Harufu ya ajabu kwenye kitunguu maji,pilipili na mahindi mabichi

Boutafrica

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
949
2,065
Serikali tunaomba mtumie wataalamu wa kilimo mchunguze kuna kitu siyo cha kawaida kinaendelea kwenye sekta ya kilimo.

Kuna harufu ya ajabu inajitokeza isiyo ya kawaida kwenye kitunguu maji,pilipili (mwendokasi)na mahindi mabichi.Hii harufu sijui ni ya kitu gani na sijui inasababishwa na nini lakini nina wasiwasi isijekuwa tunakula sumu bila kujijua na mbaya zaidi huenda yakatokea maafa ya halaiki kama tutaendelea kudharau hili.

Kama tunavyojua kitunguu,pilipili na mahindi hv vitu huwa na harufu yake ya asili lakin sikuhz za karibu naona haya mazao yanatoa harufu flani hv ya tofauti lakini harufu hiyo inafanana,sasa huenda tunaendelea kula sumu bila kujua.

Binafsi sidhan kama harufu hiyo ni salama kwa sababu haiwezekan mazao matatu tofauti yapoteze harufu yake ya asili yawe yanatoa harufu mbaya ya aina moja.
Mimi nimegundua harufu hii katika vitu hv vitatu lakini huenda kuna mazao mengine yana hii kitu.

Nashindwa kuielezea hii harufu lakini ukitaka kugundua hiki ninachosema,nenda sokoni nunua hivyo vitu nenda navyo nyumban kavitumie then utaelewa ninachosema.
 
Ata nyanya pia mkuu.. especially kwenye msimu wa nyanya. Nadhani ni mbolea na dawa zinazotumika
 
Mkuu hata carrot pia naona Zina harufu ya ajabu. Serkali ichunguze. Na Kuna kipindi hapo nyuma hoho zilikua chungu nadhan ni madawa wanayotumia kwenye kilimo
 
Back
Top Bottom