Harusi ya Maxence na Stella - Hongera kutoka JF

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,965
2,000
Nilikuwa nimepotea sana sikuwahi kuiona hii. Mac, niambie namna ya kukutumia mchango wangu kusaidia pilika hizi. Si mchango mkubwa lakini unaweza kusaidia kupata creti mbili, tatu za bia kwa wageni wako.
Mzee kichuguu nashukuru. Kama unataka kunitumia via Western Union unaweza kutumia jina hili la Maxence Melo Mubyazi au kama ni kwa njia ya kutumia credit/debit card naweza kukupa details in private.

Ahsante sana.

Mac
 

swaty

Member
May 20, 2008
8
0
Ama kweli waTanzania tusha kuwa taifa omba-omba, hata kwenye ndoa tunaomba-omba tuchangiane duhh. Tuwacheni haya jamani. Kwani mwenyewe alisema anataka kuoa kwa omba-omba?

Wewe kama unataka kumpa zawadi mpe kivyako-vyako sio upitishe UMATONYA.
Jamani sherehe ni watu na vitu kama hamna vitu kama vinywaji, na vyakula watu watasherehekeaje?? Hajawaomba mchango wa hela, hata mawazo yanatosha jameni. Kuoa inawezakuwa ni kufukuza ufuska. Mchangieni jamani achague moja.
Hongereeni wanaharusi. Tupeni ac no zenu au no za cm
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,951
2,000
Amefanya kitu cha maana sana vijana sote tuige mfano wa huyu...
Tupe taratibu za uchangiaji ili tuweze kufanikisha shughuli hii pevu........
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,965
2,000
Amefanya kitu cha maana sana vijana sote tuige mfano wa huyu...
Tupe taratibu za uchangiaji ili tuweze kufanikisha shughuli hii pevu........
Mkuu fidel80, unaweza kuwasiliana nami kwa njia ya barua pepe au kwa simu na details zaidi nakupa endapo unataka kunichangia hata mawazo kwani natambua kuwa naingia kwenye kundi jipya. Napenda maoni ya aina yoyote hata yale ya kunikatisha tamaa. Kwa kuniandikia barua pepe au kwa njia ya simu pia ni njia mbadala ya kunipa ushauri wa aina yoyote. Kama ni michango nitafurahi pia, lakini nitafurahi zaidi nikiwaona wana JF wote mpo siku ya tukio!
 

DMussa

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
1,314
1,500
Mac,
Tuko pamoja mkuu....
This is yet another milestone in your life.... God bless you brother!
 

Kipanga

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
678
0
wandugu kwani michango ni ya mahali au ndio mnataka kujazia kwenda kuzibua vifuniko???

Kama jamaa amekolea na mambo yote ya msingi amefanya nadhani tumshukuru kwa taarifa na kumtakia maisha mema mambo ya kutembezewa bakuri haijatulia kabisa....may be bwana harusi mtarajiwa atujuze huenda hana mpango wa kuchangiwa ila watu mnataka kuendekeza mazoea tu..Dar iko bomba mwanangu tulia...
 

TAIKUBWA

Senior Member
Jan 20, 2008
119
0
nawatakia maisha mema na msaidiane kule watoto
ndoa za sasa zimekuwa na matatizo mengi wengi wamekuwa wakifikiri swala la uaminifu tu ,,lakini kuna mambo mengine mwanamme na mwanamme mnatakiwa kujua hili.....nyumba ni kusaidiaana na wala si mwanaume ...na katika kusaidiana mwanaume bado anabaki kichwa cha familia na hata iweje mwanamke awezi kuwa kichwa cha familia..haya ni kutoka maandiko ya kitabu kitakatifu.... kaka Mac sina udhoefu wa ndoa ila najua ukichukua haya chini mungu akujalie nije kufurahi kwa amani ni uncles wangu....

1))JITAHIDI UWE MWAMINIFU KWA MKEO...JUA UKITOKA UMETOKA UKILAZIMISHA KURUDI UNAWEZA KUTUMBIKIA SHIMO LA CHOO N KUJUTA KWA UAM=UZI WAKO KUMBE ULIKUWA SAWA KUWA NA MWENZAKO....

