Harusi ya Jerry Muro iligharimu milioni 62, thamani ya pete Dola 1,800, Suti Taxido

Ila bongo kwa mtu maarufu kama yeye ni kidogo sana. Kuna Dean of student UDSM-Business school aliifanya ya mwanaye mwaka jana iligharimu zaidi ya milioni 100 na bado michango mingine waliikataa

Harusi million 100 huko ni kukufuru. Kuna watoto wa mitaani wanakufa na njaa kwa nini wasitoe misaada huko? Hata Kama ni umaarufu imepitiliza kiwango. Ni mtazamo tu
 
Naomba nielimishwe....nini faida yake baada ya hapo???niliwahi kuhudhuria harusi nzuri saana....michango yote takriban 30m ilipelekwa kwenye nyumba za watoto yatima tofauti hapa Dar.Zawadi zote pia zilitolewa kwa nyumba za watoto yatima.tulikula chakula vizuri na vinywaji baridi tu.Ilipendeza saana.
 
Harusi na nyumba ni vitu viwili tofauti,hela ya harusi inavyopatikana ni tofauti na hela ya nyumba.Kwa position aliyopo Jerry Murro(maarufu) kufunga harusi ya gharama ni jambo la kawaida.anajuana na watu wengi wakubwa ambayo tunaweza sema ndio wanamuweka mjini sasa wewe ulitaka awaalike kwenye harusi ya mil 20 eti kwa sabab hana nyumba nzuri?au kwa sabab anakaa kwenye nyumba ya kawaida? Kila mtu ana malengo na kama alivyosema mwenyewe alipanga hii kitu for two years so kama amefanikiwa kufanya yake na wewe fanya yako.unajua ana plans gani kuhusu nyumba au gari?kesho akisema ana nyumba ya mil 600 utakuja tena hapa JF na kuandika kingine, kila mtu afight kivyake yeye kama kaiba na wew kaibe ufunge harusi yako ya mil 100 wakikudaka imekula kwako...thats all!

Well said mkuu, hiki kitu kimemtokea hta diamond kila cku watu walikuwa wanamtukana hapa kuwa mashauz kubao wakat kapanga sinza ss matokeo yake wameumbuka baada ya kuona kumbe ana mijengo ya maana tu lakin cha ajabu badala wasifie au wakae kimya ndo kwanza wamepata sababu za kuponda tena, duh kwel sisi wabongo ni furushi la misumari hatubebeki!!!
 
Back
Top Bottom