Hasara za kutojiamini, hizi hapa…..

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
career-woman.jpg

Ukijiamini, mambo yako yanakuwa safi.....

Wanasema kila jambo lina hasara na faida zake. Kutojiamini faida yake kubwa ni kujificha mahali ambapo kila mtu anakuona na kuamini kwamba, umejificha, ni kupata nafuu ya muda kutoka katika kuhisi kutokamilika.

Zifuatazo hapa chini ni hasara za kutojiamini:

Ni vyema kuzikagua hasara hizi kwa sababu, huenda tayari nawe umezipata kiasi cha kutosha.

1. Kukosa usalama kuhusu wewe na kukosa imani dhidi yako. Huamini kama una thamani, utahisi vipi kuwa salama na utakuwa vipi na imani kwako mwenyewe? Siyo rahisi.

2. Kushindwa kuwa wazi na kushindwa na kushindwa kuwaamini wengine. Kama hujiamini, utaweza vipi kuwaamini wengine?ni vigumu, haiwezekani!

3. Kushindwa kufanya maamuzi au kukwama mahali pengi. Mtu asiyejiamini, bila mwenyewe kujua, hukwama kwenye maeneo mengi sana kutokana na kuhemkwa haraka. Kukata tamaa mapema na kufanya mambo kwa kutazama nje, badala ya kujitazama mwenyewe.

4. Kuwa na wasiwasi muda wote na kukosa amani na utulivu. Nilisema majuto ya jana na hofu za kesho hutawala sana kwa asiyejiamini na kutoa maumivu.

5. Kukabiliwa na ugumu wa uhusiano na wengine. Kwa mtu asiyejiamini kuishi naye ni sawa na kuishi na glasi.

6. Kushindwa kudhibiti mihemko mibaya na hata kuuguaugua. Hii inatokana na kufikia mahali ambapo mtu huendeshwa na ushindani na haja ya kuwa sahihi muda wote.

7. Kuogopa kukataliwa na kutojaliwa na hivyo kuwa mtumwa wa watu. Wasiojiamini hawawezi kusimama wenyewe kama binadamu kamili. Mtu ananyanyaswa katika uhusiano lakini yumo tu anang'ang'ania uhusiano huo mpaka unamletea maradhi yatakayompeleka kaburini mapema.

8. Kuumia kwa kutojua kwamba, inatosha, hasa linapokuja suala la kuishi kwa kujilinganisha, na ushindani. Hata awe na mafanikio kiasi gani, asiyejiamini hawezi kuyaona na kuyafaidi.

9. Kukabiliwa na sononi, kukosa furaha na kuhisi kutojitosha.

10. Kujitenga na kuhisi unyonge kwa watu. Hii ni hali ya kukaa kipwekepweke au kama wanavyoita ‘kiyatima.'

11. Kujifungia kwenye tabia kwa njia ya usugu. Tabia kama kunywa pombe, kufanya mapenzi sana, kucheza kamarim na kutafuta fedha kihamnazo…

12. Kushindwa kuona upande wa mzaha wa maisha. Mtu anakuwa kila wakati katika udhati (serious) hadi inamfikisha kuugua….

13. Kukataa kuwa, mtu ana matatizo na kuyaondoa, badala yake kukandamiza. Unajifanya uko safi, kumbe una maumivu makali moyoni.

14. Kujionyesha nje kwamba, mambo safi wakati mtui anahitaji msaada, yaani ana matatizo mengi tu lakini anavyojifaragua kama vile hana tatizo hata moja, kumbe moyoni ni kiama kitupu.

Rejea makala hii kama hukuisoma:

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/453126-kama-una-dalili-hizi-basi-jua-kwamba-hujiamini%85.html
 
Unachosema ndg yangu Mtambuzi ni kweli kabisa, Kwa wale walioko maofisini, watu wasiojimini hata performance zao za kazini hushuka sana! wanakuwa nin watu wasioweza kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.
 
