Harusi New York City na CHALLA, Sumbawanga

Hiyo harusi ya Marekani wala haioneshi furaha kihiivyo, imegubikwa na itifaki, urasimu, nk lakini wale wa uswazi ni full shangwe na full kujimwaga ujiwezavyo!
 
ya juu ni natural, ya chini ni artificial, wajuu expecting over 10 children wa chini expecting full of stress. acha wa enjoybana :smiling:
 
Naona bwana harusi wa challa kapewa zana za kulinda ndoa, fimbo ilokaushwa kwa moshi:target:
 
Ndoa ni zaidi ya mavazi!!! Ni kile cha kweli kilicho ndani ya mioyo yenu!!! Love forever hata kama chini ya mti.
 
mmmh......bora ya NYC.....matatizo ya nini......
Bora ya Sumbawanga sababu sio ya kununua ,ya NYC na haitadumu kwa kuwa'' masharti na vigezo vya pesa na umaarufu vimezaingatiwa'' kwa saana tu badala ya penzi la ukweli,pia ya S'wanga ni organic bana ilihali ya NYC ni GMO
 
Hiyo ya juu inaonesha maisha halisi ya watanzania wengi, hapo gharama yake kidogo sana.
 
Bora hata bibi harusi, bwana harusi suti imemvaa, katupia is right maana hajavaa.

Kwa taarifa yako hiyo suti inafahamika vyema kijijini hapo kuliko hata ofisi ya kata!huyo jomba hapo nyuma yeye anasindikiza suti!ahakikishe mara tu maharusi wafikapo nyumbani suti inafuliwa na kukunjwa vizuri tayari kwa harusi nyingine mtaa wa pili keshokutwa!!maisha bora kabisa.
 
Back
Top Bottom