Tatizo la kuwa na harufu mbaya kinywani (bad breath) - Chanzo, dawa za kuzuia na ushauri

Mbinu za kusugua meno

Toothbrush_0.jpg




Kusugua meno yako ni swala rahisi. Mbinu hii huwa na athari kubwa sana katika afya ya meno yako na afya yako kwa jumla.

Mbinu bora ya kusugua meno:

  • Kwa kutumia mswaki na kwa upole laini na itakayotoshea mdomoni mwako.
  • Mswaki kubwa hautafika kwenye meno ya nyuma ilhali ile ndogo itakufanya kutumia wakati mwingi sana katika kusugua meno. Ukiwa wahitaji usaidizi katika uchaguzi wa mswaki, zungumza na daktari wako wa meno.
  • Tumia dawa ya meno iliyo na floraidi.
  • Watoto wanapaswa kutumia kiasi kidogo cha dawa ya meno na watu wazima watie dawa ya meno inayolingana na urefu wa nywele wa mswaki.
  • Sugua meno yako angalau mara mbili kwa siku, unapoamka na kabla ya kulala. Ikiwezekana sugua meno yako baada ya kula chakula. Kama hauwezi, sugua mdomo wako hasa baada ya kula vyakula vya sukari.
  • Sugua meno kwa dakika mbili. Angalia kwenye saa kujua muda uliotumia.
  • Badilisha mswaki wako baada ya miezi mitatu au unywele ukijikunja.
Kumbuka kusugua pande zote za meno:

  • Sugua meno yako kutoka kutoka nyuma hadi mbele kwa upole.
  • Sugua karibu na ufizi kwa mwendo wa mviringo; ili unywele wa mswaki ufike sehemu ambapo meno na ufizi zinakutania mahali ambapo chembechembe ya chakula haionekani
  • Sugua sehemu zote za meno, sehemu ya nje, sehemu ya kutafuna chakula na sehemu ya ndani
  • Tumia unywele wa juu wa mswaki kusafisha sehemu ya ndani ya meno yako ya juu; kwa mtindo wa juu na chini
  • Sugua ulimi wako kwa upole ili kuondoa vijidudu au viini vinavyosababisha pumzi au harufu mbaya.
 
Unga wa mdalasini kijiko kimoja, unga wa pilipili manja robo kijiko, unga wa tangawizi nusu kijiko, tia kwenye kopo/chupa kavu, changanya , iwe na mfuniko, kila siku unapopiga mswaki ongeza kiasi kidogo juu ya dawa ya mswaki.
 
Jinsi ya kutibu pumzi mbaya Wanaosumbuliwa na pumzi mbaya wakati mwingine huwa ni vigumu njia ya kuchunguza kwa watu wenyewe. Kwa Sababu ya kuwa njia hii inaweza kuwa vigumu kwa sababu cavity ya mdomo ni ya kushikamana na pua zetu na ya ufunguzi uliloko katika nyuma ya maana kinywa cavity.Our ya harufu unaweza filter nje viungo na mzunguko wake na kama vile unaweza kabisa kuzuia nje au kupuuza kwetu wenyewe uwezekano harufu ya pumzi.

Ili kujua jinsi ya kutibu harufu ya pumzi mbaya sisi na kujifunza na doa baadhi ya kumweleza dalili Daktari . Dalili hutegemea sababu ya msingi ya pumzi yako mbaya kama vile,kinywa maambukizi,njia ya upumuaji na maambukizi na baadhi ya aina ya ugonjwa kama vile ugonjwa wa kisukari, mapafu, figo kushindwa au ugonjwa wa ini pia inaweza kuwa kuwajibika kwa kesi yako ya pumzi mbaya ya harufu .Jinsi ya kutibu pumzi mbaya

inaweza pia kuwa chini ya kitu kweli rahisi kama maskini kuboresha usafi wa meno.
Kama una shida katika kutafuta jinsi ya kutibu pumzi mbaya au pumzi yako mbaya ni ukiongozana na dalili zifuatazo:
Homa,Kikohozi kwamba inazalisha kamasi,Kupauka pua kutekeleza au Kuumwa koo ya kuzungumza na daktari wako. Kukumbuka, ni kawaida rahisi sana kupata sababu ya pumzi yako mbaya,usione aibu kumwambia Daktari wako ukweli, kwa mfano kama sisi wote tunakabiliwa na tatizo hili kwa wakati mmoja au mwingine.
Kuangalia video ya chini ya kujua jinsi ya kutibu pumzi mbaya. Dr. Katz TheraBreath simulizi Suuza, 16-Ounce chupa (Pakiti ya 2
 
Sidhani kama kupiga mswaki ni suluhisho tosha la hili swala.Ningependa kujua kama kuna dawa yoyote itakayo tumika katika kulidhibiti tatizo ili la kunuka mdomo.

