Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Ukijiamini, mambo yako yanakuwa safi.....
Wanasema kila jambo lina hasara na faida zake. Kutojiamini faida yake kubwa ni kujificha mahali ambapo kila mtu anakuona na kuamini kwamba, umejificha, ni kupata nafuu ya muda kutoka katika kuhisi kutokamilika.
Zifuatazo hapa chini ni hasara za kutojiamini:
Ni vyema kuzikagua hasara hizi kwa sababu, huenda tayari nawe umezipata kiasi cha kutosha.
1. Kukosa usalama kuhusu wewe na kukosa imani dhidi yako. Huamini kama una thamani, utahisi vipi kuwa salama na utakuwa vipi na imani kwako mwenyewe? Siyo rahisi.
2. Kushindwa kuwa wazi na kushindwa na kushindwa kuwaamini wengine. Kama hujiamini, utaweza vipi kuwaamini wengine?ni vigumu, haiwezekani!
3. Kushindwa kufanya maamuzi au kukwama mahali pengi. Mtu asiyejiamini, bila mwenyewe kujua, hukwama kwenye maeneo mengi sana kutokana na kuhemkwa haraka. Kukata tamaa mapema na kufanya mambo kwa kutazama nje, badala ya kujitazama mwenyewe.
4. Kuwa na wasiwasi muda wote na kukosa amani na utulivu. Nilisema majuto ya jana na hofu za kesho hutawala sana kwa asiyejiamini na kutoa maumivu.
5. Kukabiliwa na ugumu wa uhusiano na wengine. Kwa mtu asiyejiamini kuishi naye ni sawa na kuishi na glasi.
6. Kushindwa kudhibiti mihemko mibaya na hata kuuguaugua. Hii inatokana na kufikia mahali ambapo mtu huendeshwa na ushindani na haja ya kuwa sahihi muda wote.
7. Kuogopa kukataliwa na kutojaliwa na hivyo kuwa mtumwa wa watu. Wasiojiamini hawawezi kusimama wenyewe kama binadamu kamili. Mtu ananyanyaswa katika uhusiano lakini yumo tu anang'ang'ania uhusiano huo mpaka unamletea maradhi yatakayompeleka kaburini mapema.
8. Kuumia kwa kutojua kwamba, inatosha, hasa linapokuja suala la kuishi kwa kujilinganisha, na ushindani. Hata awe na mafanikio kiasi gani, asiyejiamini hawezi kuyaona na kuyafaidi.
9. Kukabiliwa na sononi, kukosa furaha na kuhisi kutojitosha.
10. Kujitenga na kuhisi unyonge kwa watu. Hii ni hali ya kukaa kipwekepweke au kama wanavyoita ‘kiyatima.'
11. Kujifungia kwenye tabia kwa njia ya usugu. Tabia kama kunywa pombe, kufanya mapenzi sana, kucheza kamarim na kutafuta fedha kihamnazo…
12. Kushindwa kuona upande wa mzaha wa maisha. Mtu anakuwa kila wakati katika udhati (serious) hadi inamfikisha kuugua….
13. Kukataa kuwa, mtu ana matatizo na kuyaondoa, badala yake kukandamiza. Unajifanya uko safi, kumbe una maumivu makali moyoni.
14. Kujionyesha nje kwamba, mambo safi wakati mtui anahitaji msaada, yaani ana matatizo mengi tu lakini anavyojifaragua kama vile hana tatizo hata moja, kumbe moyoni ni kiama kitupu.
Rejea makala hii kama hukuisoma:
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/453126-kama-una-dalili-hizi-basi-jua-kwamba-hujiamini%85.html