Haruna Niyonzima aongea kuhusu kutimka Yanga, mpaka sasa hajaongeza mkataba

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
Niyonzima anadai hawezi kuweka wazi kama amesaini na klabu yoyote kwani mpaka sasa mkataba wake na Yanga bado haujamalizika.

Hata hivyo anadai bado hajaongeza mkataba na klabu hiyo.

Kwa sasa Haruna yupo likizo na anaomba apewe muda apumzike na familia mbali na kuhusishwa na mambo ya mitandaoni.
~Kirerenya~

 

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,124
2,000
Juzi hapa, kwenye jukwaa hili hili walipatikana waropokaji kutoka sokoni wakasema mil100 zimempeleka Niyonzima sokoni. Leo habari zinakuja upya kwa mtindo wa 'Barua ya FIFA', hivi mnaniamini sasa niliposema Simba kichwani na miguuni sawa?

Nyie pigeni makelele weeeee, Yanga kimya kimya unatafutwa ubingwa wa 28
 

Che mittoga

JF-Expert Member
Mar 28, 2017
5,080
2,000
Mwacheni Fundi aendelee na Maisha. Kiiza aliwambia, hata msajili messi hamuwezi kuwa Champ Of VPL
We jamaa yangu kweli una mapenzi na Yanga.
Ivi hujui kwamba mafanikio ya Yanga hii misimu mitatu yalitokana na Mwenyekiti wenu Y. Manji kutumia pesa yake kufanya usajiri mzuri.
Mpira ni pesa ndugu
Simba haikuwa vizuri kipesa kwani haikuwekeza pesa nyingi kama Yanga.
Manji ndio siri ya mafanikio yenu.
Simba tulikuwa na hali mbaya hadi akina Kesi wakawa wanauza mechi. Akina Kiiza walikuwa wanagoma kucheza na hawakwenda Songea kucheza na Majimaji.
Mrudisheni Manji la sivyo wote tutafanana tu uwanjani.
Pia nashanga kipindi hicho ni kwa nini hamkufanikiwa katika ngazi ya Afrika kwani hakika mlikuwa na kikosi Bora sana kuwahi kutokea.
Au ndo nyinyi ni WAHAPAHAPA
 

moudgulf

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
83,334
2,000
Niyonzima anadai hawezi kuweka wazi kama amesaini na klabu yoyote kwani mpaka sasa mkataba wake na Yanga bado haujamalizika.

Hata hivyo anadai bado hajaongeza mkataba na klabu hiyo.

Kwa sasa Haruna yupo likizo na anaomba apewe muda apumzike na familia mbali na kuhusishwa na mambo ya mitandaoni.
~Kirerenya~

"Lugha ya kibiashara hiyo. Yanga ongeza dau au laa natimkia Simba". Pesa ya usajili haijawahi kumwacha mchezaji salama
 

Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,000
2,000
Huyu jamaa Yanga wamwache tu aende! Ametusaidia kiasi cha kutosha kwa hiyo kama anataka kwenda timu nyingine aende zake! Ni msumbufu sana huyu Mnyarwanda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom