Harufu ya ufisadi kwenye ulipaji wa fine za makosa barabarani

Transparence

Member
Sep 23, 2016
22
13
Mh. Rais alisisitiza ukifanya Malipo yeyote dai risiti ili serikali ipate mapato! Sasa ni kwanini askari wa barabarani wakitoza fine hawatoi risiti na wanaishia kukupa notification na hela mtu umelipa? tuna uhakika gani kwamba hizo hela zinafika serikalini?
 
Cha ajabu ni kuwa ukikomaa nao kwenda kulipia kituoni wanakupa risiti lakini barabarani mkuu hizo hela ni zao.
 
ukiuliza mara kitabu kiko kimoja or mara vimeisha au ooh nenda kafate kituoni! Risiti ni haki ya Mteja ili tuendelee kuchangia serikali yetu
 
Traffic hawatumii tena zile machine za EFD wanatoa risiti za mkono.
 
Baba,Kaka,Dada,Mjomba,Shangazi,Bibi na Babu huu ni mshipa uliomshinda fisi.Binafsi mara kadhaa nimelipa faini bila risiti nikiuliza naambiwa kachukue ofiini ??????.

Ukisafiri njia ya Moshi to Arusha utasimamishwa zaidi ya mara tano maswali ni yale yale Road licence,lleseni,insurance.......Hadi unashangaa hivi hawa trafic polisi hawana kazi za kufanya.
 
Haya ndio mambo ya kuyapigia kelele, mi niliwahi kukamatwa Mkoa flani kwa over speed, wakati nataka kulipa wananiambia hawana risiti wanipe askari niende naye kituoni, nikawaambia si kuna option ya kulipa kwa Simu Mpessa (Tigo and M pesa) wakasema wao hawajui, nilipojaribu kuwaelekeza wakasena wanachotaka wao ni cash, nilivyoenda kituoni kufuata risiti wakaniambia niifate jumatatu and ilikuwa Jumamosi siku ya kukamatwa na mi sio Mkazi wa Mkoa huo.

Hili suala Serikali ilifanyie kazi, nasubiri nikamatwe kwa mara ya pili ili tupotezeane muda na tufundishane sheria.
 
Cha ajabu ni kuwa ukikomaa nao kwenda kulipia kituoni wanakupa risiti lakini barabarani mkuu hizo hela ni zao.


Serikali nayo imeridhika kabisa na mfumo huo, kiukweli nchi yetu ina vyanzo vingi vya mapato ila mifumo yetu ya ukusanyaji ndiyo mibovu kabisa, chukua mfano mdogo wa ukiukwaji wa sheria za barabarani, kuna madereva wengi sana mijini wanakiuka sheria za barabarani, kama vile kupakia na kushusha abiria katika maeneo yasiyoruhusiwa, hakuna mfumo wa kuwanasa hao madereva na wakalipa fine, mimi ningeshauri kuwepo vituo maalumu vya kulipia hizo faini na visiishiwe receipt hata siku moja, maana inapotokea weakness kidogo tu wahuni wanapigia hela hapo,
 
Cha ajabu ni kuwa ukikomaa nao kwenda kulipia kituoni wanakupa risiti lakini barabarani mkuu hizo hela ni zao.
Sasa ndallo si uwe unakomaa nao hivyo hivyo? Maana traffic ni wakamataji tu, pesa wakiipokea inawasilishwa kwa mhasibu ambaye huandaa erv receipt. Haiwezekani traffic akawa na vitabu vyote viwili, check and balance itasumbua.

Na kumbuka vitabu vinne vya notification paper ni kitabu kimoja cha erv. Erv hubaki ofsini kwa mhasibu ambaye kila siku lazima apeleke makusanyo benki akaunt za hazina.

Kama ule mfumo wa majaribio ukikubali, basi utata utakoma.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom