Harufu ya kujuana kwenye ubalozi ushahidi waongezeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harufu ya kujuana kwenye ubalozi ushahidi waongezeka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpayukaji, Dec 9, 2011.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Maura W. Mwingira ni afisa ubalozi New York-AugustineMwingira mmojawapo wa mawaziri kwenye serikali ya awamu ya kwanza na mkuu wamkoa kwenye serikali ya awamu ya pili na rafiki mkubwa wa Benjamin Mkapa.
  Mindi Kasiga ni afisa habari wizara ya mambo ya nchi zanje. Kasiga ni jina linalohusiana na Rahma Kharoos Kasiga ambaye wengi wamemjuaalipoibuka baada ya rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani akituhumiwa kuwanyumba yake ndogo. Wapo wanaosema kuwa anahusiana na Anna Mkapa au wote wawilil.
  Jacob Msekwa ni afisa ubalozi wa Tanzania nchini Sweden-Pius Msekwa ni makamu mwenyekiti wa CCM. Na kuna majina kama Erick Msekwa namarehemu Julius Msekwa. Msekwa wawili walio hai bado wanaishi Ulaya Erick akifanyakazi kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa.
  Ali Karume baloziItalia- mtoto wa rais wa zamani Abeid Karume.
  Radhia Msuya balozi Afrika Kusini- hatuna uhakika kamaMsuya huyu na Msuya waziri mkuu wa zamani wana uhusiano.
  Joyce Kafanabo ubalozi wa Tanzania Marekani- kapt. PeterKafanabo alikuwa kigogo wa CCM aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa mbali mbali nchini.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Subiri @ New York atakuja kukanusha.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  where is,@@ny city?
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Comrade, umejitahidi kuoanisha majina lakini siyo kila ulichokiandika ni chakweli, kapten Kafanabo hajawahi kuwa mkuu wa mkoa wowowe hapa TZ, cptn alikuwa journalist harafu alikuwa chapombe kupindukia, cptn alikufa kwa kugongwa na gari pale afrikana- gari likiendeshwa na Padri wa Tegeta. Aliyekuwa mkuu wa Mkoa(Rukwa) na baadae mkiti wa CCM - DSm ni kakayake.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,865
  Likes Received: 6,216
  Trophy Points: 280
  dah!. . . Sijui nikatafute undugu wa kuchanjia na mnene mmoja
   
 6. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Gama uko sawa. Nilimaanisha kaka yake ambaye bahati mbaya sikupata jina lake. Ila nakumbuka aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Singida. Kimsingi sijasema ninachoandika ni asilimia mia. Ninachotaka kufanya ni kuweka dukuduku ili wenye habari zaidi waongezee. Hivyo kama kuna mwenye data nyingine naye amwage. Maana uzoefu umeonyesha kuwa mitandao hii ni silaha nzuri dhidi ya ufisadi na uchafu mwingine kama huu wa kujuana.
   
 7. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Radhia Msuya hana uhusiano na akina Msuya although inawezekana ameolewa na kina Msuya....Radhia ni mdogo wake Asha Rose Migiro.....kabla hajawa full balozi alikuwa London kwenye ubalozi wetu Uk akiwa afisa ubalozi msaidizi.....pia ana ndg yake mwingine Fatma Mtengeti anafanya hapo ubalozini Uk.....kwahio dhana ya kujuana au kuwa na jina kubwa ndio uwe ubalozini ni ukweli mtupu kwa asilimia 1000......tukifanya utafiti wa kina ukweli utaonekana wote...karibu sana le baharia le mutu uchangie hoja teehteeh...kwikwikwi
   
Loading...