2)))JITAHIDI KUWA MUWAZI KWA MAMBO MENGI NA JUA UWEZI KUWA OPEN KILA KITU ILA NAKUSHAURI JITAHIDI ILI UTAONA MKONO WA MUNGU JUU YAKO

3)))JITAHIDI KUWA CHINI MWENZAKO AKIWA JUU..YULE NI BINADAMU AMEKUZWA NA WAZAZI WENGINE NA WALA SI DADAYAKO WA DAMU..HIVYO KILA MTU ANAKUWA ANA MAMBO YAKE SO KUMFANYA AWE DADAYAKO NI UPENDO WAKO JUU YAKE.....AKIWA AMEKASIRIKA WE KUWA CHINI IKIWEZEKANA WEKA KANDA YENU YA HARUSI AALAFU UONE KAMA AJAJA KUKTUPIA MTO WA CHUMBANI ...HAPO SI KWAMBA AMEKASIRIKA BALI ANASHUKURU NA ZAID AMEKUKUMBUSHA UNACHOFANYA CHUMBANI MANYIE HAPO MLIPO...KUWA MAKINI NA HILI..USIOGPE NA WALA SI USHAMBA..

4)))MSIOGOPE KUAMBIANA UKWELI...MTAKUFA NA PRESSURE NA KUTUONGEZEA MATANGAZO YA VIFO HAPA JF JUKU TUKIHUZUNIKA...AMEARIBBU MPE CHAKE ALALE NACHO AKIPENDA ATAMEZA AKIKASIRIKA ALALE NACHO KWA RAHA ZAKE....

5)))MSIKUBALI MLALE KITANDANI KAMA MAFISI AU MARUHANI WANASUBIRI KUWAINGIA WANADAMU...JARIBUNI KUMALIZA MATATIZO YENU MAPEMA KABLA AIJAITWA KESHO HAPO NDIPO FUTAA NA AMNI ITAKAPOWAJIA MAISHANI MWENU.......KWELI KUNA WENGINE HATA UMBEMBELEZE UMWAGIE MAJI YA KILIMANJARO KANUNA ....WE FANYA MAJUKUMU UNAYOTAKIWA UCHOTE BARAKA ZAKO..

6)))KUMBUKENI KUZAA KWA MPANGO :: HILI JAMBO NI MUHIMU SANA MUNGU AMEPENDA MJE KUIONGEZA NCHI LAKINI SI KUTESA WANANCHI...NATUMAINI HAPA MMENIELEWA WANANDOWA WOTE::::::BIBIE USPENDE KUTUMIA HAYA MADAWAA YA UZAZI KWENYE NDOA WENZIO WATAKUSAIDIA KUKUZALISHIA NATUMAINI UJUMBE UMEUPATA MAMA.....SOMENI NYAKATI FANYENI MAMBO..

7))KABLA YA KUMALIZIA MWISHO MSICHOKE KUOMBA MSAADA KWA WANA jf kama MLIVYOKUJA KUOMBA BARAKA ZETU HAPA ..WOTE NI BINADAMU TUMEUMBWA NA USO WA AIBU NDIO MAANA MUNGU AKATUWEKEA COMPUTER UKIWA IRAQ TUWEZE KUSAIDIANA BILA KUJUA WEWE NINANI..HIVYO KAMA UNAMATATIZO USICHOKE KUJIITA ""YAMENIKUTA"""
SI HATUUITAJI KUJUA NI NANI ILA UJUMBE TUMEPATA TUTASAIDIANA KWA UTAKACHOULIZA KIKIWA NDA NI YA UWEZO WETU IKIWA NJE TUTAKUPA MWONGOZE

)KUMBUKENI KUWAAKUMBUKA WAZAZI WENU HATA BAADA YA HARUSI HAO NDIO FARAJA ZENU..NDIO MAANA YAKIWAKUTA MNAKIMBILIA KUPIGA SIMU KWAO..WACHA..UTAMWACHA BABA NA MAMA NA KUMFWAATA MUMEO...AU MKEO....WASAIDIENI KADRI MTAKAVYOWEZA...SI KWASABABU MUMEO AMEKUOA ATI SIWEZI BABA MBONA UNANISUMBUA HIVYO MI NIKO BIZE NA MMUME WANGU SI UNAMKEO KOMA LAANA ULAANIWA...USIJE UKU....

