Harufu ya ufisadi stendi mpya Mbezi: Je, CHADEMA ilishindwa kuisimamia Serikali ipasavyo?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,722
2,000
Rais Magufuli amesema kuna harufu ya ufisadi katika ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya mikoani na nchi jirani ambapo nyongeza ya Sh bilioni 20 haielewki ina tija gani.

Rais Magufuli ameahidi kulichunguza suala hilo na kuchukua hatua stahiki.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa inaongozwa na Chadema na baadae CCM.

Ndio kusema wakati mradi unasainiwa meya wa jiji alikuwa Isaya Mwita wa Chadema ambao ndio wasimamizi wa serikali kwenye miradi inayosimamiwa na jiji.

Je, nyongeza hii ya sh bilioni 20 ilikuwa na baraka za baraza la madiwani lililosheheni madiwani wa Chadema?

Maendeleo hayana vyama!
 

tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
11,741
2,000
Mshiki uko na sonona kali sana,mkurugenzi ndio mshika pesa fanya fasta chukua boda ukamuulize hilo swali, mimi ntalipa hela ya boda.

Yani mwaka huu mtatema ulimi meko huko kimara na mbezi hawataki kumsikia pamoja na kujipitisha sana njia hiyo.

Yani majimbo ya Dar mnapigwa spana size zote
.
IMG_20201008_023927.jpeg
 

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
1,981
2,000
Je, CCM ambao ni wapiganaji dhidi ya rushwa na ufisadi walilishugulikiaje hili suala?
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,137
2,000
Ilani ya Chama cha Mapinduzi iliahidi kutekeleza mradi huu na viongozi wa mkoa wa Dsm ngazi ya mkoa, wilaya yaani RC, RAS, DC na wale wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam kila siku bila kujali ni Idd el fitr , Jumamosi au Jumapili walikuwa wanashinda saiti kuhakikisha unaisha ili Magufuli akabidhiwe mradi wake
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,488
2,000
Siku ya matokeo utakapokuwa umepigwa, rudisha hizo spana na useme zimekurudia mwenyewe,

Mgombea wenu anajilazimisha kupendwa dar ila watu hawana time nae, sasa ameanza kununua vitu sokoni,

Sisi tunamshauri uchaguzi ukiisha aendelee na hiyo kazi ya kutumwa mboga sokoni,

Yule mama wa kikurya huwa hawataki ujinga ujinga.
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,100
2,000
CHADEMA wako bize na wizi kumbuka walotaka kupiga pesa kina Mnyika na Kubenea wakapewa za uso sasa kimenuka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom