Hashim Rungwe Sipunda: Huyu mnayemuita fisadi si mumkamate au nyie waongo?

Ndo maana nasema huyo Rungwe binafsi amenifurahisha sana kwani yeye kama Mpinzani amekiri kwamba Serikali ya CCM imefanya makubwa sana nchi hii na ameyeorodhesha kinyume na baadhi ya watu wanavyopotosha kwamba CCM haijafanya chochote miaka 50 ya Uhuru, kuhusu Awamu ya V sijawahi kusikia yoyote akisema Serikali ya CCM ya Awamu V haijafanya chochote hata raisi Magufuli mara nyingi sana amesema Mzee Kikwete na Serikali yake wamefanya kazi kubwa sana muacheni apumzike!

Hebu mjibu basi na hiyo hoja ya Rungwe kwamba magu nashindwa kumkamata Lowasa pamoja na kuwa na jeshi na mahakama maalum ya mafisadi...

Nasubiri jibu lako mkuu au kada yoyote
 
Hakuna namna awamu hii kufanya hata nusu tu ya alofanya kikwete. Itabaki maneno tu. Nikiangalia
Dart mwendokasi
Uwanja nyerere inter 3
Bara bara 60% ya nchi
Chuo kikuu muhimbili Mkomanzi
UDOM
Flyover ubungo
Flyover Tazara
Heart Institute muhimbili
Barabara ya kisasa mbezi bahari beach
Songwe airport mbeya
MOI 2 muhimbili
School za secondary kila kata
Heshma kimataifa
Uhuru wa bunge
Uhuru wa kukosoa
Kunterezi 1 and 2 umeme wa gas
Upanuzi hospital za temeke mwananyamala
Ujenzi wa nyumba na NHC
Miradi mikubwa ya nyumba ya NSSF
Daraja la Kigambini
Miradi mikubwa kama bandari kubwa ya bagamoyo
EPZ ya mkapa
Fedha na biashara kukua siku hadi siku
Imani ya wawekezaji
Ukuaji wa viwanda binafsi mfano Azam juice nk
University kibao zaid ya 30

Sidhani kama haya tutayafika ....

Halafu yote hayo yakiwezekana bila ya
Kutukana wala kukejeli watu, Kufoka foka Jukwaani na wala Mzee Mwenyewe pia hakujinyima kula Bata Duniani

Maisha ni Kama Kioo ukicheka nayo yanacheka
 
Hoja ya Mzee Rungwe imejikita kwenye nadharia kuwa nchi ilipinda. Yeah, ukitazama kwa ualhalisia, mzee awam ya nne ameacha Legacy, leo Dar ina mambo mengi ya kisasa, majengo,BRT,Daraja la Kisasa na la kipekee, kila binadam ana mapungufu yake. Kipekee nasema awam iliyopita ilijitahidi, ilipasa kuendelea pale tulipoishia na kusonga mbele, ila kuwa awamu iliyopita ni kama haikuacha legacy bali ni kupinda tu, hapo hapana.

Tatizo lao wamechukua ya kijinga wameacha mazuri yote kapuni
 
Sijui waswahili tuna laana ya wapi. Hivi hii nchi maendeleo yake hupimwa kwa mifano aliyoitoa Rungwe? Kuwa Kariakoo inang'aa? Kuwa barabara zote lami? Kuwa university ziko zaidi ya 40? Kuwa viwanja vya ndege vinapanuliwa? Kuwa kuna mwendo kasi? Ndio vipimo vya maendeleo hivyo?

Hivi ukubwa wa kiwanja cha ndege unanisaidiaje mimi mwananchi wa kawaida ikiwa watalii na wafanyabiashara wa kimataifa wanatumia viwanja hivyo kutorosha nyara za serikali na kupitisha dawa za kulevya?

Hivi maghorofa ya kariakoo yaking'aa yanisaidia nini mimi mwananchi wa kawaida ikiwa wafanya biashara hao wanatoa rushwa na kukwepa kodi hivyo kuwa na faida mara dufu?

Hivi bara bara za lami zikiwa nchi nzima kwanini reli nayo isifanye kazi ya kusafirisha mizigo mizito kutoka pwani kwenda bara ili bei ziwe nafuu na barabara zidumu kuepusha gharama kubwa ya matengenezo ya barabara hizo kwa fedha ninayolipa kodi? Reli ilifia wapi? Mbona yenyewe haing'ai?

Hivi kuwa na vyuo vikuu 40 vibavyojazwa na watu wasio na sifa mpaka elimu inalazimishwa kuonekana nzuri wakati ni hovyo kwa kuweka mpaka division 5? Graduated wanaotoka katika vyuo hivyo 40 wanaenda wapi? Kuna mazingira ya ajira hata kujiajiri?

Mwendo kasi unamsaidia nini mwananchi wa Bunda?