Last edited by a moderator:
kweli unayosema ni sahiihi sana kwani wako watu ambao hawajiamini 100% na wengi wanaoumwa maradhi nyakati hizi ni wale wasiojiamini hata katika mambo yao binafsi na hususani wale walioko kwenye ndoa ndo kabisaaaaaaa hawajiamini wala kuwaamini wale waliowazunguka
 
shem Mtambuzi asante kwa kutuwekea kioo tujiangalie, lol!
hiyo namba 12 inanitesa sana kwa watu wa jirani zangu. Mimi napenda sana utani, yaani mambo mengi out of kazi/shule/ugonjwa/......huwa nayachukulia utani. ingawa sometimes hata ugonjwa huwa natania. Binafsi nikiwa naumwa sipendi mtu aje aniangalie akiwa amekunja sura, hata kama nipo serious namna gani, napenda anitanie nichekeeee, ndo naona napata nafuu.
sasa kuna baadhi ya watu wananitesa sana, sipati angle za kuwatania.... kila nikitania, tayari nimeshanuniwa...... "unaona sababu wewe uko hivi au vile".... na vitu kama hivyo. Inawezekana kweli hawajiamini au? mi sijui bana
 
ha haaaa, hili somo mimi nimepata sufuri.......
husband akiamua kutoka na watu wanaonizunguka ni ujinga wake mwenyewe, na hilo halinihusu kabisaaaaaaaa........ na wala sitajisikia vibaya eti nimesababisha afanye hivyo
 
Mie nadhani nina tatizo la kutoelezea shida zangu kwa watu hovyo

Sipendi, siamini kama naweza saidiwa na wengine kuliko navyoweza jisaidia mwenyewe
Labda siblings au mzazi ndio naweza mwambia lakini wengine, hell no
Hata kama nalala njaa nitakunywa uji, kutangaza shida siwezi kabisa

shem Mtambuzi asante kwa kutuwekea kioo tujiangalie, lol!
hiyo namba 12 inanitesa sana kwa watu wa jirani zangu. Mimi napenda sana utani, yaani mambo mengi out of kazi/shule/ugonjwa/......huwa nayachukulia utani. ingawa sometimes hata ugonjwa huwa natania. Binafsi nikiwa naumwa sipendi mtu aje aniangalie akiwa amekunja sura, hata kama nipo serious namna gani, napenda anitanie nichekeeee, ndo naona napata nafuu.
sasa kuna baadhi ya watu wananitesa sana, sipati angle za kuwatania.... kila nikitania, tayari nimeshanuniwa...... "unaona sababu wewe uko hivi au vile".... na vitu kama hivyo. Inawezekana kweli hawajiamini au? mi sijui bana
 
Naangalia kwa karibu, naona wachangiaji wote "wanajiamini"; tusiojiamini tunapita tu bila kucomment au wanaodhani wanajiamini nao wamo kwenye kundi letu?
Past post za wengi humu naona tuko nao kundi moja tu. Lol
Ruksa kunipopoa!
 
Nisaidia kuandamana

Maandamano yataanzia Buguruni kwa mnyamani, kupitia sarender briji, then bibi titi afu Uwanja wa Mnazi mmoja

Yatapokelewa na Mkuu wa mod mkuu na risala nitasoma mwenyewe
Nachagua adhabu ya ban ya milele

unajua hata mimi nilishangaa rafiki.... nikajua umemruhusu....
mkomalie aitoe kabla hatujaandamana
 
Kuna hasara pia za kujiamini kupita kiasi? nadhani kunatakiwa kuwa na balance fulani katika kujiamini. Kutojiamini ni ugonjwa mbaya mno wa akili..nilikuwa nao nilipokuwa nakua na hadi sasa kuna baadhi ya maeneo nahisi sijiamini hasa katika mahusiano ya mapenzi
 
Unakidhi 13 na 14?

Naangalia kwa karibu, naona wachangiaji wote "wanajiamini"; tusiojiamini tunapita tu bila kucomment au wanaodhani wanajiamini nao wamo kwenye kundi letu?
Past post za wengi humu naona tuko nao kundi moja tu. Lol
Ruksa kunipopoa!
 
Naangalia kwa karibu, naona wachangiaji wote "wanajiamini"; tusiojiamini tunapita tu bila kucomment au wanaodhani wanajiamini nao wamo kwenye kundi letu?
Past post za wengi humu naona tuko nao kundi moja tu. Lol
Ruksa kunipopoa!
ha haaa, siyo hivyo rafiki.
unajua unaweza kujiamini kwa hili na usijiamini kwa lile?
mdogo wangu ni mwl. ukiingia kwa darasa lake utampenda nda jinsi anavyomimina materials... kwa kujiamini haswaaaaa.
sasa mwambie Ombea chakula kwenye kusanyiko la watu kama 10 hivi..... hawezi kabisaaaa
 
Back
Top Bottom