Hasira hazijatosha, haiwezekani JK adharau na sisi tukae kimya..!

akilimtindi

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
421
83
Nahisi hasira za Wadanganyika hazijatosha kabisa, nilihisi zimefikia kiasi cha kufanya jambo lakini kwa hili nimegundua bado kabisa. Nasema hivi kwasababu sikutegemea kabisa kwa ufuska wote huu uliofanywa na Serikali hii kwa rasilimali za Taifa hili na uliosemwa wazi na wabunge JK akalikalia kimya na wananchi wakanyamaza na kubaki tu wakinong'ona huku chini chini tena kwa woga ule wa mwaka 1947.

Kwa uelewa wangu mwepesi kwenye mambo ya siasa nilitegemea mambo kadhaa, kwanza nilitegemea kabisa kwamba kwa hili lazima JK atafanya jambo la kuonyesha kujibu tuhuma nzito zilizotupiwa serikali yake aidha kwa kuwashauri mawaziri wake wajiuzulu kupunguza munkari wa jamii ya Watanzania kwa ujumla wake, au nilitegemea basi bunge lingeonyesha dalili ya kufanyia kazi hoja iliyotarajiwa kupelekwa mezani kwa Spika tangu wiki iliyopita. Lakini ajabu kubwa ni kwamba bunge limeyeyusha na JK katoa msemo ambao kiukweli sijaamini kwamba kautoa yeye au kasingiziwa, eti kasema huo ni "upepo na utapita tuu.." hii ni dharau kubwa kuliko ninazozijua kwakuwa hii imetoka na kusikika, inamaanisha mnajisumbua na hamuwezi kufanya chochote.

Kikubwa kuliko vyote kilichonifanya nione kwamba hasira zetu bado kabisa ni kitendo cha Wadanganyika kukaa kimya pamoja na matusi hayo kutoka kwa JK, ni ajabu kubwa mno hiyo. Niliamini kabisa kwamba kwa misemo hii kutoka kwa JK wakati huu basi ilikuwa imefika wakati Wadanganyika watoke na kudai wanachokitaka maana kiko wazi tayari. Kwani kulikuwa na ugumu gani leo watu wote wakasema hawaendi popote hadi mawaziri watoke, ama hadi bunge liongeze siku na kuamua kumtwangia PM kura ya kutokumwamini? Kama hasira zimetosha basi nahisi kilichobaki ni mobilization, kimsingi tutakuwa resources tunazo kwa maana ya watu na hasira zao. Kinachotakiwa ni kuelekeza hizo resources kwenye kazi fulani kwa manufaa ya Taifa hili.

Something has to be immediately, we have to hit the iron while it's still Hot otherwise JK atathibitisha alilolisema "huu ni upepo na utapita.." We have to instead prove what Sugu said, .."hii ni dhoruba na haitapita hivi hivi, lazima iondoke na sehemu legelege kama sehemu yote".

I'm not suggesting a strike as far as no mobilization for that at the moment, nashauri ingewezekana kesho wote tutulie walau kwa kesho tu tusifanye chochote tuone JK atasema nini kuhusu sisi Wadanganyika kukaa tu kimya maana itambidi kuongea. Kama kuna mwenye plan mbadala tujadiliane, tupate mawazo kutoka pande zote maana hata CCM hili linawakera waziwazi.
 
Kikwete atakuja kutoa roho za watz.............kunashida nchini yeye anakimbilia nje kwa ajili ya kusaini tu miposho ya safari ili kujitengenezea neema ya baadaye tukimwondoa kwa nguvu ya umma

nguvu ya umma yaja kwa kasi ya ajabu
 
This is a quote from a local paper "They warned that if the ministers did not quit, it would be better if Pinda himself stepped down so as to give the President a free hand to pick a fresh team"

This statement shows how incopetent JK is, its a disgrace JK doesnt have the common sense or is incapable of sacking his own corrupt ministers??

He didnt fire Lowassa even after plain evidence of corruption and theft parliament had to do it for him, he is now unwilling to fire Pinda, maybe its time the president himself is held to account. By the way Zitto just became my new hero.
 