Hivi hali ya huduma za afya mahospitalini Rungwe anaijua vizuri?? Hata sasa kaangalie huduma hata Bugando uone zilivyo mbovu (mbovu).

Majibu gani Rungwe ajibiwe? Kusoma hamjui hata picha?
Kwa hiyo kwako wewe Dar ya enzi za mzizima ni bora kwako? Kariakoo ya mwaka 2000 unataka ibaki kama ilivyokuwa? Wewe huoni ushindani wa miji yetu kwa wenzetu Kenya angalau tunaweza kujivunia? Wewe kwako usafiri ulioboreshwa wa BRT hujivunii? Wewe daraja la mfano la Kigamboni hujivunii? Wewe NHC ilivyowekeza hadi mikoan huoni sifa japo kidogo? Huwez kupongeza awamu iliyopita kwa mambo hayo bali utaona hakuna legacy kabisa?
Hatuwez kufika popote kwa fikra za ujima. Pale palipotokeza dosari parekebishwe tusonge, lakini ukweli usemwe, awamu ya nne imejitahid,nchi imejengwa kwa mifano hai. Ukienda Arusha kuna majengo ya NSSF mazuri yamependezesha mji, kuna mradi wa kukuza miji(Tanzania Stategic Cities) ambapo miji 7 ilinufaika yaani Mbey, Tanga, Mtwara, Kigoma, Dodoma, Arusha na Mwanza ni kutoka world bank baada ya lobbying. Dar es Salaam imejengwa hasa yaani imeweza kuleta ushindani na miji kama Nairobi. Hayo mambo lazima tujivunie, makosa yapo lakini yakipimwa kwa mizania, bado mazuri yanazidi.
Mimi binafsi naona miundombinu imejengwa sana awamu iliyopita, kinachotakiwa ni kuendeleza mazuri, lakini siyo kusema kupinda, haijakaa vema kabisa. Ikiwa kila awamu utaona awam ya nyuma yake imepinda, haina afya kwa kweli.
 
Mimi namjibu kwa haraka na urahisi kabisa kwamba yote aliyoyataja ambayo ni mambo mazuri kabisa kufanywa na Serikali ya CCM, yamefanyika kwa kipindi cha miaka 10 pamoja na Awamu nyingine zilizopita yaani II na ya III, hivyo kutegemea kwamba ndani ya Mwaka I Awamu ya V ifanye mengi zaidi ya Awamu tatu zilizopita ni ujinga na kwanza hakuna mashindano kwani wote ni Viongozi wa CCM na wanatekeleza Ilani za CCM!

Ila nimefurahia kwamba Upinzani wamekubali kwamba CCM imefanya makubwa Tanzania kinyume na wengine ambao husema kwamba miaka 50 hakuna kilichofanyika, hivyo nimefurahi kwamba mme bow down kwamba Nchi yetu inasonga mbele tena kwa kasi ya ajabu kama Mpinzani alivyosema!
Sio bure hizo ni laana tu ulizorithi na utakufa masikini
 
Wana JF, Hivi kweli maoni ya mtu kama huyu nayo yanaletwa JF! hajui hata Universities zilikuwaje miaka 10 iliyopita halafu naye eti alitaka kuwa rais!
Mbona sawo tu hata wengine hawajui kuwa kuna nchi huko duniani zinawajengea nyumba wananchi wao wanapofikwa na majanga ya tabianchi
 
hivi huyu Mzee si ndo aliwadanganya wananchi atawaletea maji kwa Ndege !? hahahahaha..
 
Mzee Hashim rungwe spunda naomba ukagombee ukocha wa taifa stars maana mkwasa kaachia ngazi
 
972d61c90a6e945d3a3e799664e50637.jpg
 
Kila Awamu inayoingia inaona hivyo, Awamu ya II ya Mzee Mwinyi iliona kuwa ya I sehemu kubwa ilishindwa na kuanza kufungua nchi, Awamu ya III Mzee Mkapa aliona Mzee ambaye tulimuita Mzee Ruksa aliachia sana uchumi na kuanza kurekekebisha, ya IV Mzee Kikwete vivyo hivyo alirekebsha ya Mzee Mkapa na sasa ya V vivyo hivyo wanaona kuna baadhi ya mambo yalikuwa hayafanyiki sawa na ni lazima yarekebishwe! Kwanza unaweza kusema hata Awamu ya I Mlm.Nyerere aliona Mkoloni alikosea mengi pia na kuanza kurekebisha na kufanya tofauti, hivyo ni kawaida sana!
Kama kila anayekuja anakuja kumsahihisha mwenzie huwezi kuona kwamba kila uongozi unabolonga?
 
Uelewa wangu wa Awamu ya I siyo mzuri sana, hivyo zaidi ya kusikia kwa watu siwezi kuuhukumu sana, ila kuanzia II-V ninaelewa vizuri sana tu!
Mbona huwa unamfananisha ndugu nyerere na mtukufu magufuli?
 
