Hasira na uadui why? Kuna siri gani kwenye hizi biashara? Kwanini wanakuwa na hasira na kutengeneza uadui ukigoma kujiunga nao?

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,205
4,695
Nazungumzia biashara Mtandao yaani Network Marketing

Sizungumzii faida au hasara au uhalali wa hii biashara bali chuki au Uadui unapogoma Kujiunga nao. Hadi leo sijui nini chanzo cha wao kuwa na hasira au chuki za wazi kabisa

Namaanisha anapojaribu kukushawishi uingie au ujiunge kwenye biashara yake nawewe ukagoma au ukatoa hoja kinzani lazima ugeuke kuwa Adui yao?

Ukweli atakuchukia sana hata kama mlikuwa karibu naye

Kwanini? Kuna nini kwenye hizi biashara Mtandao? Mtu ANAFANYA uadui na kila mtu kuanzia marafiki hadi Ndugu zake wa damu kisa WAMEGOMA kujiunga kwenye biashara yake ya Mtandao

Chuki, chuki, chuki why?

Karibuni tuchangie
 
Ili apate pesa zaidi kwenye hiyo biashara, anawajibika kuwashawishi watu wa karibu wajiunge kwa wingi, kujiunga kwao ndo wafanikio yake, kwahiyo inapotokea unamchomolea dili lake basi lazima akuchukie..ila kiufupi Ni UTAPELI TU.
 
Multi Level Marketing ni cult fulani hivi ambayo usipokua makini unaweza chukia ndugu, rafiki na wewe mwenyewe ukajichukia. Kwanza wanakuaminisha hao ndio familia yao na ndio watu pekee wanaokujali which is true kwa muda huo imagine unajaribu kuunganisha watu halafu wote wanakuona unapoteza muda isipokua wao tu ndio wanakuthamini, hapo ndio chuki dhidi ya watu wako wa karibu inazidi.​
Pili wanakua na seminars zao kila baada ya muda ili kukutia sumu zaidi ila pia wanakufanya ujichukie zaidi kwa wewe kushindwa kushawishi watu kujiunga nao hali ya kua unapewa mafunzo mara kwa mara . Hali inayokufanya ujione mzembe kwa kutopata wengine chini yako. Wakati ukweli ni kua bidhaa zao sio relevant na bei ni kubwa maradufu. Ila sababu ya zile seminars zao wanakuaminisha tatizo ni wewe na si wao.​
Hapo unajitutumua tena unaenda kutafuta mtu wa kujiunga nae lakini nae anachomoa. Kutokana na huu mlolongo ni lazima umchukie kila mtu aisee maana nafsi yako ishakosa amani.​
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Kwanini Magufuli husipokubaliana nae kwa hoja unageuka kuwa adui yake na anawaaminisha watu kwamba wewe ni msaliti wa taifa,na anaweza kukutumia watu wasiojulikana wakutandike risasa zaidi ya 16?
 
Back
Top Bottom