Hashim Rungwe: Watu wana njaa, hawawezi kushiba usaha wa majipu!

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Akihojiwa na gazeti la mwananchi,aliyekuwa mgombea urais bwana Hashim rungwe amesema watu wana njaa na hawawezi kushiba usaha wa majipu.....kwa maoni yangu huu ni wito na kilio cha wananchi wa Tanzania kuhusu Maisha magumu,uchumi umeishinda srrikali kila mahali ni kilio,
IMG-20160520-WA0005.jpg
 
Mzee Hashim watu walizoea kupiga Fedha bila kufanya kazi.Michongo kila Mahali.Ni watu waliyolelewa Hivyo.Serikali ya Awamu ya pili inabadili Tabia hiyo ili watu waishi kwa Kipato Halali Hili litachukua muda watu Kuzoea.Pesa nyingi chafu zilikuwa zinazunguka Nchini kufikia mahala watu kuona waliyojaliwa na wasiyojaaliwa na kuanza kuibuka TABAKA KUBWA za waliyonazo.Kuifanya Jamii ya waliyowengi kujisikia kana kwamba Serikali Imewatenga.Kwa Mabadiliko haya ya Serikali kubana kila MIANYA Haramu kitatuletea Nafuu hasa katika Serikali kuweza kuhudumia Wananchi wake kwenye Huduma Muhimu.Pale wasimamizi wetu wanakuwa Waadilifu
 
Huyu mgombea urais alinifurahisha kipindi cha kampeni alikuja huku kwetu Mwanza, akalala ka hotel Fulani hivi kanaitwa PK halafu kampeni alifanya sehemu moja hivi nje ya mji BUSWELU, hakuwa na makuu mzee wa watu
 
Natamani nipate audio yake,huyu mzee huwa ana ka msisitizo Fulani hivi
 
Tuambie uliko tuwatume takukuru....haiwezekani watu tunatembea na mabakuli ya bati kama tuko boarding halafu wewe unakula bata mpaka Kuku wanalalamika Mulhat Mpunga
 
Back
Top Bottom