Sio bure hizo ni laana tu ulizorithi na utakufa masikini

Kwako wewe ni laana kukiri kuwa awamu zote viongozi wametoka CCM ila ni Baraka kwako kwa kuzishindanisha awamu ya nne na ya tano? ni Baraka Zaidi kulinganisha uongozi wa miaka 10 na uongozi wa mwaka mmoja?

JPM hawezi na hapaswi kumpuuza JK,maana bila JK mgombea aliyekimbilia CHADEMA angekuwa mgombea wa CCM na walalamikaji wasingekosa cha kusema.

Kwa msingi huu tu viongozi hawa wawili huwezi kuwagombanisha.Yanayoendela ni kusahihisha palipokosewa.
 
huyu mzee ukimsikiliza utatamani umsikilize siku nzima haishiwi maneno huyu, Rungwe at his best...
 
Hakuna namna awamu hii kufanya hata nusu tu ya alofanya kikwete. Itabaki maneno tu. Nikiangalia
Dart mwendokasi
Uwanja nyerere inter 3
Bara bara 60% ya nchi
Chuo kikuu muhimbili Mkomanzi
UDOM
Flyover ubungo
Flyover Tazara
Heart Institute muhimbili
Barabara ya kisasa mbezi bahari beach
Songwe airport mbeya
MOI 2 muhimbili
School za secondary kila kata
Heshma kimataifa
Uhuru wa bunge
Uhuru wa kukosoa
Kunterezi 1 and 2 umeme wa gas
Upanuzi hospital za temeke mwananyamala
Ujenzi wa nyumba na NHC
Miradi mikubwa ya nyumba ya NSSF
Daraja la Kigambini
Miradi mikubwa kama bandari kubwa ya bagamoyo
EPZ ya mkapa
Fedha na biashara kukua siku hadi siku
Imani ya wawekezaji
Ukuaji wa viwanda binafsi mfano Azam juice nk
University kibao zaid ya 30

Sidhani kama haya tutayafika ....
Na bado watu walikuwa wanapiga dili na jk anakula bata. Mjomba yeye story nyingi kazi hamna.mipasho ya ukubwani
 
Kwa hiyo kwako wewe Dar ya enzi za mzizima ni bora kwako? Kariakoo ya mwaka 2000 unataka ibaki kama ilivyokuwa? Wewe huoni ushindani wa miji yetu kwa wenzetu Kenya angalau tunaweza kujivunia? Wewe kwako usafiri ulioboreshwa wa BRT hujivunii? Wewe daraja la mfano la Kigamboni hujivunii? Wewe NHC ilivyowekeza hadi mikoan huoni sifa japo kidogo? Huwez kupongeza awamu iliyopita kwa mambo hayo bali utaona hakuna legacy kabisa?
Hatuwez kufika popote kwa fikra za ujima. Pale palipotokeza dosari parekebishwe tusonge, lakini ukweli usemwe, awamu ya nne imejitahid,nchi imejengwa kwa mifano hai. Ukienda Arusha kuna majengo ya NSSF mazuri yamependezesha mji, kuna mradi wa kukuza miji(Tanzania Stategic Cities) ambapo miji 7 ilinufaika yaani Mbey, Tanga, Mtwara, Kigoma, Dodoma, Arusha na Mwanza ni kutoka world bank baada ya lobbying. Dar es Salaam imejengwa hasa yaani imeweza kuleta ushindani na miji kama Nairobi. Hayo mambo lazima tujivunie, makosa yapo lakini yakipimwa kwa mizania, bado mazuri yanazidi.
Mimi binafsi naona miundombinu imejengwa sana awamu iliyopita, kinachotakiwa ni kuendeleza mazuri, lakini siyo kusema kupinda, haijakaa vema kabisa. Ikiwa kila awamu utaona awam ya nyuma yake imepinda, haina afya kwa kweli.

Suala sio awamu. Suala ni maendeleo, kipimo chake ni nini? Ni majengo na barabara?
 
Kama kila anayekuja anakuja kumsahihisha mwenzie huwezi kuona kwamba kila uongozi unabolonga?

Ni kawaida hiyo na hutokea Dunia nzima, ni hulka ya Binadamu, leo hii D.Trump amesema akiingia siku ya kwanza Januari 20. anafuta Obama care, sasa hvi tayari Chama cha Republican wameshaanza kushugulikia kufuta Obama care, pamoja na kufuta vikwazo vya Kiuchumi ambavyo Obama aliiwekea Urusi, na mambo mengine mengi ambayo Obama na Uongozi wake walifanya D.Trump amesema atabadilisha kama siyo kuyafuta kabisa, sasa unajua ni kwa nini Trump anafanya hivi?
 
Back
Top Bottom