao kwao kipaumbele ni stawi wa chama,
 
hata kama ni kweli hayo uliyo yabandika hapo!! hawana haki ya kuvunja kanuni, taratibu na sheria walizo weka wao wenyewe!!!

shida kuu nchii mnapenda jadili individuals!! nakuamini hawakosei ni binadam na wanakosea!!! sheria ikate kotekote!!
Ni kanuni na sheria zipi zilizovunjwa na hao wabunge?kuhoji mambo ya msingi kwa mustakabali wa ustawi wa taifa letu?
 
busara kuvunja kanuni na taratibu?? upinzani kuna mahala wanakosea sana na ni kutafuta kiki kipind hiki!! busara gani unayeizungumzia wakati wao hawana??
Unapo pinga hoja pinga kwa hoja,ni kanuni zipi wamevunja?
 
Ndugu kumbukeni niliwahi kusema hapo awali kwamba kupitishwa kwa bajeti kuu ya serikali bila kuwepo wabunge wa upinzani italeta shida sana kiutendaji kwa sababu wabunge waliobaki ndani hawakuwa na hoja za msingi kuikosoa serikali nakuishauri ipasavyo zaidi ya kuongea kishabiki bila uchambuzi makini wa hoja....Mfano mzuri jana makampuni ya simu na taasisi za fedha zimetoa maelekezo kwa makato yatakayolipwa na mlaji yaani 18% VAT kwa gharama za miamala ya fedha,,,.LAKINI cha ajabu serikali leo imekuja na kauli kinzani yakusema ni marufuku kutoza gharama za miamala ya fedha...sasa nani atakaye fidia hasara hizo kama sio mlaji??????????????????? jambo hili litakuja kufanana sana na kupiga marufuku uagizaji wa sukari nje ya nchi lakini mwisho wa siku upungufu mkubwa wa bidhaa hiyo umeonekana nchini kitu ambacho kimepelekea bei kuwa juu hadi leo!! nini serikali inafanya????????? kuitwa mpinzani sio kwamba hana haki yakutoa ushauri mzuri kwa manufaa ya taifa,,,, kasumba ya kufuata maamuzi ya kisiasa ndo yanaligharimu taifa kwa kulivuruga taifa badal ya kuliongoza kwa njia nyoofu!!!
uwezo bila busara ni zero walipaswa kufuata kanuni ili wasurvive kwa manufaa ya umma
 
Mimi nawapongeza wabunge wa CCM kwa kupigania nchi tupate masanamu ya Diamond na Magufuli akipiga push up, na ninampongeza yule aliyelia kwa bunge kuonyeshwa live kwani ameonyesha ukomavu wa hali ya juu kwa taifa lake, vilevile naomba serikali ikubali ombi la mbunge kessy kuwa hata wanaofuga kuku na waendesha baiskeli walipe kodi kwani hamna kitu cha bure hapa serikali inakosa mapato
 
Kumbe bunge lilifichwa mwanao asione wewe ulionaje kama kaonyeshwa dole la kati .....kweli ww bwege uchwara
sawa basi, kwa hiyo wewe una mawazo gani kama wewe. usitukane tu bila hoja kichwani. umepewa akili itumie sio unafikiri kwa kutumia miguu na macho mzee
 
Mkuu tayari mkaganyiko umeanza tazama tra wanamuagiza gavana kusitisha utozwaji wa 18%vat kwenye miamala ya mabenki,gavana anasema tra hawajui walisemalo!
Serikali ya kukurupuka. Ukawa wajipange 2020 nchi yao. Yoyote atayeteuliwa ntampa kwa Ukawa.
 
Serikali ya kukurupuka. Ukawa wajipange 2020 nchi yao. Yoyote atayeteuliwa ntampa kwa Ukawa.
Huo ni uamuzi mzuri sana mkuu ebu eneza wazo lako kwa watu angalau 1milion huo ndio utakuwa mwanzo mwema wa kujikomboa
 
Back
Top Bottom