Harufu ya ufisadi mkubwa katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,653
Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli, ilianzisha utaratibu wa kuwapatia wajasiariamali wadogo vitambulisho maalum vya wajasiriamali kwa bei ya Shilingi 20,000/-, ambapo katika awamu ya kwanza Mwezi Desemba, 2018 Serikali ilitoa jumla ya Vitambulisho 670,000 ambapo kila Mkuu wa Mkoa Nchini alipewa vitambulisho 25, 000 avigawe kwa wafanyabiashara wadogo katika Mikoa yao.



Hivi vitambulisho vilianza kama vitambulisho vya wamachinga na mama ntilie. Ila baadaye ikafikia kila aina ya biashara na huduma ndogo ndogo ni lazima iwe na kitambulisho. Tulisikia mpaka watumishi wa ndani, wavuvu, mafundi garage etc nao wanatakiwa kuwa na vitambulisho.

Wafanyabiashara wengi walidhani hivi vitambulisho ukipewa ndyo miaka yote kitakuwa kikitambulika. Kumbe kila baada ya mwaka mmoja kinaexpire na wanatakiwa wanunue kingine.

Hivi sasa vimeletwa vitambulisho vingine na kila mfanyabiashara anatakiwa akanunue tena. Yani atoe 20,000 apewe kitambulisho kingine.

Hii ni kama kodi ya kila mwaka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ambayo inakusanywa na inaenda kwenye mfuko wa mtu binafsi.

Kwa mwaka wa kwanza inasemekana viliuzwa vitambulisho almost million 1.

Tukiassume viliuzwa 670,000 tu vilivyotolewa awamu ya kwanza, Maana yake ofisi ya Rais chini ya Tamisemi ilipokea kama 13b kutokana na mauzo ya vitambulisho vya wajasiriamali.

Mwaka huu tena anategemea kupokea kiasi icho au zaidi ya icho kutokana na vitambulisho vya wajasiliamali vinavyotolewa kwa awamu ya pili.


Kumbuka waliopewa jukumu la kuviuza/ kuvigawa kwa wafanyabiashara wadogo kuanzia TRA, wakuu wa mkoa, wakuu wa wilaya mpaka watendaji ni watumishi wa serikali na wanalipwa mshahara na serikali sio JPM au ofisi ya Rais.

Ingawa hii pesa inakusanywa na TRA, ila inapelekwa kwenye ofisi ya Rais kulipia gharama za utengenezaji na uandaaji wa hivi vitambulisho ambao hatujui vinatengenezwa kwa gharama gani na pesa kutoka mfuko wa nani.

Kuna harufu ya ufisadi tena mkubwa sabubu hakuna sheria ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo iloyopitishwa, au inatoa description (ufafanuzi) kuwa ni mfanyabiashara mdogo na kiwango gani anatakiwa kulipa na anapata wapi hivyo vitambulisho, kwa bei gani na vifungu gani vya sheria vinamlinda anapokuwa na ivyo vitambulisho. Na mapato ya hivi vitambulisho yanakwenda wapi.

Pia vitambulisho hivi ni kama kodi kwa mfanyabiashara maana anatakiwa kurenew kila mwaka kwa gharama ya 20,000Tsh.

Tunatambua kuwa mapato na matumizi katika office ya Rais hayakaguliwi na hakuna wa kuhoji. Ili kuondoa taaruki au harufu hii ya ufisadi, inatakiwa vitambulisho hivi viwe chini ya mamlaka maalumu inayokaguliwa na mapato yanayokusanywa jamumuishwe katika mapato ya TRA yanayotokana na kodi.
 

Attachments

  • JPM Katengeneza Mwenyewe Vitambulisho vya Machinga!_360p.mp4
    16.6 MB
Hivyo vitambulisho alivitoa Magufuli tena akiwa Ikulu, watu wakauliza huu ni mradi wa nani?!

Bado nasubiri jibu.
 
Hivyo vitambulisho alivitoa Magufuli tena akiwa Ikulu, watu wakauliza huu ni mradi wa nani?!

Bado nasubiri jibu.
Jibu gani sasa unasubiri wakati alisema anatengeneza mwenyewe na hakuna mamlaka chini yake inayoweza kataa kuvitambua.
 
Unashangaa hilo mkuu?!

Nenda kule kata ya IKUTI RUNGWE.
Mfanyabiashara mdogo Analipa tsh20000 kwa mwaka.

Na analipa tsh20000 ya maendeleo ya kijiji kwa mwaka kama mke na mume.

Kama huna inabidi uende kwenye maendeleo ya kujitolea.

HAPO ishu sio pesa wanazotoa ila ishu wanazifanyia nini?

Hakuna soko lenye kueleweka kama soko bali kuna magenge.
Hakuna stand ya kijiji kwa ajili magari yanayopakia mazao.
Hakuna choo chochote cha kijiji.

Ukumbuke kijiji kipo katika barabara kuu ya mkoa mbeya na songwe.

Ni kijiji ambacho kinaingiza pato kwa taifa vizuri.
LAKINI MPAKA SASA BARABARA NI YA VUMBI MVUA IKINYESHA BIASHARA YA MAGARI IMEKATA.

30000 KICHWA KIMOJA KWA MWAKA KIJIJI BADO KINATUMIA MAJI YA MTO RUMBE KWA MATUMIZI MBALIMBALI YA NYUMBANI.

#Naipongeza_Ccm.
 
Mlizoea kuchukua 1000 za wamachinga kila siku halafu mnaingiza mifukoni mwenu
 
Mlizoea kuchukua 1000 za wamachinga kila siku halafu mnaingiza mifukoni mwenu
Hata leo zinachukuliwa . Nenda kwennye masoko uone kama hawalipi ushuru wa eneo. Kama hawalipi hawapati eneo la kupanga biashara zao.
 
Back
Top Bottom