Harusi zisiwe usumbufu, ukitaka kuoa kwa harusi kubwa wewe na familia yako mjipange kwanza vizuri

Huu utamaduni wa kuchangisha watu pesa wakati mtu anapooa huenda ulikuwepo tangu karne na sisi tukaurithi kutoka kwa babu zetu au kutoka kwa wakoloni wetu lakini kadri muda unavyoonda unageuka kuwa usumbufu mkubwa.

Fikiria mtu anatuma meseji kwenye WhatsApp group la harusi alilokuunganisha bila ridhaa yako, anatuma kwenye WhatsApp yako ya binafsi, anatuma pia texts za kawaida, zote hizo ujumbe ni mmoja kukumbusha kulipa mchango wa kijana wao ambao wakati mwingine hata haujatoa ahadi ya kuutoa!

Ukitaka harusi kubwa kadiria kulingana na kipato chako na cha familia yenu, wengine wa mbali wawe ni kujazia tu, epuka kuwapa watu usumbufu usio wa lazima.
Wewe changisha pesa, hilo ni jambo la kijamii, akina mengi mbona walichangisha?

Kuchangisha sio kusumbua watu bali kushirikisha watu. Na si lazima uchangiwe na wengi, huwezi simama mwenyewe kwenye mambo kama haya lazima uwe na jamii ambayo ni muhimu kwako.
 
Kuchangia harusi ni ujinga

Mm sintokuja eti kutoa laki au 70 au.50

ETI NIMUUNGE MKONO MSELA AKA GEGENDE, then 2yrs waaachana.

Upuuzi tu huo.

BORA NISAIDIE ADA ZA SHULE KWA WAHITAJI.
 
Imenikuta kwa jamaa tulisoma wote advance, last week kanitumia sms ya mchango bila hata salamu kana kwamba huwa tunaongea mara kwa mara. Mbaya zaidi kaniunga kwenye group la michango.

Sina shida na michango. Tatizo ni kukosa uungwana na utu.
Achana nae
 
Single 70,000 Double 80,000

Ukifika chakula sahani moja ambacho kinaweza kua kibaya vile vile hunywi bia na soda huwezi kunywa nyingi.

Tusione marafiki wanatongoza mashemeji zao utakuta jamaa kila akikokotoa anaona wazi pesa aliyotoa haijaisha bado.
Kumbe dah
 
Tunamuomba mheshimiwa Magufuli apige marufuku michango ya harusi....Hahahahahahah
 
Tunamuomba mheshimiwa Magufuli apige marufuku michango ya harusi....Hahahahahahah
 
Mkuu naomba nikazie pamoja na kero zote hizo baada ya miezi 6 au mwaka ndoa chali kila mtu na maisha yake vijana na ndoa za miemko bhana shida tupu
Inauma sana,unakuta jamaa alikudai mchango kwa fujo kama deni vile afu miezi 6 hakuna ndoa...hili inabidi serikali iingilie ili kila mtu apambane na hali yake
 
Hujamuelewa anasema uzi uwekwe juu kama hizo nyuzi nyingine huko za voda,nmb etc zenye kipini ili kila mmoja auone maana unaelimisha na una ujumbe mzuri
Kosa lake ni nini?.Mkuu unategemea kufunga Harusi nini?.Tulia dawa iingie ukitingishika tu utapata madhara makubwa.
 
Wapenda Harusi msiwe wakali na kuweni tu wakweli ! Tunajua hali tu ndo imebana na kuwa siyo! Hapo nyuma suala la Harusi na hasa Dar ilikuwa ndio habari ya mjini.

Dar kipindi cha nyuma kidogo hata kumpata mtu mkabadilishana mawazo ya maisha ilikuwa ni shida!
Mtu unakuta yuko busy na kamati kama 10 hivi za Harusi hana muda kabisa!

Na harusi nyingi ilikuwa ni fuata mkumbo na kutafuta pesa za chap chap!
Mtu anakuwa amechanga Harusi kama 10 mfululizo naye kwa hasira anaenda pale Corner Bar au Ambiance siku mbili naye anatangaza Harusi ! Anaanza kuchangisha watu pesa za harusi!

Hiyo ndo siri ya talaka nyingi kuongezeka leo Dar leo.
 
Kina jamaa yangu alifunga ndoa na harusi yake ilikuwa ya maskhara kwelikweli.
Asubuhi walitinga kwa Mkuu wa Wilaya, wakafunga harusi wakiwa watu Wanne tu, Bwana na Bibi harusi, Best Man na Woman wao. Wakatoka hapo wakapita kwenye supu baadae saa nne wapo mzigoni wanaendelea na kazi.
~No mchango.
~No sherehe.
~No honeymoon.
~No madeni.
~No lawama.
~Ndoa imefungwa na maisha yanaendelea!
 
Back
Top Bottom