9)))


NAWATAKIA KILA LA KHERI NA MUNGU AKUBARIKI KWA UAMUZI WAKO
 
Last edited by a moderator:

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
9,256
2,000
Jamani ndoa ni tamu tena pale mnapokuwa mnatambua mnapendana.

Mdogo wangu Maxence, jitahidi kukwepa kuingia mlango wa nyumba ndogo maana kwa kuwa nyumba ni ndogo mtu huingia akiwa ameinama na akitoka humo keshachoka hoi....

Naamini mlio mbali na Dar mtawasiliana naye ili awaconnect na kamati kwa ajili ya masuala ya maandalizi...... (mimi siyo msemaji am just advicing tu)
 

Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,852
0
Hongera Max, nakutakia kila lenye heri katika maandalizi na shughuli ifanikiwe. Nitakuwa huko miezi hiyo, nitauzengea huo mnuso.
 

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
834
250
Ni kweli inapobidi kusaidiana tusaidiane;halafu hili suala la hiari sidhani kama kuna mtu amelazimishwa kuchangia.
Kama vilevile unavyoweza kumpatia mtu zawadi,sidhani kama yule unayempatia ankulazimisha kumpatia zawadi na kama ikitokea hivyo basi hiyo siyo zawadi tena.
 

Kilinzibar

Senior Member
Mar 6, 2008
125
0
tunashukuru kwa taarifa ambazo ni nzuri sana hii ni step kubwa katika maisha ya mwanadamu,pongezi sana na kila lakheri.

sasa kuna utaratibu gani wa michango sizani kama ni issue mana sasa kuna M-pesa sasa twendeni na wakati no excuses hapo!!!!
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Maxence HONGERA.
HIVI NDIYO TUNACHANGIA VIPI?
NAWASHANGAA WANAOPINGA KUCHANGIA ARUSI ETI NI OMBA OMBA. KWANI AJABU NI IPI KUCHANGIA? HATA MAKANISANI NA MISIKITINI TUNACHANGIA BILA KULAZIMISHWA NA HATUPIGI KELELE JE HAPA AMBAPO TUNAMCHANGIA NDUGU YETU AMBAYE ANAHUDUMU JF TUSIWEZE KWELI? SISI NI FAMILIA MOJA.
ULISHA WAHI KUONA WAPI WANAFAMILIA WANAMTELEKEZA MWENZAO ANAPOOA?
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,965
2,000
Maxence HONGERA.
HIVI NDIYO TUNACHANGIA VIPI?
NAWASHANGAA WANAOPINGA KUCHANGIA ARUSI ETI NI OMBA OMBA. KWANI AJABU NI IPI KUCHANGIA? HATA MAKANISANI NA MISIKITINI TUNACHANGIA BILA KULAZIMISHWA NA HATUPIGI KELELE JE HAPA AMBAPO TUNAMCHANGIA NDUGU YETU AMBAYE ANAHUDUMU JF TUSIWEZE KWELI? SISI NI FAMILIA MOJA.
ULISHA WAHI KUONA WAPI WANAFAMILIA WANAMTELEKEZA MWENZAO ANAPOOA?
Mchukia fisadi,

Namba zangu zipo kwenye signature yangu na email yangu pia. Nashukuru kwa support niliyopata kwa wana JF wakiwemo hawa:

  1. FD & Family
  2. Mwafrika wa Kike
  3. Roya wa Roy
  4. John Mnyika
  5. Msanii
  6. Invincible na
  7. Dar si Lamu
 

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,235
2,000
Max,

hapo nyuma niliuliza......huo ubwabwa tutaula lini....maana wengine twataka sana kuhudhuria hiyo karamu.......is it still July au umeshabadili tarehe......zingatia wengine tunatokea mbali

......otherwise kwa waliokuchangia nawapa pongezi sana........taratibu tutajumuika nao
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom