Harusi za sasa chanzo cha mabibi harusi kuwa na mawazo/kukonda kupoteza mvuto

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Suala la harusi kwa sasa limekuwa likifanya mabibi harusi wengi kudhoofika miili yao na nyuso zao kupoteza mng'ao kwa mawazo ya kutaka masherehe makubwa.

Wengine wanaumwa mpaka vidonda ukimuuliza veepee!Anasema michango haijakamilika na sherehe imewadia.

Hii inapelekea hata siku ya sherehe mabibi harusi hawa kutokupendeza na wakati meingine kuwa kama vituko.

Wengine hata hawataki kuona picha zao za harusi..

Swali: Kwanini wanaume wao hawapati hayo?

Nawasilisha
 
Hao mabibi harusi wanaokusanya michango wenyewe badala ya kamati wanakua wameipania sana harusi na zawadi(wanapania sherehe sio maisha ya ndoa),ni kama wanataka shukran au kurudishiwa kiaina michango aliyowachangia shosti zake.

Kwa bwana harusi ni kimbembe wanakazi sana maana wao ndio wasimamiaji wakuu wa masuala ya bajeti yote ya harusi hadi kufikia kukopa kiasi kikubwa cha pesa ili tu bibi harusi afurahi,hapo bado hajaweka makazi sawa(kama kapanga)
 
Hivi ukiwa na harusi ni lazima upokee michango mikubwa?

Tulipofikia ni pabaya sana mtu anapopatwa na janga kama ajali ama maradhi unakuta mtu anatoa 20,000 lakini harusi anatoa kuanzia 200,000.

Kwani harusi haitabiriki kiasi cha kwamba mtu ahitaji mchango mkubwa kwa sababu imemkurupusha kama ajali?

Inafika mahali ukitaka kuoa jipange mwenyewe usitegemee sana michango turudi kwenye falsafa ya kila mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake.

Ukiona unategemea sana michango inamaana unajaribu ku-fake hadhi yako, hamna maana ya kuanza maisha ya ndoa na kwa ku-fake hadhi yako ilimradi ujionyeshe wewe ni wa hali ya juu.
 
Kwanza Siku hizi wanawake wengi wanapenda harusi lakini ndoa hawapendi
Pili wengi wanapenda kupania na kunuia makubwa kuliko uwezo wao!!mfano unakuta mtu anapiga budget ya make up sio chini ya milioni utaacha kudata kweli?hapo bado gauni doh!! Watu wakikugomea mchango ndo unaanza kukongoroka!!

Ushauri wa bure!!tujikune pale mkono unapofikia tuache show off za kijingaa!! Mwishowe utakondeana hadi wanja udundeee siku ya harusiiiii
 
Ukweli mtupu
 
Hili la kutokujitegemea katika mchango ndio chanzo kikuu
 
Kwanza Siku hizi wanawake wengi wanapenda harusi lakini ndoa hawapendi
Pili wengi wanapenda kupania na kunuia makubwa kuliko uwezo wao!!mfano unakuta mtu anapiga budget ya make up sio chini ya milioni utaacha kudata kweli?hapo bado gauni doh!! Watu wakikugomea mchango ndo unaanza kukongoroka!!

Ushauri wa bure!!tujikune pale mkono unapofikia tuache show off za kijingaa!! Mwishowe utakondeana hadi wanja udundeee siku ya harusiiiii
 
harusi kubwa?ulimbukeni tu kuna maisha baada ya harusi na wasijisahau kuwa lengo kuu ni ndoa sio kuuza sura kwa sherehe yakukata na shoka
Tatizo wao wanachojua ni siku ile moja..ndio maana ndoa za siku hizi ni ndoano
 
Back
Top Bottom