Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,580
- 46,167
Huu utamaduni wa kuchangisha watu pesa wakati mtu anapooa huenda ulikuwepo tangu karne na sisi tukaurithi kutoka kwa babu zetu au kutoka kwa wakoloni wetu lakini kadri muda unavyoonda unageuka kuwa usumbufu mkubwa.
Fikiria mtu anatuma meseji kwenye WhatsApp group la harusi alilokuunganisha bila ridhaa yako, anatuma kwenye WhatsApp yako ya binafsi, anatuma pia texts za kawaida, zote hizo ujumbe ni mmoja kukumbusha kulipa mchango wa kijana wao ambao wakati mwingine hata haujatoa ahadi ya kuutoa!
Ukitaka harusi kubwa kadiria kulingana na kipato chako na cha familia yenu, wengine wa mbali wawe ni kujazia tu, epuka kuwapa watu usumbufu usio wa lazima.