Hashim Rungwe ataka serikali isitumie nguvu Kibiti, Rufiji

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,873
Aliyekuwa mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma ) katika uchaguzi Mkuu wa mwka 2015, Hshim Rungwe ameitaka serikali kutumia busara zaidi kuliko nguvu katika kumaliza tatizo la mauaji ya watu yanayoendelea mkoani pwani.

Mpaka saa zaidi ya watu 35, wakiwamo viongozi na askari wa Jeshi la Polisi, wameshauawa katika Wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga.

Siku chache zilizopita katika mahojiano maalumu na Rungwe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama chake na wakili wa kujitegemea alisema serikali inapaswa kukaa na waziri wa maeneo ambayo mauaji huwa hutokea ili kutafakali historia ya maisha ya waliouawa.

“Mauaji ya Pwani yanasikitisha na yanaacha hofu miongoni mwa watu . ukiyatanzama ni kama ya visasi kwani ungekuwa ni ujambazi wa kawaida watu hao wangekuwa wanaiba chochote . lakini wao shida yao ni kuua tu,” alisema Rugwe.

Alisema tatizo la Kibiti halitadhibitiwa kwa kuazisha kanda maalumu ya kipolisi, bali ni kujua kwanini watu wanauawa na kisha serikali ishughulikie sababu hizo na si kushughulika na wauaji tu.

“mauaji ya chuki na visasi ni mabaya, ndiyo yanayoisumbua Israel, unakuta watu wengine wanalipiza kwa walichofanyiwa na ndugu zao.

Ndiyo maana ninasema wale ambao ndugu zao wameuawa waulizwe maisha na mahusiano ya hao marehemu na watu wengine yalikuwaje, majibu yatakayotolewa ndicho chanzo cha mauaji,” alisema Rungwe.
 
Mbabe magufuli hawezi kukubali ushauri kama huo,mwisho wa siku atasemakua na Watakiona cha mtemakuni.alafu kesho wanaendelea na mauaji.
 
Lakini pia waangalie kama swala la kuminywa haki za watu iwe kisiasa au kijamii huwa zina ibua chuki za namna hii na hata kupelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe
 
pia wajaribu ku-address masuala yafuatayo (inaweza kuwa hakuna uhusiano, but who knows)...

- kuna watu walishapata shubiri Mtwara kwa ajili ya gesi wakati ule wote mtakuwa mnakumbuka
- kuna watu bado wana kinyongo kutokana na figisu za October 2015 kule Zanzibar
- nk
 
Lakini pia waangalie kama swala la kuminywa haki za watu iwe kisiasa au kijamii huwa zina ibua chuki za namna hii na hata kupelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe
Pale sio kuminywa lengo ni kuanzisha eneo la dola ya kiislamu Ya siasa kali ambayo itakuwa chini Ya kundi la kigaidi. Wamelichagua hilo eneo Kama lao la kuendeshea operation zao kutokana na eneo kuwa na misitu mingi. Hiyo mbinu Ya hit and run to the Forest inatumiwa sana Na magaidi na majeshi ya waasi. Hao huhitaji kuongea nao lugha wanayoijua ni risasi tu. Sana nashauri waganga wa jadi wa uchawi wa k.ivita washirikishwe kwenye hii Vita na wataalamu wa Uchawi walioko polisi na JWTZ wapewe nafasi ya kuutumia.kova apelekwe kibiti aongoze vikosi
 
Jambo hili linataka watu wenye busara kama JK hapo litaisha fasta.
Serikali impeleke kamanda Ahmed msangi au mzee mstaafu kamanda kova wampe mkataba aongoze mapambano tuone Kama wataendelea kufurukuta wote watahama nchi tena uchi
 
SPUNDA KAFUMBUA FUMBO ALIPOSEMA HIVI NANUKUU

"Ndiyo maana ninasema wale ambao ndugu zao wameuawa waulizwe maisha na mahusiano ya hao marehemu na watu wengine yalikuwaje, majibu yatakayotolewa ndicho chanzo cha mauaji,”

Maana yake ni kwamba ndugu wa Marehemu waulizwe
1. Kama Marehemu alikuwa na ugomvi na mtu yoyote
2. Kama Marehemu alikuwa ana wasiwasi na mtu yoyote
3. Marafiki wa Marehemu ni akina nani (maana adui anaweza kuwa yuko karibu yako)
4. marehemu alionana na nani siku hiyo, ni nani mtu wa mwisho marehemu kukutana naye siku hiyo
5. Je kuna mtu aliyekuwa anakuja mara kwa mara kwa marehemu siku kadhaa kabla ya marehemu kufariki, ni nani?
6. Je Marehemu amewahi kufanya lipi baya hata kama limesahaulika na alimfanyia nani?

Spunda kafumbua fumbo:
 
Pale sio kuminywa lengo ni kuanzisha eneo la dola ya kiislamu Ya siasa kali ambayo itakuwa chini Ya kundi la kigaidi. Wamelichagua hilo eneo Kama lao la kuendeshea operation zao kutokana na eneo kuwa na misitu mingi. Hiyo mbinu Ya hit and run to the Forest inatumiwa sana Na magaidi na majeshi ya waasi. Hao huhitaji kuongea nao lugha wanayoijua ni risasi tu. Sana nashauri waganga wa jadi wa uchawi wa k.ivita washirikishwe kwenye hii Vita na wataalamu wa Uchawi walioko polisi na JWTZ wapewe nafasi ya kuutumia.kova apelekwe kibiti aongoze vikosi
sasa kwanini na waislam wanauwawa kama unadai ni mauaji ya kidini? mimi naona washirikishwe vya kutosha wananchi wa maeneo uhusika kukomesha umwagikaji huu wa damu.
 
Somalia wote ni waislamu lakini boko haramu wanawachinja waislamu wenzao kila siku kisa sio wa itikadi kali wenzao. Hayo makundi ya kigaidi ya itikadi kali kwao mtu yeyote asiye itikadi kali kwao ni kafiri. Waislamu waliouawa sio wa itikadi kali
 
Pale sio kuminywa lengo ni kuanzisha eneo la dola ya kiislamu Ya siasa kali ambayo itakuwa chini Ya kundi la kigaidi. Wamelichagua hilo eneo Kama lao la kuendeshea operation zao kutokana na eneo kuwa na misitu mingi. Hiyo mbinu Ya hit and run to the Forest inatumiwa sana Na magaidi na majeshi ya waasi. Hao huhitaji kuongea nao lugha wanayoijua ni risasi tu. Sana nashauri waganga wa jadi wa uchawi wa k.ivita washirikishwe kwenye hii Vita na wataalamu wa Uchawi walioko polisi na JWTZ wapewe nafasi ya kuutumia.kova apelekwe kibiti aongoze vikosi
Waisilamu wangapi wameuwawa hadi sasa?
 
Back
Top Bottom