MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Nashindwa kuelewa ni kwanini baadhi ya mambo hasa yanayolihusu taifa tunatanguliza ushabiki na hisia zisizokua na msingi wowote kwa taifa.
Nimejaribu kufuatilia kisa hasa cha Naibu spika pamoja na kamati yake ya bunge ya haki, maadili na madaraka ya bunge kiilichopelekea kuwatimua wabunge wa upinzani sio kutofuata kanuni na taratibu za bunge bali ni hasira, hisia za kiitikadi, hofu na kukosa busara za kiongozi. Kwa mtu mweledi kiuongozi huwezi kutatua matatizo yako kwa kuwaadhibu wakosaji wako wote, hiyo haipo duniani kote! busara hua inatakiwa kutangulia wakati wa maamuzi siku zote.
Nina uhakika kwa kiongozi makini mwenye busara asingeweza kuwatimua wabunge kama akina Lissu, Zitto na Mdee, alitakiwa kwanza kuwachukua kama wapinzani angetafuta namna nzuri ya kuishi nao vizuri, hawa ni wasomi wazuri kuwatumia kwa maslahi ya kitaifa, michango yao ingeweza kusaidia kung'amua mambo magumu sana kama ambavyo tuliona awamu ya tano.
Matokeo yake hasira na hisia za kisiasa zisizokua na maana ndizi zilizotumika.
Kwa hakika pamoja Naibu spika kama msomi wa sheria pamoja na uwepo wa mwanasheria mkuu bungeni ni hakuna anayemfikia Mh Tundu Lissu, Mwanasheria alikuwepo wakati wa awamu ya tano meishoni, Naibu spika alikuwepo bunge la katiba pia wote hawa hawakua na uwezo wa kung'amua mambo kumpita Tundu LISSU na hata Mh Zitto Kabwe.
Nina imani kabisa mambo kama haya ya miamala ya pesa kwenye taasisi za kifedha na mitandao ya simu na lile suala la kukatwa viinua migongo kwa viongozi wakuu wa kisiasa wangekuwepo wabunge hawa wa upinzani wangeweza kuishauri vizuri serikali, angalia sasa kuhusu suala la miamala ya fedha linataka kufanana na suala la sukari.
Ni ukweli usiopingika kutokuwepo kwa wapinzani bungeni kutaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa sana, tutegemee mengi kujitokeza baadaye zaidi kutokana na maamuzi yaliyofanywa na wabunge wa CCM peke yao.
Pasina shaka yeyote uwezo wa Tundu Lissu na Mh Zitto ni mkubwa sana kuliko wabunge wengi wa CCM. Hii na ndio maana Mh Tundu LISSU ni wakili wa Mahakama kuu ya Tanzania kwa sababu Rais wa wakati ule Mh Kikwete aliona uwezo wake na ndio maana akaona ampe nafasi hiyo. Juzi juzi tu serikali aliwasilisha bungeni hoja ya walichokiita mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano lakini kwa macho ya Lissu na Zitto walikataa kabisa bungeni kwa kudai kua ule haukua mpango wa maemdeleo! Lakini wakati huo Naibu spika alikuwepo, Mwanasheria mkuu wa serikali alikuwepo lakini pia waziri wa katiba na sheria nae alikuwepo kwanini hawakuiona kasoro hiyo? Asingekuwepo Zitto na Lissu ni mpango upi ambao ungejadiliwa?
Ikumbukwe kwa kiasi kikubwa kwenye bunge la jamhuri ya Muungano awamu ya tano Spika wa bunge la wakati huo Mh Anne Makinda aliwatumia sana Lissu, Mdee, Zitto na Change kwa masuala mbalimbali yaliyokua na tija kwa taifa letu! Naibu spika Dkt Tulia ameamua kuachana na busara za mama Makinda, yeye ameona kila anayeomba mwongozo ni kumuadhibu tu kwa kutohudhuria vikao hadi mpaka wapinzani wote waishe bungeni.
Nina uhakika kukosekana kwa upinzani wakati wa kujadili na kupitisha bajeti ya serikali kutakua na madudu mengi Sana, tutegemee mkanganyiko wa kauli na sheria mbali mbalimbali serikalini pindi utekelezaji utakapoanza.