Hasira za Kumfumania Mume Akijivinjari na Hausigeli Kwenye Gari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasira za Kumfumania Mume Akijivinjari na Hausigeli Kwenye Gari

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sunday, August 23, 2009 6:32 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ambaye alimfumania mumewe akila uroda na hausigeli wake kwenye gari lao la kifahari aina ya Porsche lenye thamani zaidi ya Tsh. Milioni 140 ameliuza gari hilo kwa Tsh. Milioni 4 tu. Ili kulipa kisasi cha kumfumania mumewe akila uroda na msichana wake wa kazi kwenye gari lao kifahari aina ya Porsche 911, mama mwenye nyumba aliamua kuliuza gari hilo kwa bei ya kutupa.

  Mwanamke huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni, alipata hasira baada ya kumfumania mumewe na msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye aliajiriwa kwaajili ya kuwaangalia watoto wake.

  Gari hilo ambalo thamani yake ni takribani paundi 70,000 (Zaidi ya Tsh Mil. 140) liliwekwa kwenye tovuti ya Gumtree likiuzwa kwa paundi 2,000 tu (Tsh. Mil 4.6).

  Ili kuwavutia wateja zaidi, mwanamke huyo aliziweka chupa za mvinyo za mumewe kwenye buti la gari hilo kama zawadi kwa mnunuzi wa gari hilo.

  Akielezea tukio hilo mwanamke huyo alisema kwamba siku ya tukio alimuaga mumewe anaenda kumtembelea mama yake lakini alirudi mapema tofauti na alivyotarajia baada ya kukorofishana na mama yake aliyeenda kumtembelea.

  Alirudi nyumbani na kukuta watoto wamelala lakini mumewe hayupo. Wakati akimtafuta mumewe kwenye nyumba yao alisikia sauti zikitoka kwenye banda ambalo gari lao huhifadhiwa.

  Alipoenda kuhakikisha ni sauti za kitu gani zinatoka kwenye banda hilo, alipigwa na butwaa kumkuta mumewe wa miaka 15 akila uroda na msichana wake wa kazi ndani ya gari lao.

  "Sikuamini kabisa, huyu msichana ana umri wa miaka 17 tu, nilikuwa nikimchukulia kama binti yangu" alisema mwanamke huyo.

  Mwanamke huyo kutoka mji wa Solihull, alisema kwamba aliamua kuliuza gari hilo kwakuwa alishawahi kumfumania mumewe akitembea nje ya ndoa na wanawake wengine mara kadhaa kabla ya siku hiyo na aliongeza kuwa hana mpango wa kuivunja ndoa yao ya miaka 15.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2889110&&Cat=2
   
Loading...