Hasimu wa Bashe akana jina mahakamani; atimuliwa na wazee wa Nzega | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasimu wa Bashe akana jina mahakamani; atimuliwa na wazee wa Nzega

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Aug 19, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  mgombea wa ccm upande wa nzega mimbizi wetu dk kigangwalla ameenda kukana jina lake mahakamani jana ..habari zaidi zinasema dk alienda kukaana baada ya kushauriwa na baadhi ya waanasheria ...je hili litamsaidia kumuizinisha kugombea kama mkimbizi
  YETU MACHO

  Wakati hayo yakiendelea mgombea huyo alikuwa na kikao na wazee wa ccm wilaya ya nzega kuandaa jinsi gani ya kumsaidia kumkapenia..kijana huyo alipofika akumuamkia hata mtu mmoja na habari zaidi zinasema hilo liliwawakasirisha baadhi ya wazee na kumuuliza mbona hana heshima akasema sio lazima kumuamkia mtu..wazee wakiwa wanaanza kumfundisha akapigiwa simu akapokea alipomaliza akarudi ndani na kuulizwa kijana mbona huna heshima akajibu nina heshima tatizo lenu nini??akawaambia hii ni simu ya wakubwa toka juu siwezi kuacha kupookea na hakuna mwenye mamlaka kunizuia kupokea simu zangu ndipo mwenyekiti na wengine wakasema kikao kimekufa na kila mtu achukue ustaarabu wake

  mzee mmoja alipoulizwa akaasema huyu kijana atujui anahisi huko juu ndio watampa ubunge haya sasa hiyo kampeni ataifanya mwenyewe na tuone ataishia wapi nishawaambia wenzangu nisisikie kikao cha kumhusu huyu muhuni alilamama mzee mmoja

  Hayay huyu ndie MBUNGE WETU WA CCM KUPITIA MAKAMBA/RAIS KIKWETE
  KAZI TUNAYO
   
 2. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona mwandishi mwenyewe unaonekana umepitia shule tuu?!Nachelea kusema wewe ndiye mwandishi ninayemfahamu Samson Mfalila wa magazeti ya michezo!Kama si mwenyewe tafadhari badilisha hilo jina tusije tukamhukumu Mfalila aliye smart!
   
 3. D

  Dick JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kina taratibu zake. Kama yeye alijua kuwa kupitishwa kuwa mgombea ubunge ni kuwa juu ya taratibu hizo, imekula kwake!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Aug 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Akikana jina lake ndio inakuwaje na kwa nini alikane?
   
 5. dkims

  dkims Senior Member

  #5
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mkuu amekana jina lake la sasa au la zamani?????????/
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Bado ndio kwanza tuko kwenye mazoezi mechi haijaanza bado si mchezo yaani kazi ipo na si ndogo
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pure umbeya. How can I/we trust you?
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Aug 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280

  Habari hii imeandikwa na Mwananchi:
  Kigwangalla azua kizaazaa wilayani Nzega


  Thursday, 19 August 2010 09:29

  Mwandishi Wetu, Nzega  KAMATI ya Siasa ya CCM Wilaya ya Nzega, imevunjika baada ya mgombea ubunge wa jimbo hilo Dk Hamis Kigwangalla kudaiwa kuonyesha utovu wa nidhamu katika kikao hicho.

  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Nzega, Dk Kigwangalla alikuwa hatii anachoelezwa na mwenyekiti wa kamati hiyo hivyo kusababisha mwenyekiti kuvunja kamati hiyo.

  "Ni kweli kamati imevunjika leo (jana) wakati tukijadili ajenda ya mwisho, lakini sisi kama chama lazima tutamsaidia ili aweze kushinda,"kilieleza chanzo hicho.

  Taarifa zilisema kwamba mgombea huyo aliingia katika kikao hicho ambacho lengo lake lilikuwa ni kupanga mkakati wa kumsaidia kushinda, lakini hakuwasalimia wajumbe.

  Kufuatia hatua hiyo, mwenyekiti wa kikao akamuliza kwanini hajasalimia wajumbe, lakini kabla ya Kigwangalla kujibu, simu yake ikaita.

  "Alipoanza kupokea simu kabla ya kujibu swali, mwenyekiti akamwamuru azime simu, yeye akamjibu kwamba hawezi kwamba hawezi kuacha kupokea kwa kuwa inatoka kwa wakubwa," alisema mjumbe mmoja aliyekuwako katika kikao hicho.

  Kutokana na kitendo hicho, wajumbe waliamua kuvunja kikao bila ya ajenda ya kupanga mkakati wa ushindi kujadiliwa.

  Hata hivyo, Dk Kigwangalla alipopigiwa simu ili aeleze kuhusu taarifa hizo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

  Katika hatua nyingine, taarifa kutoka Nzega zinadai kuwa maaofisa wa Idara ya Uhamiaji wamelazimika kumhoji mama yake, Dk Kigwangala ili waweze kupata ukweli wa uraia wake.


   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kichuguu naona umemuweka jamaa panapostahili.
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  la zzamani
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  we hata mzazi wako unaweza usiamni ndie aliekuzaa kwa style hiyo lohhh
  wenzako wanauliza kwanza chanzo unajibiwa...
   
 12. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #12
  Aug 19, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM achana na huyo Dr Kigwangwalla,kwa vile issue ya Bashe imekwisha mrudisheni kwenye mbio za kusaka kiti cha jimbo hilo.

  Dr Kigwangwalla atakuyumbisheni sana mpaka mtajuta kumfafamu
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hii Nzega ilikuwa apewe Bashe, lakini ugomvi wake yeye na Ridhiwani ndani ya UVCCM inapelekea hata kumchomea (uongo) ili tu mambo yake yakwame. Hapo JK an JK juniour ROHO KWATU kabisa. Namsikitikia kibaraka Ma-rope hapo atakapo kuja kukaa upande wetu, mwambieni aangalie historia ya makatibu wa CCM wote (Gama, yule wa Iringa, Kolimba (RIP) ukiondoa Rashid (RIP). Walitolewa na kunuka kama kinyesi.
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ma rope atakuja kujuta siku akiondolewa ukatibu mkuu, and it is very soon.
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Aug 20, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Eti Kikwete amekana Ridhiwani hahusiki na kuondolewa kwa Bashe!
   
 16. Gottee

  Gottee Senior Member

  #16
  Aug 20, 2010
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu kweli hawezi kuwa Sam Mfalila! Mheshimiwa badili hilo jina haraka! Unashusha hadhi za watu!
   
 17. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Samson Mfalila katika nchi ya watu milioni 40 wanaweza kuwa zaidi ya wawili.Huyo mnayemjua nyinyi wengine huenda hawamjui pia!
   
Loading...