Tafadhali msaada wenu
.
 
Nenda kwa daktari wa meno wasafishe meno, tunatakiwa tuwe tunaenda kusafisha meno mara mbili kwa mwaka kila baada miezi sita.

Ukienda huko kama kuna jino bovu watakutibu lakini kama hamna, hio kusafishwa itakusaidia na uendelee kusafisha meno vizuri; piga mswaki mara mbili kwa siku na pia toa mabaki ya vyakula kwenye meno (flossing) mara mbili kwa siku.ku-floss ni muhimu kuliko hata kupiga mswaki kwani hii huondoa mabaki ya vyakula vilivyonasa kwenye meno ambavyo huwezi kutoa kwa kupiga mswaki.

Vyakula vikikaa sana kwenye meno ndio inafanya bacteria wazaliane na kusababisha mdomo wako kunuka na kukuletea magonjwa mengine ya meno kama fizi kuvimba na kuanza kutoa damu mpaka meno yanalegea na kung'oka.

Kila la kheri, kamuone daktari mapema mkuu.
 
Tatizo letu sisi Wa Tanganyika hatuamini kitu eti mpa akiseme Mzungu au Aseme Daktari. Lakini akisema MziziMkavu au wewe Ropam wanataka WaTanganyika Prof ndio maana sisi Wa Tanganyika hatuendele hjata kidogo tumezoea kutawaliwa kiakali na wazungu.
 
Tatizo la kunuka mdomo wakati mwingine halitokani na kutopiga mswaki, kama vile mnuka vikwapa haimaanishi haogi. Hili tatizo linahitaji madaktari waliobobea katika taaluma na kichwa.

Lingine ni kweli linatokana na kutopiga mswaki hasa kama huoshi ulimi mara nyingi unakuwa na ugaga ambao hutoa aharufu hasa kwenye koromeo, hivyo unahitaji kusugua hadi utapike.

Hivyo unaweza kuanza kwa kupiga mswaki ulimi kama huna meno yaliyooza, ikishindikana waone wataalamu wa vinywa.

Pole sana maana hilo jambo linakera sana, lakini ni vizuri wewe umelijua wengi wanaonuka midomo hawajitambui na wanapenda sana kunong'oneza jamabo ambalo linawakera wengine bila wewe kujua.
 
Mkuu ropam Tatizo letu sisi Wa Tanganyika hatuamini kitu eti mpa akiseme Mzungu au Aseme Daktari. Lakini akisema MziziMkavu au wewe Ropam wanataka WaTanganyika Prof ndio maana sisi Wa Tanganyika hatuendele hjata kidogo tumezoea kutawaliwa kiakali na wazungu .

Upo sahihi MziziMkavu..mda mchache tu uliopita nilikuwa jukwaa la science, kuna jamaa kaanzisha thread ya wakenya fulani wamedesign tablet computer yao.Sasa sikilizia wabongo tulivyodiss ile thread, wakati angekuwa marehemu steve jobs na apple yake wangekuwa ndo wamedesign hiyo tablet pc wote tungeitukuza...issue ni kwamba wabongo tumekosa uzalendo kabisa kwenye uwezo na ufahamu miongoni mwetu!
 
Upo sahihi MziziMkavu..mda mchache tu uliopita nilikuwa jukwaa la science, kuna jamaa kaanzisha thread ya wakenya fulani wamedesign tablet computer yao....sasa sikilizia wabongo tulivyodiss ile thread, wakati angekuwa marehemu steve jobs na apple yake wangekuwa ndo wamedesign hiyo tablet pc wote tungeitukuza...issue ni kwamba wabongo tumekosa uzalendo kabisa kwenye uwezo na ufahamu miongoni mwetu!


Tuna tabia ya kuwababaikia Wazungu tu kitu amefanya Mzungu tu basi ndio tunakubali lakini angelifanya Mtu Mweusi kitu hicho chicho alichofanya Mzungu tunaleta dharau ama kweli (MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO)
 
Sidhani kama kupiga mswaki ni suluhisho tosha la hili swala..ningependa kujua kama kunadawa yoyote itakayo tumika katika kulidhibit tatizo ili la kunuka mdomo...tafadhali msaada wenu

Kama bahati vile,leo leo asubuhi nimetoka kwa jamaa alikuwa anamimina presentation juu ya matatizo kama hayo.Kwa upande wa harufu mdomoni.Tatizo ni ukozefu wa onion na kwa utaalam maji yanayopatikana maeneo ya milimani yana onion za kutosha.

