Hasara zinazosababishwa na umeme wa TANESCO tupeleke wapi madai ?

Hhm

Member
Apr 28, 2010
69
14
Wana JF salaam, naomba nipate mchango wa mawazo juu ya hili. Umeme wa Tanesco sasa umekuwa ni umeme usiyo salama tena kufuatilia hasara mbalimbali tunazozipata kutokana na kupungua au kuongezeka kwa nguvu ya nishati hii.

Hasara hizi ni kama kuunguliwa na tv set, home theater, fridge na vitu vingene vinavyotumia nishati hii.

Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi mimi kama mtumiaji ninapopata hasara ya namna hii ninalindwa na kifungu kipi cha cheria ya mashirika yanayotoa huduma kwa jamii , nauliza hivi kwa faida ya watanzania wenzangu.

Home apliences ni vitu vya gharama na ni vyema kufahamu tunafanyaje endapo haya yanatokea.
 
Jibu mbona jepesi sana mkuu! Hasira zetu tuzipeleke kwenye sanduku la kura 2015 kwa kuipumzisha govmnt nzima ya chama tawala. After that,mfumo mzima wa utendaji katka govmnt,taasisi na mashirika ya uma uta change pia. Hapo tutakuwa tumepata ufumbuzi wa kudum wa watatizo ya kina Dowans na mpwa wake Iptl
 
Tumia fridge guard, tv guard ambavyo uwa vinarekebisha umeme kabla haujafika kwenye jokofu au runinga vinginevyo uwafungulie kesi ya madai.
 
kusubiri uchaguzi 2015 ndio mabadiliko ya siasa yaweze kuleta suluhu ktk tatizo la umeme hapo ni kulea ugonjwa wkt mgonjwa yupo ICU.
mpango: ni kufumua uongozi wote kuanzia bodi, kurugenz hadi uongoz wa vituo vya umeme.
kuunda mamlaka ya usimamiz wa vyanzo vya uzalishaji umeme. tanesco ibaki ktk usambazaji na uuzaji.
serikali isitoe ruzuku ktk gharama za uendeshaji bali ruzuku ziwe za manunuzi ya mitambo tu.
kubadili umiliki wa kampuni kutoka kwa serikali(100%) na kuwa hisa za wananchi(45%), serikali(35%) na mashirika mengine ya umma(20%).
yote hayo yanaweza kufanyika endapo kukiwa na mabadiliko ya sera na sheria
 
Back
Top Bottom