Tunasubiri siku 14 kuona kama bunge litakaa na kujadili hili suala. Kama siku 14 zitapita na hakuna mabadiliko katika baraza la mawaziri na bunge kama litakataa kujadili hili suala ndipo tutajua nini cha kufanya. Kwa sasa ni mapema sana kuchukua maamuzi.
 
Inabidi tukubaliane sisi sote wakati wa mazungumzo na minongono umepita karibia miaka ishirini tunayazungumzia yale yale huku wengi wetu tunazidi kuumia. "Tahrir Square" maandamano, migomo time for action
 
Sina hakika kama wabunge wa magamba wataunga mkono hoja Hii walikuwa wakali wakati wa kuchangia inapofika wakati wa kuchukua hatua waoga Njoo kwasababu wao Si wawakilishi wa wananchi waliowatuma ila wako kwa maslahi ya chama chap cha makamba.

Nakuelewa vyema sana Mkuu, hivi inawezekana kwamba bado wabunge wa CCM wana matarajio ya chama kuwatetea wakirudi majimboni kwa hali ilivyo sasa hivi?

Nadhani wamekuwa wakali kiasi fulani wakijua kwamba wakirudi majimboni mwao kuna moto unawasubiri, pakiwaka moto kwa sasa chama kina uwezo wa kuwatetea?

Kama sivyo kwanini wabunge wanakuwa waoga kufanya kazi tuliyowatuma? ina maana kwamba hii yote bado ni maigizo ingawa wao bila kujua wanatusaidia sana kuwasha kuongeza kuni kavu kwenye huu moto unaowaka sasa. Kama hili litapita hivi hivi bila kushughulikiwa ipasavyo, nahisi JK atakuwa amekomaa kwenye siasa chafu na kwa misingi hii basi kesho au kesho-kutwa anaweza kufanya lolote na tusiweze kumfanya chochote.
 
Baada ya kiko cha bunge kuahirishwa, na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali dhidi ya mawaziri waliotuhumiwa, imedhihirisha habari zilizoandikwa na Tanzania Daima kuwa Rais amekingia kifua mawaziri, na kusema ni upepo tu utapita.

Waziri mkuu naye ameendeleza uongo wake kwa umma, baada ya kushindwa kutekeleza ahadi ya kutoa maamuzi kama alivyoahidi J1.

Sasa Msako ndiyo umeanza rasmi dhidi ya serikali legelege chini ya rais legelege.
 
Nadhani wananchi wote mliokuwa makini kufwatilia mwenendo wa kikao cha bunge leo mmeshuhudia jinsi Waziri mkuu alivyoulaghai umma wa watanzania kwa kuongelea masuala yasiyokuwa na msingi kwa Taifa letu na kuruka yale ambayo watanzania wote tulitega masikio kuyasikia kwa hamu kubwa. Tulitegemea angetoa uamuzi/kauli ya serikali juu ya mawaziri wote ambao wamefanya ubadhirifu katika ofisi za Umma. katika hali kama hii, waziri mkuu hata kugusia hajagusia. Naimani huyu katudharau sana sisi tunaojiita wenye nchi. Hatuwezi kuendelea kuiacha serikali yetu mikononi mwa viongoz wezi na wabadhirifu na wanaotetea mfumo dokozi.

Shime wananchi wote wazalendo tunajidiliane hapa what is the way forward????hii hali hatuwezi kuendelea nayo. Maana serikali imeamua kulinda wezi kibabe.
 
Tupo Afrika mzee! Ndiyo siasa zetu hizi! Ahadi za uongo zinatolewa na PM na wananchi wote wanamsikia na hatimizi, na hasemi kwamba aliahidi lakini hafanyi kwa sababu gani. Anakaa kimya tu kana kwamba hakuongea kitu. Mambo haya yanawezekana Afrika tu, tena Tz ndio sana.
 
Inasikitisha kuona serikari ikiwafanya tena wanzania mataahira wa akili, haingii akilini kuahirisha bunge bila kutoa taarifa ya wezi wa pesa za uma, rungu wamelipewa tena la kwenda kuendelea kuiba, lakin cha ajabu wote tuko kimya, wabunge nao hoo is there any plan B ya ufumbuzi wa tatizo hili,jamani tusaidiane katika hil
 
Back
Top Bottom