Hasara ya COVID-19 kwa wakulima wa mazao ya bustani

Sep 25, 2018
27
20
Habari wanajamvi,

Je, kwa hali inayoendelea mnahisi kwa wakulima wa ndani ambao wanalima mazao ya bustani wameathirika au wanaathirika vipi kwa kipindi hiki na je, ikitokea lockdown itaathiri vipi mazao yao kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Elimu ya matunzo ya mazao shamba bado dogo na bado hakuna elimu kwa jamii kubwa ya Watanzania

2. Miundombinu haijafika kwa wahusika mfano cold rooms facilities, hiyo ni shida kubwa sana

3. Vyombo vya kusafirishia bidhaa vikifungwa kuna uelekeo au mbadala wa kuzoeza kupunguza hasara?

Sambamba na haya na tunaona soko la kimataifa lilivyoshake; je, tunaweza kulisha baadhi ya mataifa mengine hasa nchi za Ulaya. Je, nini kifanike kufikia lengo?
 
Mimi najikita mwisho kabisa hapo..Uwezo wa kulisha mataifa mengine tunao ikiwa kama uzalishaji utatutosheleza ndani pia..Lakini pia tumeona wiki iliyopita ndege yetu imesafirisha mazao ya mbogamboga kwenda ulaya..So yote yawezekana tusife moyo,,mahitaji bado makubwa nchi za wenzetu
 
Back
Top Bottom