Harufu na moshi kutoka soko la samaki la Ferry zinawakera Ikulu-Waziri wa Uvuvi

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Leo waziri wa uvuvi na mifugo alitembelea soko la samaki la kimataifa la ferry maeneo ya Kigamboni na kuwalalamikia wakaanga samaki kuwa harufu na moshi wa samaki unamkera sana maana unawanyima watu wa pale Ikulu ya Magogoni...
Anaendelea kwa kusema kuwa hata wageni wanaotembelea pale Ikulu hawakai kwa raha sababu ya hizo harufu
Hivi huyu waziri ametumia akili zake sawasawa katika kuongelea hii hoja? Mi nilidhani angeenda pale na mkakati wa namna ya kuhakikisha mazingira yale ni safi na angesema serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa harufu na moshi huo unadhibitiwa
Hebu changieni wanaJF
Source...ITV news
 
Sidhani kama kweli waziri huyu anajua au anaamini alilolizungumza. Wageni kukerwa na hiyo harufu,mmmh, hapana si wote except George Bush! Alipokuja Bush mwaka 2008 hiyo harufu ilipotezwa kabisa for almost wiki tatu. Baada ya hapo hali ilirudi kama zamani. Je ina maana kwamba kumbe ile harufu ni uzembe fulani. Tujiulize ziara ya Bush ilitumia dawa gani kui-suspend hiyo harufu, na kwa nini kwa wakati huo tu? Je wakaaji wa pale ikulu wa kila siku walikuwa wanalijua hilo ila hawakuwa na mbinu mbadala?
 
kila waziri anajifanya ameanza kazi kwa ziara za kushtukiza na kuongea utumbo,tumemsikia shukuru,na wengine wengi mpaka walioliwa na fataki. Badala ya kuongelea ni jinsi gani washirikiane kubolesha mazingira ya soko,sijamuelewa vizuri huyu mustachi.
 
Hao ndo wale wanaopewa kazi kwakujuana maana hata common sense hana wala sio hatumii!!!
Wahamishe ikulu kuikimbia hiyo harufu kama hawawezi kuleta mabadiliko yakuikimbiza yenyewe!
 
Naomba kuuliza, hivi lile bomba la maji taka linalovuja miongo kadhaa sasa na inayochafua bahari hadi inabadilika rangi haiwezi ikawa ndo chanzo kikubwa zaidi cha 'harufu' kuliko Ferry na samaki?
 
Hamisheni Ikulu kama mnakereka.......
Nendeni Manzese, ila baadaye msilalamike vibaka wakiwakwapulia vyupi vyenu......
Uzuri wa Bongo hata rais anapata tabu kutokana na maisha valu-valu tunayoishi.......
Mara tairi imepata pancha kwenye msafara, mara mafuta mchafu kwenye gari, bado tu kukwapuliwa simu.....
 
Hahahaaaa unajuaje labia kishakwapuliwa cheni hawasemi tu
 
Najua pale ni soko la kuuzia samaki. Tunakaangia nyumbani na kama ni kuhifadhi watoe majokofu ya kuhifadhia hao samaki. Mpeni alternative, moshi unaingia pale Ikulu na inawezekana hiyo ndiyo assignment ya kwanza kwake
 
amaa kweli tumepata mawaziri...eti wote wanaiga style ya magufuli ya kushitukiza, i mean sfari za ghafla...tatizo ni kwamba hata wakishtukiza wanaongea utumbo. hivi hizi ni safari za kushtukiza kweli? mbona wanakuwa wanamsururu wa waandishi wa habari ili wapate coverage?
Shame on them!!!
 
Leo waziri wa uvuvi na mifugo alitembelea soko la samaki la kimataifa la ferry maeneo ya Kigamboni na kuwalalamikia wakaanga samaki kuwa harufu na moshi wa samaki unamkera sana maana unawanyima watu wa pale Ikulu ya Magogoni...
Anaendelea kwa kusema kuwa hata wageni wanaotembelea pale Ikulu hawakai kwa raha sababu ya hizo harufu
Hivi huyu waziri ametumia akili zake sawasawa katika kuongelea hii hoja? Mi nilidhani angeenda pale na mkakati wa namna ya kuhakikisha mazingira yale ni safi na angesema serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa harufu na moshi huo unadhibitiwa
Hebu changieni wanaJF
Source...ITV news

