Hashimu Rungwe amtolea uvivu Rais Magufuli, ahoji nchi imepinda kuelekea wapi?

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Ahoji kauli ya Rais kuwa nchi imepinda kuelekea wapi, Kuelekea Ubungo au Temeke? Anahoji kila mara Rais anasema ufisadi wakati kapewa jeshi, polisi na kodi za kumsaidia, kwanini hakamati hao mafisadi, ahoji CCM kuhoji ufisadi wa Lowasa na kushindwa kumkamata, hivyo wanamsingizia.
Amesema ndani ya miaka 10 nchi imepiga hatua kubwa kwenye maendeleo kuna barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami, vyuo vikuu vilikuwa vitatu leo kuna vyuo vikuu vingi, kuna viwanja vya ndege vimejengwa na vingine kupanuliwa usafiri wa boti za kisasa njia za majini lakini Rais Magufuli anadai nchi imepinda, anahoji maendeleo hayo ndio kupinda kwa nchi?
Anendelea kudai kuwa Magufuli hajafanya chochote cha kujivunia kuwa kainyoosha nchi na kuleta maendeleo tofauti na kununua ndege na kununua ndege unachukua fedha na kununua tu, sio kazi kubwa
Tazama mwenyewe hapa
 
Mtu anaipeleleka nchi kwa haraka utadhani anawahi ndege, sisi hatuhitaji hiyo haraka tumekwisha zoea maisha yetu hayahaya kimasikini
Hhahahahaha, umezoea kula dona dagaa na maisha yanasonga?
 
Achana na watu kama huyu ambao hawajifahamu. Mtu hajui hata Vyuo vikuu vilikuwa vingapi!

Hoja ya msingi ni kwamba Kikwete alipoingia madarakani alikuta vyuo vikuu vichache na mapaka anaondoka vilikuwa vimeongezeka. Kwahiyo, kuna hatua kuelekea mbele ilipigwa. Sasa hii huwezi kufananisha na mtu ambae hakujua hata Saddam Husein alikuwa rais wa wapi, lakini bado wakalazimisha kwiba kura na kumfanya rais. Na haya ndio matokeo yake, inchi inaenda kama gari bovu, na kutwa kuwaponda wenzie kwamba hawajafanya kitu, yeye ndio anakuja kurekebisha au "kunyoosha" nchi kama anavyodai. Ni mkasa huu...
 
Ila hii ghiliba ya kusema kunamafisadi alafu hawakamatwi ni mbaya sn. Ccm hawawezi kufisidi na kujikamata wenyewe. Takukuru wapo likizo . Serikali ina mkono mrefu km tu mwenyenchi uliyewachagua ukiwahoji na kuwa na mtazamo tofauti ndo utaona mkono ulivo mrefu.
FreeLema
 
Hoja ya msingi ni kwamba Kikwete alipoingia madarakani alikuta vyuo vikuu vichache na mapaka anaondoka vilikuwa vimeongezeka. Kwahiyo, kuna hatua kuelekea mbele ilipigwa. Sasa hii huwezi kufananisha na mtu ambae hakujua hata Saddam Husein alikuwa rais wa wapi, lakini bado wakalazimisha kwiba kura na kumfanya rais. Na haya ndio matokeo yake, inchi inaenda kama gari bovu, na kutwa kuwaponda wenzie kwamba hawajafanya kitu, yeye ndio anakuja kurekebisha au "kunyoosha" nchi kama anavyodai. Ni mkasa huu...
Kwakweli ni MKASA MKUBWA KWA TAIFA
 
Mbona kikwete anajua UKIMWI ni kujitakia?
UDOM mwanzilishi ni Mkapa, vyuo vingine ni madhehebu ya kidini na vilianza wakati wa mkapa. Chuo gani unachofahamu kilianza wakati wa Kikwete? BRT ya Dar ni mkopo wa world bank na mambo yalianza enzi ya Makapa. Kuna harufu ya ushabiki wa kidini bado watu inawasumbua sana!!
Mbona husemi Reli iliyoangushwa na utawala uliopita? ATCL iliyokosa ndege hata moja wakati wa utawala huo?
Kumbukeni hapa ni JF. Kuna wasomi wengi kuliko wapiga zomari!
 
Kwakweli ni MKASA MKUBWA KWA TAIFA

Na kama mtu afikirii anaweza akahoji, ohooo sasa akijua Saddam alikuwa rais wa Iraq sisi inatudaidia nini? Jibu ni kwamba ingetusaidia kufaham umakini wa mtu huyu, kitu ambacho ni muhimu kwa nafasi aliyokuwa anaomba. Suala la Saddam lilitikisa dunia nzima, na mtu yeyote mzima mwenye kufuatilia mambo asingeshindwa kufaham angalau alikuwa rais wa wapi. Tumepata kiongozi ambaye sio makini, na kama alivyosema Hashim Rungwe, anaendesha nchi kwa chuki na visasi.
 
Ahoji kauli ya Rais kuwa nchi imepinda kuelekea wapi, Kuelekea Ubungo au Temeke? Anahoji kila mara Rais anasema ufisadi wakati kapewa jeshi, polisi na kodi za kumsaidia, kwanini hakamati hao mafisadi, ahoji CCM kuhoji ufisadi wa Lowasa na kushindwa kumkamata, hivyo wanamsingizia. Tazama mwenyewe hapa

watanzania sijui kawalaani nani, wakati wengine wanapambana na adui mkubwa ccm, wao wanajifanya wameona gold ktk ccm.Baada ya CCm kupona gharika na kuanza fanya yaleyale wanajifanya kulia.Kwanini wasijifunze hata kukaa kimya tuu,kuliko kutetea kitu wasichokielewa.
 
Back
Top Bottom