Uchunguzi wa muda mfupi, tuseme uchunguzi binafsi umeonyesha wale viongozi wanaopita bila ya ridhaa za wananchi au wameshinda uchaguzi kwa njia za udanganyifu uliotokana na wao au tume ya Uchaguzi, viongozi hao hawana maadili mazuri na kazi zao na maendeleo yao binafsi huonekana muda mfupi tu baada ya kuanza kuzoea mazingira.
Viongozi wanaoingia kwa njia hizi kuanzia raisi mpaka anaefagia njia, huingia kazini kwa makeke na majigambo makubwa sana kiasi ya kuwakubalisha wananchi kuwa sasa tutaendelea lakini wapi baada ya mwaka tu tamaa ya maendeleo kwa wananchi inaanza kuondoka na hatimae hukatika kabisa. Na badala yake wale wavukishwa daraja wanazidi jeuri na kuanza kumiliki mali magari na majumba makubwa tu, hilo liweke kando.
Kasi ya uwajibikaji huondoka yale majigambo huzima mfano hai ni Zanzibar, sasa serikali inaelekea kushindwa na ile kasi yake haipo imeanza kutoweka, leo hii Zanzibar inaongoza kwa uchafu kuanzia mijini, vijijini hata mashamba ni uchafu kwa kwenda mbele, wale waliokodiwa kutoka Tanganyika kazi imashinda haijulikani wapo wapi na yule Waziri inaonekana yupo kimya kama alieambia Nyamaza na tulia.
Nadharia ya yajayo nafurahisha sasa inaonekana wazi kabisa yajayo yanakirihisha.