Ndio haya tu aliyoongea waziri au ni sehemu ya mazungumzo yake.????!!!!! Kama kweli Inashangaza

Sasa waziri na yeye akiwa mtu wa kuelezea matatizo wananchi wengine wafanyaje? Hilo soko kumbe lipo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Ngoja tumpe idea anatakiwa awe sehemu ya solution

  • Shirikiana na wizara husika waweke miundombinu ya majiko ya gesi mbapo wakangaji samaki watakodishwa kwa masaa kwa bei nafuu kabisa kukaanga samaki wao. Tatizo la moshi litapungua
  • Harufu sio tatizo halisi ni matokeoa ya tatio halisi amablo ni Usafi. Kwenye menagement ya utawala wa soka iwepo idara ya safi na mku wa kitengo apewe majukumu ya usafi

Wajapan wanaweza kulia wakirudi kuchki soko walilojenga. Badala yakukuta maendeleo watakuta linarudi nyuma
 
Wauze BMW mbili za ikulu na hela inayopatikana lijengwe jiko la geso hiyo sehemu.

Hii itasidia hakutakuwa na moshi tena ikulu, mazingira hayaharibiwa kwa kuharibu miti etc na raisi wetu bado atabakia na fleet ya Landcruiser, Nissan na Benz.

Waziri kwa kweli statement yako ya jana ni kituko cha mwaka.
 
Najua pale ni soko la kuuzia samaki. Tunakaangia nyumbani na kama ni kuhifadhi watoe majokofu ya kuhifadhia hao samaki. Mpeni alternative, moshi unaingia pale Ikulu na inawezekana hiyo ndiyo assignment ya kwanza kwake

Ferry ni soko la wabichi na waliokaangwa......kwa hiyo jamani punguzeni kukaanga moshi unatukera ati!
 
Nilipomsikiliza anaongea sikuamini kama ni waziri au mpiga debe wa mwaloni. Rais unapokuwa na waziri zezeta kama huyu ujue umewaliza waliokuchagua. Hicho ndio kiwango chake cha juu cha kufikiri, tutegemee sampuli ya aina hiyo itufikishe kwenye asali na maziwa.Tumekwisha watanzania. Hao ndio viongozi waliopewa nyadhifa sio kwa umahiri wao kuongoza bali kwa fadhila fulani. Pole Kikwete. Hatutegemei mtu wako huyo anaweza kujenga hoja ili kukushauri kufanya maamuzi yenye maana, ameachwa nyuma mno kwenye enzi za kifalme ambapo kumtetea mfalme ilifaa sana kupalilia ugali wako na watoto wako enzi hizo.

Ushauri wa bure, apigwe chini kwenye dirisha la mabadiliko kama hajui kusoma nyakati ukutani.
 
Hao ndo wale wanaopewa kazi kwakujuana maana hata common sense hana wala sio hatumii!!!
Wahamishe ikulu kuikimbia hiyo harufu kama hawawezi kuleta mabadiliko yakuikimbiza yenyewe!

Wahamishie ikulu dodoma:A S-alert1:
 
Leo waziri wa uvuvi na mifugo alitembelea soko la samaki la kimataifa la ferry maeneo ya Kigamboni na kuwalalamikia wakaanga samaki kuwa harufu na moshi wa samaki unamkera sana maana unawanyima watu wa pale Ikulu ya Magogoni...
Anaendelea kwa kusema kuwa hata wageni wanaotembelea pale Ikulu hawakai kwa raha sababu ya hizo harufu
Hivi huyu waziri ametumia akili zake sawasawa katika kuongelea hii hoja? Mi nilidhani angeenda pale na mkakati wa namna ya kuhakikisha mazingira yale ni safi na angesema serikali imejipangaje kuhakikisha kuwa harufu na moshi huo unadhibitiwa
Hebu changieni wanaJF
Source...ITV news
Yeye ndo anaona kero sana kwa kuwa na mamlaka ya kuwaagiza wengine waondoe hiyo harufu. Na wavuvi na wakaanga samaki wasemewe na nani? au wao pua zao hazioni kero. Dawa yake ipo jikoni
 
Back
Top Bottom