Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Raia wa Nigeria, Ramon Abbas, maarufu kwa jina la Hashpuppi amekiri makosa ya utakatishaji fedha katika mahakama nchini Marekani.
Hashpuppi, aliyejipatia umaarufu kwa maisha yake ya anasa mitandaoni, ambapo ana wafuazi zaidi ya milioni 2.5 katika mtandao wa Instagram, amekiri makosa ya utapeli unaofikia jumla ya dola milioni 24 za Marekani (sawa na zaidi ya Tsh. bilioni 55).
Nyaraka za mahakama zilizowekwa wazi zinaonesha katika tukio moja, Hashpuppi alijaribu kumtapeli dola milioni 1 za Marekani (zaidi ya Tsh. bilioni 2.3) mtu mmoja aliyetaka kufadhili shule moja ya watoto nchini Qatar baada ya kujifanya benki kwa kuonesha nyaraka feki na kutengeneza tovuti feki.
Hashpuppi anatajwa kuwa mmoja wa matapeli wakubwa zaidi wa mtandaoni duniani. Umaarufu wake na wezo wake wa kutengeneza mtandao kumemwezesha kufanikisha matukio makubwa ya utapeli kwa ufanisi mkubwa.
Tapeli huyo alikamatwa mwezi Juni akiwa nchini Dubai, anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela na atapaswa kulipa fidia kamili kwa wahanga.