Harusi iliyovamiwa ilikuwa ya watoto

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MAHARUSI waliovamiwa na majambazi wilayani Tarime katika Kijiji cha Kinesi mwishoni mwa wiki hii, ambapo washerehekeaji watano wakiwemo ndugu na marafiki wa karibu wa maharusi hao waliuawa huku wengine wanane wakijeruhiwa, imebainika walikuwa watoto.

Aidha mmoja wa waliouawa aliyetajwa kwa jina la Wangwe Wambura, ameelezewa kuwa ni kaka mkubwa wa bwana harusi ambaye alikuwa kama baba mlezi na katika sherehe hiyo alikuwa katika nafasi ya baba mkwe wa bibi harusi.

Mdogo wa maharusi (jina limehifadhiwa), aliiambia HabariLeo Jumapili jana kwamba bwana harusi huyo ana umri wa miaka 16, na alikuwa amefunga pingu za maisha kupitia ndoa ya kimila na mkewe ambaye amemaliza darasa la saba mwaka jana.

Licha ya umri mdogo wa bwana harusi huyo, mtoa habari huyo alisema pia alikuwa hajamaliza elimu ya msingi kwa kuwa alikatisha masomo kutokana na machafuko yaliyosababishwa na mapigano ya ukoo ambayo yamekuwa yakitokea katika wilaya hiyo mara kwa mara.

“(Bwana harusi) aliacha shule akiwa darasa la sita kwa sababu ya vita lakini bibi harusi alimaliza darasa la saba mwaka jana,” alisema kijana huyo.

Alipoulizwa mwaka ambao bwana harusi aliacha shule alisema hana uhakika. Akisimulia namna maharusi hao walivyonusurika katika tukio hilo, alisema baada ya kusikia milio ya risasi, maharusi hao walikimbilia katika uzio wa majani karibu na nyumba hiyo na kulala chini katika miba.

“Waliposikia tu milio ya risasi, walikimbilia kwenye uzio na kulala kwenye miba kwa saa nzima hivi na hiyo ndiyo iliyokuwa pona yao,” alisema.

Licha ya kaka wa bwana harusi ambaye ndiye mlezi wa maharusi hao, pia watoto wawili wa mlezi huyo (majina yao yamehifadhiwa), walijeruhiwa vibaya kwa risasi za moto katika tukio hilo.

“Mmoja (wa watoto wa mlezi huyo) alipigwa risasi tumboni na tayari amefanyiwa operesheni lakini tunashukuru Mungu kuwa wanaendelea vizuri ingawa baba yetu ametuacha tukiwa bado wadogo,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.

Shemeji wa bwana harusi, Rhobi Mwita ambaye ni mmoja wa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, amesimulia kuwa kundi la watu wenye silaha waliwavamia wakiwa kwenye harusi hiyo saa tano usiku na kuanza kuwashambulia kwa risasi na mapanga.

“Walikuwa wamevaa makoti kama polisi na mmoja alinishika shingo ili aninyonge lakini mwenzake akamzuia, ndipo akanipiga na chuma kizito na mateke huku akinitaka nimpe simu ya mkononi,” alisimulia Mwita.

Mwita alisema baada ya kutimiza malengo yao wavamizi hao walipora ng’ombe watano, punda mmoja na baiskeli moja na kisha kutokomea katika vijiji vya jirani.

“Yaani maharusi wamekuwa na huzuni kubwa baada ya sherehe yao kugeuka kuwa msiba mkubwa na wana mawazo sana kwa kweli,” alisema ndugu moja wa maheremu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Hadi jana asubuhi Jeshi la Polisi lilikuwa limeimarisha ulinzi katika maeneo ya tukio. Hata hivyo hakukuwa na taarifa za kukamatwa kwa mtuhumiwa yeyote.

“ Sasa hivi naingia Kenya sidhani kama tutaelewana naomba mtupe nafasi kidogo tutasema kitu,” Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Tarime, Consitantine Masawe aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu.

Msako wa watuhumiwa unafanyika kwa kushirikiana na nchi jirani ya Kenya kwa kuwa katika vijiji ambako tukio hilo lilifanyika ni mpakani ambako jamii ya watu kutoka Kenya na Tanzania hushirikiana katika shughuli za kila siku.

Hata hivyo viongozi wa kijamii wakiwemo madiwani na Mbunge wa Tarime, Charles Mwera wametupia lawama Polisi wakisema imeshindwa kudhibiti wimbi la wizi wa mifugo katika wilaya hiyo jambo ambalo wanadai ndicho chanzo cha mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Wengine waliouawa katika tukio hilo ambao uhusiano wao na maharusi bado haujajulikana ni pamoja na Mwita Mathias na Marwa Miyoro, ambao ni wakazi wa kijiji hicho cha Kinesi na Matoka Sokoni, ambaye ni mkazi wa Nyamwaga na Magaiwa Makindi ambaye haijajulikana eneo alikotoka.

Baadhi ya waliojeruhiwa ni Chaha Makena (19), Wangwe Wambura, Mwikwabe Marwa (70) ambaye alipigwa risasi ya mgongoni mkazi wa Genkuru, Mfugo Kiura (30), mkazi wa Nyamwaga ambaye alijeruhiwa kichwani na mkono wake wa kulia kukatwa panga hadi kudondoka na Morisi Wambura mkazi wa Kinesi ambaye umri wake haujajulikana.
 
issue ya harusi ni nyninge na issue ya kuuwawa ni nyingine, huu ndio uandishi wenye mashaka maana ukisoma heading ni kama vile mwandishi alikuwa nataka kusema kuwa waliuawa kwa sababu ya kufunga arusi ili ngali ni watoto,
point ya maana hapa ni mauaji na either angekuwa mkubwa au ni mtoto, ni kitendo chenye kuogopesha na kutia hofu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom