Hasira hasara soma kisa hiki

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Hasira Hasara!

Mmiliki wa kampuni moja kubwa aliamua kutembelea site ili aone kazi zinavyoenda, akakuta Kijana mmoja amesimama huku wenzake wanapiga kazi. Akamwambia, "Wee Kijana, mimi sijaajiri mtu ili aje asimame, nimeajiri mtu kwa kumlipa laki 5 ili afanye kazi". Boss akazama mfukoni, akatoa milioni 1 na laki 5, akampa yule Kijana halafu akamwambia, "Hiyo ni Pesa yako ya miezi mitatu, kuanzia leo kazi basi, sitaki tena kukuona".

Kijana wa watu akasepa. Baada ya muda kidogo, Boss akawauliza Vijana waliobaki, "Hivi huyu Kijana niliyemtimua kazi, ni Fundi wa nini ili kesho tuajiri mwingine?". Ujue Kampuni nyingi kubwa, huwa zina Wafanyakazi wengi sana, kiasi kwamba, siyo rahisi Boss kuwafahamu wote. Wale Vijana wakamjibu, "Boss yule siyo Fundi na wala siyo Mwajiriwa wa hii Kampuni, yule ni Muuza Karanga, huwa anapita hapa kutuuzia Karanga".

Hii ndio inaitwa "Hasira Hasara".
 
Back
Top Bottom