Sina hakika kama maji ya Kilimanjaro yanatokea kwenye mlima huo, kama ni kweli basi yanaweza kuwa na 30-60% ya onion contents per 1cm[SUP]2[/SUP] area.

Ndio maana American Foundations for ground water and minerals Inst wameformulate onion paper iko kama litmus white paper, unaadd kwenye maji then unakunywa. Harufu yote inatoweka.

Inbox me will help you if you dont mind.
 
Wana forum pamoja na madokta, tatizo langu ni kuwa mdomo hutoa harufu mbaya ingawa huwa napiga mswaki atleast mara 2 kwa siku. Nimejaribu kutumia hydrogen peroxide lakini wapi. Je naweza kupata tiba ya kienyeji/kitaalamu kumaliza tatizo hili? Je harufu hii inasababishwa na nini? Naombeni mchango wenu.
 
Sina utaalam sana lakini wengine wametumia maziwa mtindi kunywa angalau mara mbili kwa siku yanasaidia.
 
Hiyo hali inaitwa halitosis .husababishwa na uvutaji wa sigara, chakula kama vitungu, nyama, etc, bacteria infection . Jitaidi unaposafisha jitaidi usafishe ulimi wako vizuri, kama hiyo hali bado inaendelea angali kama unavuta sigara uache . Nenda hospital ukapima mapafu yako au fisutra perforation kati ya oesophagus na tumbo (stomach)
 
Hiyo hali inaitwa halitosis .husababishwa na uvutaji wa sigara, chakula kama vitungu, nyama, etc, bacteria infection . Jitaidi unaposafisha jitaidi usafishe ulimi wako vizuri, kama hiyo hali bado inaendelea angali kama unavuta sigara uache . Nenda hospital ukapima mapafu yako au fisutra perforation kati ya oesophagus na tumbo (stomach)

Thanks alot Ndokeji, however mi sivuti sigara na wakati wa kupiga mswaki huwa nasugua ulimi vilivyo. Anyway, nitafuata ushauri wako to the letter.
 
Inaweza ikawa pia infections kwenye sinuses ambazo ni chamber ndani ya pua ambazo huvimba(sinusitis) na kusababisha kamasi ambazo husaidia wadudu kuzaliana hivyo kusababisha harufu kutoka unapopumua, pia kamasi hizo hupita nyuma ya pua na kutokea mdomoni(post nasal drip) karibia na koo hivyo kufanya bacteria waoteane hapo na kusababisha harufu mbaya mdomoni ukitaka kutest ingiza vidole tofouti sehemu mbalimbali za ulimi uone kama sehemu karibu na koo ndio inanuka au la.

Matibabu inategemea na cause kama ni fungal, or bacteria sinusitis.kama tatizo lako limeanzia mdomoni jaribu listerine gaggle lakini ikishindwa ujue tatizo labda limeanzia puani(sinusitis) muone dactari for further checkup.
 
Inawezekana moja kati ya meno yako limeoza, Check kwa matabibu meno.

Pia watu wengi sana hatujui namna ya kupiga mswaki, Ni vizuri pia ukapata elimu ya jinsi ya kupiga mswaki.

Kwa kifupi ukilifikisha jambo hili kwa wataalam wa meno utasaidika
 
Harufu mbaya mdomoni kwanza inatokana na kushindwa kufanya usafi wa kinywa vizuri ,yaani unaweza kuwa unasafisha kinywa bila ya kutumia dawa za meno(toothpaste) ua dawa ya kuoshea kinywa ( mouth wash) na ukukumbuke kusafisha ulimi kwa siku hizi ipo miswaki maalimu ya kusafishia ulimi,kwani mabaki ya chakula yanyobaki huoza kwenye ulimi na kuleta harufu mabaya,piga mswaki kila unapomaliza kula chakula,hususani wakati umemaliza kula chakula cha usiku,usiende kulala bila ya kusafisha kinywa.

Usile chakula kingi wakati wa usiku kwani watu wangine mifumo yao ya kuyayusha chakula ni dhaifu kwa Hali hiyo chakula huchacha na kuoza( ingestion) na kusababisha harufu mbaya,ukijaribu yote hayo na harufu ikiwa bado inatoka ujue unaugonjwa kwa kitaalam unaitwa halitosis ,hii ni kutokana na kunasa kwa chakula katika kamfuko kadogo katika njia ya kupitishia chakula( oesophageal hernia) matibabu yake ni kumuona Daktari bingwa wa masikio ,koo na pua (ENT)atakupima Kama kuna uwezekano atakupasua na kurekebisha udhaifu katika koo lako.

Daktari aliyefunzwa kutumia chombo cha endoscope anaweza kutumia chombo hicho kutambua Kama una kasoro ya aina yeyote katika koo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom