Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Picha: Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema, Hashimu Juma
Tarehe 07 OKtoba 2021, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha) Hashimu Juma Issa (63) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka mawili, likiwemo la kuchapisha taarifa za uongo na kuzisambaza kwenye mtandao wa YouTube.
Mshtakiwa huyo alifikishwa Mahakamani hapo Alhamisi Oktoba 7, 2021 na kusomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali Yusuph Abood mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu.
Wakili Abood alidai mahakamani kuwa Oktoba Mosi katika eneo la Kinondoni B, mtaa wa Ufipa, mshtakiwa alisambaza taarifa kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro.
Alidai kuwa mshtakiwa alichapisha kwenye kompyuta na kusambaza taarifa kuwa "Sirro ni gaidi namba moja nchini Tanzania na fisadi."
Ilidaiwa katika shitaka lingine kuwa Oktoba Mosi katika eneo la Kinondoni B, mtaa wa Ufipa, mshtakiwa alitoa maneno ya uchochezi kuwa "Sirro ni gaidi namba moja nchini Tanzania na fisadi" kwa lengo la kutengeneza chuki kwa wananchi.
Mshitakiwa huyo alikana mashtaka hayo.
Wakili Abood alidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na uko katika hatua za mwisho.
Issa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh3 milioni kila mmoja, barua ya utambulisho pamoja na kitambulisho cha taifa.
Pia, soma:
1). Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA, Hashimu Issa Juma apelekwa kusikojulikana
2). Mwenyekiti wa BAZECHA akamatwa kwa tuhuma za uchochezi kati ya Serikali na Wananchi
3). Baada ya kufutiwa mashitaka na DPP, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA akamatwa tena na kuswekwa rumande